Wednesday 12 August 2015

TENDO LA NDOA NI ZAWADI SI HAKI.

Mungu alitoa sex kama zawadi kwa waliooana.
Ametoa zawadi ya sex ili kutufundisha kuhusu yeye na uhusiano wake na sisi.
Utendaji wa sex ni picha ya muunganiko kwa kutoa vyote (vile tulivyo) kwa mwenzako (mke au mume) na pia ni picha ya kumkubali kumpokea mwenzako (wote) kama alivyo kwako.

Kuna faida wazi kabisa kwa uhusiano wa tendo la ndoa kwa mke na mume kama vile afya ya mishipa, kupunguza maumivu, kufanya MP kuwa stable, kupunguza depression (unyonge wa kihisia), kupunguza (stress) msongo wa mawazo na kuongeza kuridhika kwa mahusiano ya ndoa.

Mungu anawapa uhuru wanandoa kunywa na kufurahi raha ya mapenzi kila mmoja kwa mwenzake kama wanandoa, hata hivyo sababu za kiroho na kisayansi haziwezi kutumika kama silaha ya mwanandoa mwingine kumthibiti mwenzake.
Uwezo wa kimapenzi kati ya mke na mume bado ni zawadi ambayo tunatakiwa kupeana bure na kwa kupenda na kwa moyo wa furaha (kutoa na kupokea kila mmoja kwa mwenzake katika ndoa).
Pale mwanandoa mmoja anapokuwa na mtazamo kwamba tendo la ndoa ni haki basi kunakusinyaa kwa aina fulani katika mahusiano huanza kujitokeza.
Mke hawezi kuwa na raha ya mapenzi katika ndoa kama mume atakuwa ni mtu wa kulazimisha na kutaka kwa nguvu kama haki yake (demanding) na pia si raha sana pale mke anapotoa tendo la ndoa kwa sababu anawajibika kutoa hata kama hakuwa tayari.

Tendo la ndoa linaloridhisha (great sex and satisfying sex) ni pale kila mwandoa anakuwa amejiadabisha kutoa kwa uhuru mwili wake kwa mwenzake.
Unapotoa kwa uhuru mwili wako kwa mume au mke wako na kupokea mwili wake kwa uhuru unaipa ndoa kitu sahihi cha asili yake na Mungu hufurahia na kutoa kibali.


No comments:

Post a Comment