Tuesday 18 August 2015

NI VIZURI KUBADILISHA MAZINGIRA.

Kubadilisha mazingira au eneo au mahali ni jambo la msingi sana kwa ajili ya wanandoa kufurahia ukaribu kimapenzi (intimacy).
Inajulikana kwamba kwa wanandoa kwenda mbali na nje ya nyumbani kwao kama Motel huweza kuwafanya kupata msisimko mkubwa na tofauti wa kimapenzi.

Sababu za msingi ni kwamba:
Kunakuwa na privacy kwa wahusika yaani mke na mume wanaweza kuvaa wanavyotaka.
Pia kunakuwa na uhuru kwani mkiwa sita kwa sita unaweza kupiga kelele, unaweza kuugulia kimapenzi, mnaweza kucheza, kucheka bila majirani wala watoto kuwasikia.

Hakuna kuingiliwa na kitu chochote kama ndugu kuwatembelea au watoto kuwaita kwa ajili ya kitu chochote. Pia kama simu zimezimwa ndo mnakuwa dunia yenu wenyewe.

Zaidi na kubwa kuliko yote ni kwamba wanandoa huwa mbali na masumbufu ya maisha kama vile kupika, kuangalia watoto, kutembelewa na ndugu au majirani nk.

Ukiona suala la tendo la ndoa linakupa maumivu kwa maana kwamba hakuna anayeridhika au wewe mwenyewe huridhiki ufahamu kwamba na ndoa yako itakuwa na maumivu.
Hata hivyo hujachelewa kurekebisha mambo, anza sasa.
Wanandoa wengi hujikuta katika wakati mgumu wa kuwa karibu kimapenzi, inawezekana mmoja au wote hujisikia wamechoka muda wote, au wanajisikia msongo wa mawazo au basi tu hakuna mwenye hamu na mwenzake, no feelings.
Haitakiwi kuwa hivyo, naamini ingekuwa hivyo wala msingekubaliana kuoana.

No comments:

Post a Comment