Tuesday 18 August 2015

WEWE NI AINA GANI?

Kila mwanamke ana mtazamo wake tofauti kuhusiana na ndoa yake. Kuanzia wale wanaokuwa makini kuhusu mume hadi wale ambao hajali lolote.

Je, wewe ni mwanamke yupi kati ya hawa?

MKE MLEAJI.
Mume akiwa na hitaji lolote hulitimiziwa. Mume akiwa mgonjwa ajue chicken soup hakosi.
Anakuwekea love note kwenye bag lako la kazini au lunch yako ya kubeba kazini. Anafanya kazi zote za nyumbani kama kuosha vyombo na kufua nguo bila malalamiko.
Pia anajua mume anachoka na kazi hivyo jambo la msingi ni kuhakikisha nyumbani kuna amani hivyo mke wa aina hii hujichosha na kazi.
Wanawake wa aina hii huchoka sana na kutoa kwa waume zao kila kitu kwa jina la amani.
Tatizo la mke wa aina hii akiamua kugombana anagombana kwelikweli.

MKE KAMA MAMA..
unamtengenezea breakfast ya nguvu mumeo asubuhi, unahakikisha unamkumbusha ratiba za mambo anatakiwa kuhudhuria.
Unamkumbusha kumeza dawa alizopewa na daktari.
Unapanga nguo zake za kazini kila siku.
Unahakikisha anakula chakula tena balance diet hata kama hataki vegetables unahakikisha anakula.
Unafanya yote hayo kuhakikisha unamtunza.
Na wanaume wenye mke wa aina hii wakati mwingine hufurahia kwa kuwa wanaume wengi hupenda kutunzwa ingawa wakati mwingine huudhika Kutokana na tabia zao za kukefyakefya kama mama na hakuna mume anayependa kuoa mke ambaye ni kama mama yake.
Mke ni mke na mama ni mama na haipaswi kuchanganywa.
Tatizo la mke wa aina hii humzoesha vibaya mume kiasi kwamba anakuwa tegemezi na mke hujikuta mume amekuwa kama mtoto mwingine.

MKE KAMA BINTI..
Ni mwanamke ambaye hawezi kufanya vitu mwenyewe au peke yake.
Hawezi hata kubadilisha bulbu, hawezi hata kuwasha Computer au TV mpya kuifanya ifanye kazi.
Kulipa bills bila msaada wa mume, hawezi kufan bank hadi mumewe awepo. Kila anachofanya anajiona hawezi hadi mumewe awepo.
Anakuwa kama vile ni binti ambaye anahitaji directions zote kutoka kwa baba yake.
Mke wa aina hii huvumiliwa sana mwanzo wa mahusiano hata hivyo mahusiano yanavyozidi kwenda mume hujiona ni usumbufu.
Wanawake wa aina hii inawezekana wakati watoto walikuwa neglected na hawakupata attention kutoka kwa wazazi wao hivyo hujikuta hajiamini kila analofanya.

MKE BOSI..
Mke wa aina hii huweza kumpa mume orodha ya vitu anatakiwa kufanya, mume hupewa taratibu za kusaidia kazi za nyumbani. Huweza kutoa amri za nani awe rafiki wa mume wake au la. Anampa mume kikomo cha muda anatakiwa kutazama Tv au kujihusisha na masuala ya sports na rafiki zake.
Wanawake wengi wa nchi zilizoendelea wapo kwenye kundi hili.
Hii tabia huondoa uhuru wa mwanaume na hivyo anaweza kuwa disconnected kwani mwanaume huhisi anaondolewa heshima yake ya kuwa mwanaume.

MKE SUPER..
mwanaume hafanyi kazi yoyote ya nyumbani kama kupika na kufua labda mwanaume aamue mwenyewe.
Anahakikisha watoto wanapata kila wanachohitaji.
Hapa haijalishi mke wa aina hii ana kazi yenye kipato kuliko mume wake au la.
Mwanamke wa aina hii huchoshwa na kazi kiasi kwamba anakosa na usingizi.
Pia mwanamke wa aina hii huweza kujihisi mume hana appreciation kitu ambacho kinaweza kumfanya ajisikia hana furaha na matokeo yake anaweza asiwe na mawasiliano mazuri na mume.

MKE KILA KITU NI MTOTO/WATOTO..
Wakati mwingine kuwa mzazi huongeza stress katika ndoa.
Na tatizo kubwa ni kwamba baada ya mwanamke kuwa na mtoto hujikuta mume hana nafasi tena kwake.
Mke hujikuta ana hitaji kubwa la kutumia muda au uwezo wake kwa mtoto kuliko mume.
Wanawake wa aina hii hutumia muda wote kwa ajili ya kuhudumia watoto na ni wapo wonderful kuitwa mama ingawa husahau kuhusu mume.
Ukweli ni kwamba hakuna ubaya wa kuwa na watoto, jambo la msingi ni kuwa na muda na mtoto na pia kuwa na muda na mume.

No comments:

Post a Comment