Saturday 8 August 2015

NDOA SI YA MAJARIBIO.

Kuna ushauri mmoja tu muhimu sana kwa yule anaetafuta mchumba ili awe mke au mume nao ni kwamba usikimbilie au kuingia haraka bila kuchunguza kwamba huyo unaetaka kuingia naye kwani ukiingia hakuna haraka ya kutoka kwani ni shimo ambalo kutoka ni hadi kifo.
Kama wewe ni binti au msichana au mwanamke ambaye unatamani kuolewa jambo la msingi ni kuhakikisha umejua tabia kabla ya kuamua kuoana naye.
Na kama wewe ni mvulana au mwanaume ambaye unatamani kuoa jambo la msingi ni kuhakikisha unajua fika tabia ya huyo binti au mwanamke unateaka kumuoa.
Kuna mambo muhimu sana ambayo binadamu hufanya uamuzi na uamuzi wake huweza kuathiri maisha yake hapa duniani na maisha yake baada ya kufa, moja ya jambo ilo ni ndoa.
Ndoa si safari ya majaribio kwamba nikiingia haraka haraka basi hata kutoka nitatoka haraka haraka, usijidanganye!
Adhabu ya kuingia kizembezembe kwenye ndoa ni kuvumilia maisha ya huzuni na maumivu maisha yako yote yaliyobaki duniani na huyo utakaye oana naye.
Kabla ya kuoa au kuolewa tumia muda wa kutosha kutafakari majaribu, matatizo, shida na magumu yote ambayo hutokea kwa wanandoa na kwamba una uhakika mwanaume au mwanamke unayetaka kuingia naye kwenye ndoa ana hizo sifa ya kusaidiana na wewe kuhakikisha ndoa inakuwa kitu cha Baraka kwako.
Jiulize mwenyewe kama mwanamke au binti je, nina uwezo wa kimwanamke, stamina na tabia ya kuweza kubeba majukumu ya ndoa kwa uangalifu maisha yako yote ya ndoa?
Na kama ni mvulana au mwanaume jiulize je, ninao uwezo na tabia ya kuweza kuwa baba wa watoto na kichwa cha nyumba au familia na kuwa mwanaume bora kwa mke wangu maisha yangu yote yaliyobaki duniani na mwanamke naenda kumuoa?
Unaweza kuingia harakaharaka kwenye ndoa kwa kuwa unatamani kuolewa; kumbuka ukiingia kwenye ndoa hakuna kutoka wala hakuna haraka ya kutoka ni hadi kifo kitakapowatenganisha.

No comments:

Post a Comment