Wednesday 12 August 2015

MAPENZI..a.k.a MAHUSIANO.

Je, umewahi kujiuliza ni nini siri ya mahusiano yanayodumu kwa muda mrefu, miaka nenda rudi na wahusika wakawa na furaha na kicheko bila unafiki?

Jitahidi kufanya yafuatayo naamini mahusiano yako yatakuwa imara na yenye afya

Hakikisha unasifia zaidi kuliko kulaumu.
Ukiwa na rafiki zako hakikisha unaongea mambo 2 au 3 mazuri kuhusu mpenzi wako au mke wako au mume wako.
Kumbuka kwamba kufanya vitu kila mtu kwa tofauti ni kitu cha kawaida kwani kuna njia nyingi sana za kumenya kiazi au kukunja nguo.

Hakikisha mnakuwa na muda wa pamoja na mpenzi wako.
Kama hujaoa au kuolewa hakikisha unaoana na mwanaume au mwanamke ambaye unapenda kumsikiliza na anavyoongea.
Kumbuka ndoa wakati mwingine ni kitanda cha maua ya waridi na wakati mwingine ndoa ni kitanda cha miiba.

Kumbuka zawadi nzuri sana kwa watoto wako ni kumpenda mama yao.
Pia kumbuka kuhakikisha unajihusisha vizuri na kazi ndogondogo za nyumbani kama ni mwanaume kama vile kufua nguo, kusafisha nyumba nk.

Ukiona kuna uwezekana wa kuzipiga kikwelikweli basi hakikisha mnapigana mkiwa uchi! Serious!
Kubali, kutokukubaliana.
Usitamke kabisa neno talaka
Usiende kulala huku umekasirika labda iwe ni saa tisa usiku na umechoka huwezi kufanya chochote.


Mawasiliano mazuri ni ufunguo wa ndoa na mahusiano yako.
Usisahau kusema “Nakupenda”
Uwe na kimbelembele cha kusema “Nimekosa nisamehe’
Hakikisha ndugu (inlaws) wanakaa mbali na ndoa yako

Usilinganishe ndoa yako au mahusiano yako na wengine kwani unachokiona nje haina maana kinaweza kupatikana ndani.

Hakikisha si kitanda kilekile, milalo ileile, chumba kilekile, nyumba ileile, wakati uleule wa kufanya mapenzi na mke wako au mume wako kwani tofauti huleta maana.
Mwisho!
Uhusiano wako na Mungu ni muhimu sana katika mahusiano, Mungu ndiye mwenye upendo hivyo unavyozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo unavyozidi kuwa na upendo na mtu unayejua kupenda.
Mafanikio ya ndoa yoyote yanauhusiano mkubwa sana na uelewa kuhusu Mungu ni nani katika maisha yako.
Usipuuze ...

No comments:

Post a Comment