Thursday 22 October 2015

HAYA NI MUHIMU BAADA YA KUMALIZA TENDO LA NDOA.

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia.
 
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa.
 
Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukia kwake kisha kuuchapa usingizi.
 
Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila 
yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.
 
1.KUOGA PAMOJA.

Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapowasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.
 
Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
 
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.
 
2.KUSIFIANA.

Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.
Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza.
Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.
 
3.KUELEKEZANA.

Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika

4.ZUNGUMZIENI MAISHA.

Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla.
 
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa.
 

Friday 16 October 2015

BADO MAPENZI YANAKUTESA?..1

Ni wazi kwamba mapenzi yanachukua nafasi kubwa sana katika maisha ya binadamu, na ipo dhahiri kwamba mapenzi yanaweza kuleta furaha maishani mwako lakini wakati huohuo yanaweza kuleta maumivu, mateso na karaha.

Watu wengi sana bado wanalizwa na mapenzi na hii ni kwa sababu hawafuati kanuni sahihi ya mapenzi, ndiyo, mapenzi yana kanuni zake.

Kwa bahati mbaya kabisa, kwa sasa mapenzi yamegeuzwa na kuwa kama kitu cha kujaribu au kufanyia biashara na ndiyo maana yanawatesa wengi. Lakini ni kwanini mapenzi  yaendelee kututesa?  au ni kwa sababu hatujui maana halisi ya mapenzi.

MAPENZI NI NINI?
Katika hali ya kawaida, mapenzi hayaelezeki kuwa ni nini. Ni vigumu sana mtu kukueleza maana ya mapenzi ndiyo maana kila mtu ana uelewa tofauti juu ya suala hilo.

Mtaalamu mmoja wa masuala ya mapenzi aliwahi kuyaelezea mapenzi ndani ya kitabu chake cha More About Love, ambapo alisema; ‘Love is natural feelings, which take place from the deepest part of your heart upon somebody or something else’ akimaanisha kuwa mapenzi ni hisia za asili ambazo huchukua nafasi kutoka sehemu ya ndani kabisa ya moyo juu ya mtu au kitu chochote. Tena bila kuwa na visingizio au masharti ya aina yoyote.

HISIA NI NINI?
Huu  ni msukumo wa vichochezi katika homoni za  ndani ya mwili ambazo hutokea kutokana na  mazingira husika.
Lakini huwa tofauti kati ya mtu na mtu na ndiyo maana watu hutofautiana madaraja ya kupenda.

Mfano halisi ni kwamba, utakuta mtu anapenda sana wanawake weupe, lakini mwingine hataki hata kuwaona.
 Lakini mapenzi siyo mawazo au uamuzi wa mtu, bali mapenzi ni hisia ambazo hutokea pasipo uamuzi wa mtu.

Kutokana na hali hiyo, utasikia mtu akisema ‘sijui nimempendea nini huyu mwanaume’ ni kweli yeye hajaamua lakini hisia zimefanya awe hivyo.

USIRUHUSU  MAPENZI YAKUTESE
Kwa nini mapenzi yakuumize? Unakosea wapi, kwanini ukataliwe kila mara? Haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza kuhusu mateso ya mapenzi.

Kamwe katika maisha yako usiruhusu mapenzi yakutese, najua yawezekana kila mpenzi unayempata haudumu naye, wewe ni mtu wa kulia kila siku, hujawahi kufurahia maisha hataa siku moja, jipange upya.

Thamini na jali zaidi maisha yako kwanza, fikiria kipi ni bora kati ya mapenzi na maisha yako, ni kipi kilitangulia? Kama maisha ndiyo yalitangulia  kwa nini usijijenge kwanza kimaisha ndipo mengine yafuate?

Hata kama unateswa na mtu unayempenda kwa dhati, hata kama ni mzuri kushinda malaika, kwani bila yeye maisha hayaendi? Si kweli na kama unaweza kuishi bila yeye kwa nini akutese namna hiyo?

Hakuna kitu kinachouma kama mapenzi endapo utakosea kanauni zake, ukaruhusu moyo wote kuelekea huko, hakika yatakutesa.

