Tuesday 18 August 2015

JE,UNATIMIZIWA MAHITAJI YAKO KTK MAHUSIANO?

MAHITAJI MUHIMU KATIKA MAHUSIANO YOYOTE YA KIMAPENZI

Ni kitu cha msingi sana kuhakikisha katika mahusiano mahitaji yako yanajulikana na kueleweka kwa mwenzako.

Mahitaji yako yakijulikana na kutekelezwa kawaida unajisikia vizuri na kujiona upo salama katika hayo mahusiano iwe ndoa au uchumba.

Partner wako hawezi kusoma mind (wanaume mara nyingi tunasoma magazeti na si nini mwanamke anawaza kichwani) na kujua mahitaji yako, ndiyo maana kuna wakati unahitaji wewe mwenyewe kumueleza ili aweze kukupa kile unahitaji, ingawa ni kweli wapo ambao wameshakata tamaa kabisa kwamba hata nikimwambia najua hatafanya, bado hilo si jibu kwani jambo la msingi ni wewe kuongea na mpenzi wako na kumueleza nini unahitaji kutoka kwake tena kwa busara na hekima au kwa upendo.

Mahitaji muhimu katika mahusiano ya ndoa yamegawanyika katika sehemu kuu tano nazo ni

1.Mahitaji ya kihisia.

2.Mahitaji ya Kimwili.

.3.Mahitaji ya kijamii

4.Mahitaji ya kiroho.

5.Mahitaji ya kiusalama.

Mfano wa muhitaji ya kihisia ni kama ifuatavyo

Hitaji la kusikia na kuambiwa unapendwa, una thamani kwa mpenzi wako, kujisikia wewe ni muhimu katika maisha yake, kujisikia wewe ni mali yake, hitaji la kujisikia unaheshimiwa wewe binafsi na yeye, hitaji la kujisikia mpenzi wako anakuhitaji zaidi ya kazi zingine unazofanya kama kulea watoto nk, hitaji la kujisikia wewe ni mtu wa kwanza kwake kwa kila kitu, kujisikia wewe ni mtu maalumu kwake, hitaji la kujisikia unaaminiwa, unakubalika na pia anakupenda na kukuhitaji, hitaji la kujisikia ana appreciate kwa jinsi ulivyo na unavyofanya nk

Mfano wa muhitaji ya kimwili ni kama ifuatavyo:

Hitaji la kuguswa (touched and caressed), kupata busu, kukumbatiwa, na kushikwa hata kubebwa akiweza, hitaji la kujiona unaruhusiwa kuwa naye katika faragha yake, kujisikia huru kuwa naye kimwili pale unapo muhitaji, kujisikia wewe ni sehemu yake pale mnapowasiliana na watu wengine, kutiwa moyo, kuwa na tendo la ndoa linalokuridhisha kama upo kwenye ndoa.

Mfano mahitaji ya kiroho ni kama ifuatavyo:

Hitaji la kuheshimiwa na kusaidiwa mambo yako ya kiroho, kuheshimiwa kwa tofauti za kiroho zilizopo.

Kuwa na wakati wa pamoja kuomba pamoja huku mmekumbatiana au kushikana mikono na kuwa kitu kimoja kwa Mungu wenu.

Mahitaji ya kihisia ni kama ifuatavyo:

Hitaji la kupenda na kupendwa.

Hitaji la kuwa mali ya mume wako au mke wako na kuwa na maana ya maisha pamoja naye.

Hitaji na kujiamini (self positive image)

Hitaji la kuwa na usiri yaani kuwa mwenyewe bila kuingiliwa.

Mahitaji ya kijamii ni kama ifuatavyo:

Hitaji la urafiki na mke au mume pamoja na wengine wanaowazunguka.

Hitaji la uhuru wa kujihusisha na masuala ya jamii bila kukatazwa na mke au mume.

Mahitaji ya kiusalama ni kama ifuatavyo:

Hitaji la kujisikia salama na hatari yoyote.

Hitaji la kujisikia salama kwamba mahitaji yote katika ndoa yanatimizwa.

No comments:

Post a Comment