Tuesday 18 August 2015

NI KUWEKANA WAZI TU.

Kawaida linapokuja suala la mapenzi opposite attract na the same repel kwa maana kwamba mara nyingi huwa tunavutiwa na strength za mwingine kwa kuwa hufanana na weakness zetu.
Watu ambao hutuvutia sana ni wale ambao huonesha strength katika maeneo ambayo sisi tupo weak.
Ukikutana na mtu wa jinsia tofauti na wewe na mkawa pamoja kwa muda mrefu pamoja na ukavutwa kutokana na strength zake ambazo zinakubaliana kwenye weakness zako penzi huzaliwa na baadae inaweza kuwa ndoa.

Ndoa ni kuwekana wazi.
Wakati Bwana harusi na Bibi harusi wanaposimama mbele ya Mhubiri kanisani na kutoa ahadi zao kwa Mungu na wageni wote walioalikwa huwa wanaahidiana kwamba
“Ninakuahidi kukupenda na kukunyenyekea kwa muda wote wa uhai wetu”

Hii ina maana kwamba maharusi huwa wanakazia kwamba kwa kuwa nakubali kiapo chako na unyenyekevu wako kwangu leo basi nitajifunua kwako mzimamzima kuanzia sasa si kimwili tu bali kisaikolojia pia kwani hadi hapa nimejidhihirisha/nimejifunua kwako katika upande ule wa mazuri tu (strength) kuhusu mimi.
Sasa kwa kuwa tunaoana nitajiweka wazi kwako mzimamzima na nina imani kubwa na wewe kwamba utaendelea kunipenda kama nilivyo.
Ndoa ni kuwekana wazi, ni kila mmoja kujidhihirisha kwa mwenzake kama alivyo pamoja na weaknesses zake.
Vitu vyote ambavyo vilikuwa vimejificha wakati wa uchumba hadi honeymoon basi kuanza kwa ndoa vyote huwa mezani juu kwa kila mmoja kuona.
Na hapo ndipo kwenye mtihani wa kwanza wa wanandoa wapya.
Honeymoon siyo residence ya kudumu ya ndoa, baada ya honeymoon (na wengine hata wakati wa honeymoon) wanandoa wapya hushikwa na mshangao wa partner anavyobadilika na kuwa kama mwingine kabisa.
Ukweli ni kwamba unapoona partner wako anaonekana kama mwingine tofauti na yule wa wakati wa uchumba, ukweli ni kwamba sasa matching inaanza, kufahamiana kikwelikweli kunaanza na wenye hekima na busara huwa makini katika kukabiliana na hizo tofauti na kuendelea kusherehekea hizo tofauti kwa upendo na kuvumiliana kwani huwezi kumbadilisha na kumbadilisha ni kupoteza muda wako.

No comments:

Post a Comment