Itaendelea....

BADO UNATESWA NA MAPENZI?

Yawezekana hadi sasa bado kuna mtu anakusumbua, umejaribu kumbembeleza lakini hataki kukubaliana na wewe, huyo hakufai.

Mapenzi hayapo ili yatutese,  badala yake mapenzi yapo kwa ajili ya kutupa faraja maishani mwetu.

Muondoe kabisa akilini mwako mtu wa aina hiyo, kwani atakufanya uyaone maisha kwa mtazamo hasi jambo ambalo siyo zuri.

TUFANYEJE ILI MAPENZI YASITUTESE?
Hili ni swali ambalo kwa hakika linahitaji majibu yakinifu, ili kuondoa vilio vya mapenzi vinavyowakumba watu wengi kila kukicha, kama nilivyoeleza huko nyuma kuwa, mapenzi yana kanuni zake ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kuepusha upande wa pili wa shilingi ya  mapenzi, upande wa maumivu.
 
UAMINIFU
Hii ni suala la kwanza kabisa katika kuepuka maumivu ya mapenzi, kwani ukiwa mwaminifu katika ndoa au uhusiano wa kimapenzi ulionao, basi itakuwa ni vigumu kwako kuteswa na mapenzi maana utakuwa umefuata moja ya kanuni zake.

Si jambo la busara kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja ukidhani ni ujanja au ni kwenda na wakati, la hasha, mapenzi hayaendi hivyo na usipokuwa makini utaishia kulia kila mara.

Utakapobainika kuwa wewe si mwaminifu, watu wengi watakutumia kimapenzi kwa faida zao na mwisho watakuacha ungali bado unawahitaji na hapo ndipo mwanzo wa chungu ya mapenzi huanza, yaani kuachwa na mtu ambaye bado unampenda.

Kwa waliowahi kutokewa na hali hiyo, wanaelewa namaanisha nini. Acha kurundika wapenzi. Jiheshimu na  mapenzi yatakuheshimu.

UONGO
Sumu yenye nikotini kali katika mapenzi ni uongo, kama wewe ni mzuri wa kupiga porojo katika uhusiano wako, basi mapenzi ni lazima yakutese.
 
Kwa nini uwe muongo katika mapenzi? Kuna faida gani ya kuwa na wapenzi wengi? Kwanini mapenzi yanakuumiza?

Leo uko na huyu, kesho uko na yule, maisha hayo hadi lini rafiki yangu? Utaishia kuwadanganya wanawake hadi lini ndugu yangu na wewe mwanamke, utawapanga hao wanaume hadi lini? Unadhani kuwachuna hao mabwana ndiyo maisha yanaishia hapo?

Tuachane na maisha ya kutangatanga na mapenzi, badala yake tuhangaikie maisha yetu.

Je, bado mapenzi yanakutesa? Umechelewa, kwani muda unaoupoteza katika kuhangaikia mapenzi, unatakiwa kuutumia kuwaza mambo ya muhimu ili mwisho upate maendeleo.

Kama una mpenzi au bado hujampata, basi vuta subira atakuja. Jambo moja la muhimu kuamini ni kuwa kila mmoja ana mwenza wake maishani, tatizo linakuja pale tunapoishiwa na uvumilivu na badala yake tunageuka watu wa kudandia na kubadilisha wapenzi kama nguo kila kukicha.

Kusema ukweli hayo siyo  maisha. Vuta subira, msubiri wako yuko njiani anakuja, na kama umeshampata, basi tulia naye huku mkipanga mikakati ya mafanikio kwenye ulimwengu huu uliojaa ushindani.
Hivi sasa maisha ni magumu, inakuwaje unakubali mapenzi yakutese?

Siwazuii watu kupenda, lakini  waache kuyapaparukia mapenzi kwa kutofuata kanuni zake. Yataishia kutuliza kila kukicha.

Mapenzi yapo tangu enzi za mababu zetu, kwa nini kuyaendea pupa, epuka sana kunga’ng’ania mapenzi kwa mtu asiye na chembe hata moja ya mapenzi juu yako, kwani kufanya hivyo ni kuzidi kujiletea mateso  maishani.

Napenda kuhitimisha kwa kusema kuwa, wewe ni mzuri mno, mapenzi yasikuumize kwani wako wa maisha yupo lakini bado hamjaonana na mkikutana haitakuwa shida kuanzisha uhusiano kwani mapenzi ya dhati huwa kama sumaku na chuma ni lazima vivutane.

Mwisho kabisa, waza sana juu ya maendeleo ya kimaisha na si mapenzi, kama unafanya kazi basi ongeza ufanisi kazini ili baadaye uishi maisha bora wewe na mkeo au mumeo kwa kuwa na mahitaji muhimu katika familia.

Monday 12 October 2015

KWA WANAUME.

Kama wewe ni mwanaume ni dhahiri unajua umuhimu wa kufanikisha utundu wakati wa tendo la ndoa.
Utundu katika sex ni kitu ambacho hupelekea kuwa na siku zenye kumbukumbu tamu na siku zenye kumbukumbu ovyo kabisa.
Pia utundu wako ndio unaokupa njia ya kufanya mke wako afurahie sex au kuona kitu cha kawaida na kuwa mbali nacho kabisa.
Kama mwanaume techniques zifuatazo hutakiwi kuzikwepa kabisa siku zote ukitaka sex iwe kitu kitamu na mpenzi wako.

JIFUNZE KUCHELEWA KUFIKA KILELENI
Kuwahi kukojoa mapema (ejaculation) ni muuaji mkubwa wa faragha na huhitaji kufanyia kazi kurekebisha hii tabia. Kama unawahi kufika kileleni kabla ya mpenzi wako au kufika pale ambapo mpenzi wako anahitaji basi Unahitaji kupata solution ya kudumu. Inawezekana kupata jibu hata kwa wiki au mwezi na ukawa unafika pale panatakiwa.
Hakuna kitu huumiza wanawake kama kitendo cha wewe kumaliza dakika mbili na kumwacha akiwa bado ana hamu na zaidi sana akiugulia kumuacha solemba kwa kumuonjesha utamu ambao hakumalizia.

FAHAMU SEHEMU AMBAZO MWANAMKE ANASISIMKA
Kila mwanamke ana sehemu ambazo husisimka zaidi na kupelekea kunyegeka na kuwa na hamu na kutana tendo la ndoa, mwanaume Unahitaji kujua ni sehemu ipi mke wako husisimka zaidi ukizingatia kwamba kila mwanamke ana sehemu yake. Mwanamke mwingine akiguswa viganja vya mikono tu chini analowa kabisa, na mwingine ukigusa matiti mtakosana maana unamuumiza. Mwanaume mtundu katika mapenzi hujua mke wake anasisimka na kuwa hoi akichezewa wapi.
Ukishafahamu ni sehemu ipi na inafanywa vipi ili asisimke basi huna budi kutumia muda wako wa foreplay kumpa bibie tamutamu yake hadi aridhike kwamba ana mwanaume anayemjali na si kurukia tu kule chini Afrika ya kusini na kuanza kuchimba dhahabu bila hata kujua mgodi wenyewe upoje.

UBUNIFU
Wanawake wengi katika ndoa na mahusiano hulalamika sana hasa kutokana na kukosa msisimko wa mapenzi wakati wa faragha. Wanalalamika kwa kuwa wanaume kila siku hutoa kitu kilekile, anakubusu, anakugusa kidogo na akiona chini kumelowa tayari anachomeka kama anapigilia misumari na ikiingia tu anapigilia akiona tayari huyo amemaliza na kuondoka zake.
Wanawake wanapenda surprise na kusisimuliwa katika njia mpya, mwanamke anahitaji kitu kipya baada ya muda, anahitaji sex position mpya, anahitaji busu jipya, anahitaji kunyonywa kupya na anahitaji kusikia neno kipya kwenye masikio yake.
Ni juu yako wewe mwanaume kujifunza mbinu mpya na kuwa mbunifu kitandani, wanaume ndivyo tulivyo tunahitaji kuwa wabunifu, fanya kitu kipya ambacho kitamfanya mwanamke ajisikia ana mwanaume ambaye ni MWANAUME


Sunday 11 October 2015

WANAUME WANGEPENDA WANAWAKE WAJUE HAYA.

Ni jambo lisilopingika kwamba ukitaka mahusiano mazuri katika ndoa jambo la msingi ni kumfahamu vizuri mwenzako hii ni pamoja na wanawake kujua wanaume wapoje.
Masuala ya mahusiano kwa sasa yanaandikwa na kuzungumzwa kila mahali na bado yanazidi kuvunjika haraka kama yanavyojengwa haraka.
Wanaume kama wanyama wengine (Species) wa kiume (siyo wote) hawako interested sana na romance bali wanataka sex moja kwa moja bila kupoteza muda, na hata kabla hajaoa anaweza kuwa alifundishwa na kufundishika, lakini siku zinavyozidi kwenda wengine hujisahau na kurudi kulekule kwenye utaratibu wao.
Wanaume ni kama vile hawana muda for sweet nothings (kwa mtazamo wao) acha kwamba wao akiona titi tu ameshasisimka na kuwa tayari.
Hivyo ukiona hufanyi vile anatakiwa ni vizuri kuongea naye ili mrudi kwenye mstari kuliko kulalamika au kubaki kimya na kudhani anajua kile anafanya.


Hata kama tangu akwambie "nakupenda" ni wiki mbili zilizopita au mwezi uliopita; kwa mwanaume hana maana kwamba hakupend, anakupenda sana.
Hata kama mwanaume anajua kabisa kwamba mwanamke anapenda kusikia neno “Nakupenda” mara kwa mara kama mwanamke mwenyewe anavyopenda kujiangalia kwenye kioo, wanaume wengi bado anaweza asiwe tayari kusema.
Hiivyo usiwe mwanamke wa hofu na mashaka unachotakiwa kujua ni kwamba wapo wanaume wapo hivyo so mnaweza kukaa pamoja na kukumbushana kwamba sasa unahitaji akwambie nakupenda.

Kawaid wanaume wenyewe kwa wenyewe hupenda sana kusifiana kuhusu mambo ya mahusiano ya kimapenzi ya nyuma na hujisikia vizuri, wakati huohuo hawapendi kabisa kusikia wake zao au wapenzi wako wa kike wakizungumzia mambo ya mahusiano yao ya nyuma.
Hivyo ni busara kuwa makini kuongea mambo yako (details) na mwanaume, ama sivyo mnaweza kukwazana.

Wanaume wengi hawapendi sana mwanamke anayetoa maelekezo, ushauri, mapendekezo au maswali kwa kurudiarudia mara nyingi.
Wanaume wanatumia sana akili wakati wanawake wanatumia sana moyo.
Hata kama hajafanya inawezekana bado anapiga hesabu zake kichwani jinsi ya kutekeleza, hana maana kwamba hakuelewa.

Usifikiri mwanaume atakasirika sana akisikia wanaume wengine wamekusifia mke wake au mpenzi wake.
Wanaume wengi hujiona fahari kusikia wanaume wengine wanamsifia mke wake au mpenzi wake.
Pia hata kama mwanaume utamuona anamwangalia mwanamke kwa jicho au kumsifia, haina maana kwamba si mwaminifu au ana uhusiano naye, wanaume ndivyo walivyo.

Wanaume wengi siyo waongeaji na huwa wanashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya wanawake wanaongea sana.
Kwa hiyo kama wewe mwanamke ukiona mume wako au mpenzi wako unapoongea naye ana hali ya kutokukusikiliza inawezekana kichwani mwake yupo busy, siyo kwamba hapendi unachoongea ila wewe ndo hujamwelewa.

Wanaume huumia moyo kama wanawake, hata kama amevaa mwili wa chuma na kichwani chake ni cha shaba bado ndani amebeba moyo laini wa nyama, na bado anahitaji kujisikia anapendwa na anahitajika na mwanamke.
Mwanaume si jiwe kwamba hana feelings, hata wanaume imara, wababe na jasiri huwa wanalia na kuvunjika moyo.
Hivyo mwanamke Unahitaji kumpa kile anastahili.

Wanaume ni watu wa sport na wanawake ni watu wa romance.
Mwanaume yupo tayari alale anaangalia kombe la dunia (soccer) kwenye TV lakini si michezo ya kuigiza au tamthilia hata kama ni saa moja. Pia anaweza kuwa yupo tayari kwenda Dar kutoka Morogoro kwenda kuangalia mechi ya Simba na Yanga lakini akawa hayupo tayari kwenda Dar kufanya shopping na wewe sana sana atakupa pesa ukanunue mwenyewe.
Ukitaka kumpatia mwambie mechi ya Yanga na Simba tutaenda wote na kabla ya mechi tutapitia Shopping kwanza , anaweza kukubali kuliko ukikataa na kumwabia hakujali kwa kuwa anapenda.

Hakuna kitu kinawauma wanaume (siyo wote) kitendo cha mwanamke kudai kitu chake au ahadi yake au zawadi yake au kuanza kubishana kwa kutofanya kile aliahidi kabla ya sex.
Utaharibu mambo!
Afadhari participate kwanza na mkimaliza ndo anza kasheshe zako maana atakuwa amepunguza pressure yake hapo atakusikiliza na kukuona wa maana, lakini si kabla

Haya ni maoni tu, usichukulie ndiyo msingi wa mahusiano yako na mumeo kwani kila ndoa ina mwanaume wa aina tofauti. ila kama unaona yanaelekeana basi ni muhimu kufahamu haya kabla hujaanza kumbadilisha mumeo au kumlalamikia.

JE,UKE UMELEGEA NA KUPOTEZA MVUTO?

Wapo wanawake akishazaa watoto wawili au watatu uke wake hulegea na kupelekea kutofurahia tendo la ndoa.
Hasa kama hakuwa mtu wa mazoezi tatizo linaweza kuwa kubwa, hata hivyo kufanya mazoezi ya Kegel ndiyo jibu kamili ya kurudisha uke kwenye mstari na kuanza kufurahia tendo la ndoa.
Mara nyingi wanawake huwacheka sana wanaume ambao visamaki vyao ni vidogo sana kwa kuwatania kwamba hata ukikohoa tu wakati wapo sita kwa sita kanachomoka, wakati huohuo wanaume nao huwacheka wanawake ambao huko chini kwenye machimbo ya dhahabu kuna pwaya mno kiasi kwamba mwanaume akiingiza mpini hasikii kitu chochote yaani hakuna ule mgusano au msuguano unaoleta raha ya tendo la ndoa.
Wengine wanaita ana uke kopo la kimbo.
Pia kuna wanawake uke umejaa maji kwelikweli hata uume ukiwa ndani ni kuteleza tu bila msuguano wowote wala kubana kokote matokeo yake hakuna ladha na utamu wa tendo lenyewe.

Dawa ipo tena bure na ipo ndani ya uwezo wako, kitu cha msingi ni kukubali mabadiliko na kuwa na hamu ya kutaka kubadilika.
Kuwe na uke tight unaokupa raha wewe na mume wako na zaidi afya yako ya uzazi kuwa imara.
Hata kwa wanaume zoezi hili ni simple wala halina gharama.

Ni kawaida wanaume wengi kuogopa kwenda kwa daktari kuongea masuala ya afya ya uzazi, hapa huhitaji kwenda kwa daktari, ni wewe mwenyewe kuwa serious kwani ukifanya vizuri utakuwa na uwezo wa kusimamisha mti wako kwa muda mrefu na pia unaweza kuhimili kubana kutofika kileleni mapema kabla ya mwandani wako.

Wanawake wengi baada ya kuzaa zaidi ya mara moja na kama hawakuwa watu wa mazoezi misuli ya uke hulegea na kupelekea kupoteza mnato na u-tight wa uke na pia kutojiamini wakati wa kufanya mapenzi kutokana na kupwaya kwa uke.
Kitaalamu hili zoezi huweza kurudisha hiyo hali ya kuwa tight baada ya miezi miwili kwa kufanya kila siku mfululizo na kwa kujitoa na kuwa serious.

Je, hili zoezi ni gumu?
Si gumu
Ni rahisi sana
Ni salama
Siyo zito na halichoshi
Linaweza kukupa matokeo baada ya wiki nane

Je, unaanzaje au nitajuaje huu ndo msuli wenyewe?
Kwanza ili kufanya hili zoezi anza kwa kutambua misuli ya uke au uume inayohusika kwa kuzuia mkojo unapotoka, then kojoa kwa kukata huku ukikaza misuli kwa kutoa mkojo kwa kuhesabu sekunde 4 hadi 10 au namba 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 the unakojoa tena ujazo wa kijiko cha chai then unaanza upya kwa kukata na kuhesabu 1 – 10 kila unapoenda kukojoa muda wowote.

Hii inasaidia kutambua msuli unaohusika na kukaza uke au uume.
Msuli uliotumia kuzuia mkojo ni rahisi kuuhisi ndo huo unahusika.
Hii misuli husaidia kukaza matundu matatu huko chini kwa mwanamke ambayo ni uke, tundu la mkojo na tundu la kutolea haja kubwa.
Ndiyo maana watu wanaofanya upuuzi ule wa sodoma na gomora kuna wakati huhitaji kuvalishwa nepi maana misuli imelegea hauwezi kuzuia tena haja kubwa.

Ukishapatia kujua msuli upi unamtumia kuzuia mkojo, basi unaweza kuendelea na zoezi hata kama hukojoi au kutoa haja kubwa kwa kuendelea kukaza kama vile unakojoa au unatoa haja kubwa ingawa siyo.
Unaweza kurudia zoezi muda wowote hata kama hukojoi mahali popote, kwenye kiti ofisini, kwenye daladala nk.
Wakati unafanya Hakikisha kuna tofauti ya sekunde tatu hadi kumi.
Pia unaweza kuongeza kukaza hiyo misuli kila ukikojoa fanya zaidi ya 20 kwa siku
Fanya kwa wiki nane mfululizo.
Kumbuka!
Kama wewe ni mwanamke ambaye chini kunapwaya au mume wake amekuwa analalamika kwamba hapati ladha na utamu halisi basi hili zoezi la kubana misuli litakuwezesha kubana uume au kuuvuta kwa ndani, au kwa kuukamua hatimaye anapata raha kwa msuguano unaokuwepo na wewe kufika kileleni haraka.
Ukitaka kujua uke wako unakubali zoezi jaribu kuingiza kidole wakati unafanya hili zoezi then utahisi kidole kubana zaidi kuliko kawaida.

JIFUNZE

Ukitaka kuwa na mahusiano mazuri na yule unampenda siku zote ni muhimu kujtahidi kumfahamu mwenzi wako upya kila siku kuliko kawaida yako.
Jitahidi kupata ufahamu wa kutosha kuhusu yeye jinsi anavyofikiri, na jinsi anavyotenda.
Vumbua zaidi kwa nini yeye na wewe kuna tofauti na jifunze jinsi ya kutumia hizo tofauti kufanya ndoa au mahusiano kuwa imara na wa kudumu.
Jifunze jinsi ya kufahamu yeye na pia ni namna gani unaweza kukubaliana naye katika jambo lolote, au jambo lolote kuhusu watoto, ndugu zake, mambo ya kanisani au kazini.
Pia fanya kila njia kupata ufahamu wa kutosha kuhusu yeye katika masuala muhimu ambayo mara nyingi huwa chanzo cha mifarakano na kuharibika kwa mahusiano kama vile
Pesa
Jinsi ya kulea watoto
Imani za dini
Tendo la ndoa
Na kila kitu ambacho kwenu ni muhimu sana

WANAWAKE TU.

Sabuni nyingi ambazo ni medicated huwa na kiasi kikubwa cha pH na kusababisha upungufu wa lactic acid (vulava & vagina) na huharibu mazingira ya asili (flora) na kupelekea kupata maambukizi kuliko kuzuia
Mwili wa Binadamu kawaida una pH kati ya 6.0 hadi 7.0
Uke kawaida huwa na pH kati ya 4.0 hadi 5.5 pia uke hutoa majimaji (secretion) yanayojulikana kwa jina la lactic Acid ambayo ni muhimu sana kuhakikisha mazingira katika uke yanakuwa na kiasi kidogo cha pH (Acid nyingi).
Kuwa na kiasi kidogo cha pH maana yake ni kuwa na acid nyingi ambayo husaidia kuondoka bacteria wasio rafiki wa mazingira ya uke, kwani maeneo yanayozunguka uke (vagina & vulva) yamezungukwa na ma mazingira ya ki-acid ili ku-balance viumbe (micro organisms) ambayo wanaishi kwa urafiki na kutokuwa na acid ya kutosha husababisha viumbe wasio rafiki (bacteria) kuleta maambukizi ambayo huweza kusababisha harufu mbaya hatimaye ladha chungu.
Sabuni nyingi za kuogea hata medicated, zina kiwango kikubwa cha pH kutoka 6.0 hadi 14 na hii huwezesha kuyapa challenge mazingira yanayozunguka uke na asili yake na husababisha maambukizi zaidi kuliko kusaidia kupunguza maambukizi.
Ndiyo maana kwa mwanamke kutumia medicated soaps ambazo zina pH 6.0 hadi 14 mfululizo si dawa bali ni kutaka kutengeneza mazingira ya maambukizi zaidi kwa bacteria kwa sababu hakuna acid tena kwa ajili ya kuzalisha lactic acid inayoyapa mazingira ya uke asili ya kupambana na maambukizi.

Katika ulimwengu wa sasa kuna sabuni maalumu kwa ajili ya wanawake kusafisha genitals zao na hizi sababu zina pH ndogo ambayo haiwezi kuathiri uwepo wa lactic acid na hizi sabuni hufaa sana wanawake ambao hupata maambukizi mara kwa mara.
Nenda uliza duka la madawa kama unaweza kupata women genital soups iwe maalumu kwa ajili ya kujisafi bila madhara ya kuharibu uoto wa asili huko chini.
Pia ni vizuri kwa mwanamke kutumia muda wa kutosha kujisafisha pussy yake kuliko kutumia muda mwingi kusafisha na kupaka rangi kucha au kushinda na kioo kwa ajili ya uso, lips wakati huko chini mambo si shwari.

Nani alikwambia wanaume wana uwezo mdogo wa kunusa?
Wananusa sana na wengine huonja kabisa hivyo usafi ni muhimu.

MAKOSA KUMI YA KUEPUKWA NA KILA MWANANDOA.

1. Kutokuheshimiana
Si vizuri kumtamkia maneno mabaya mwenzi wako mbele za watu.
Mke au mume anahitaji kuheshimiwa, kupewa asante kuwa appreciated na zaidi kumsifia mbele za watu na sivinginevyo.
Kuongea mambo mazuri kwa mke au mume wako mbele za watu ni muhimu sana.
Wapo wanaume hutukana wake zao mbele za watu na wapo wanawake hujibu mbovu waume zao hata mbele za watu au wageni. Kama kuna kitu amekuudhi kwa nini usisubiri mkaongee chumbani mkiwa wawili?

2. Kutosikiliza mmoja akiongea
Hii inajumuisha kuwa na mawazo ya mbali wakati mume au mke anaongea, yeye anaongea wewe unaendelea kuangalia TV, Unaendelea kusoma gazeti, unaendelea kusoma kitabu, Unaisikiliza laptop kuliko mume wako au mke wako.
Pia hii inajumuisha kuwa mbali kimwili (body language) wakati mwenzako anaongea, wapo wanandoa ambao hata mwenzake hajamaliza kuongea tayari anadakiwa kwamba najua ulichokuwa unataka kusema, pia wapo ambao hata ukiuliza swali yupo kimywa, mbaya zaidi ni pale unapoona na kuhisi mwenzako ana tatizo lakini ukimuuliza anabaki kimya au anakwambia hakuna tatizo, Inaumiza sana hasa kwa wenzetu wanawake ambao asilimia kubwa ya wanaishi kwa hisia, na kuumiza hisia zao ni kitendo kibaya sana, ni vitu vidogo lakini ni muhimu kuliko unavyodhani.

3. Kukosa mahaba (sexual intimacy)
Ukiacha mke wako au mume wako anahangaika na kutoridhishwa kimapenzi maana yake unachimba shimo ambalo ukijifukia utatokea jehanam, na kama unaona umepoteza interest na sex fanya kila njia kupata ushauri na msaada ili urudi kwenye mstari.
Matatizo mengi ya ndoa zinazokufa huanza kwa ugonjwa wa kutoridhishwa kimahaba na mume au mke.
Kumbuka ndoto za watu wengi kuoana ni kupata mtu atakayemtosheleza kimapenzi.

4. Kujiona sahihi mara zote
Hii inajumuisha wewe kuwa ndo msemaji na muelimishaji wa mke wako au mume wako, yaani wewe ndo unajua kila kitu, upo sahihi siku zote, au bila neno lako la mwisho basi information haijakamilika.
Siku zingine kubali kwamba umekosea au huna jibu, hakuna mtu anaweza kufurahia kuwa na mtu ambaye siku zote yeye ndo yupo sahihi labda kama unaishi na mtu mwenye mtindio wa akili.

5. Kutokufanya kile unasema
Siku zote Imani bila matendo imekufa na Imani ni matendo, “Actions do speak louder than words”. Ukisema utafanya kitu Fulani, fanya.
Wanawake ni viumbe ambao hutunza sana ahadi tunazowapa, hivyo usiahidi kitu ambacho huwezi kufanya, kwani mwenzio anaandika kwenye ubongo wake siku akija kukutolea mahesabu ya ahadi hewa umefanya utaipata fresh, pia na wanaume (si wote) kwa ahadi hewa hatujambo, tujifunze kufanya kila tunachosema.
Tusitoe ahadi tamu kumbe hewa, unaumiza sana.

6. Utani unaoumiza
Kama mwenzio anakwambia utani wako unamuumiza achana nao, kuna utani mzuri lakini kuna wakati mnaweza kufikishana pabaya na lazima uwe makini kusoma saikolojia za mwenzi wako, kuna wengine anaweza kukutania wewe usikwazike, na utani huohuo ukimrudishia yeye anakwazika so be very careful usimuumize mwenzako.

7. Kutokuwa mwaminifu
Kudanganya na kuwa na siri zako binafsi katika mahusiano huweza kujenga wawili kuwa mbali na kutokuaminiana.

8. Kuwa mtu unayeudhi kila wakati
Inaweza kuwa ni mzembe, mchafu, mtu wa kuchelewa kila mahali, mtu wa kusahihisha kila kitu mwenzio anafanya, mtu wa kulalamika tu kila wakati kila kitu, kuwa kimya tu mwenzio akitaka muongee masuala ya ndoa au familia. Unajua unaushi lakini unaendelea kuudhi.

9. Kuwa mchoyo
Yaani unatumia pesa nyingi sana kwa mambo yako na mume wako au mke wako akitumia pesa kidogo tu kelele na zogo hadi nyumba inakuwa moto.
Hadi nyumba yako haipo friendly maana hata kuburudika kwa soda tu kwako ni issue wakati ukiwa mwenyewe unajichana ile mbaya na kuku kwa chips na kitimoto na watu ambao ni nje na familia yako, hiyo ni aibu!

10. Ukali kama pilipili kichaa
Kila mwanandoa anahitaji kuwa mstaarabu linapokuja suala la kutatua mgogoro wowote, wapo ambao tatizo likitokea mke au mume na watoto wanatamani kuhama nyumba maana hapakaliki, Ni kweli kwa kelele zako na mihasira yako unaweza kuwin huo mgogoro lakini mbele ya safari bado utajikuta ni wewe ndo umeharibu zaidi.
Sidhani kama kuna mtu anapenda kukaripiwa kama mbwa ndani ya ndoa