Sunday 11 October 2015

WANAUME WANGEPENDA WANAWAKE WAJUE HAYA.

Ni jambo lisilopingika kwamba ukitaka mahusiano mazuri katika ndoa jambo la msingi ni kumfahamu vizuri mwenzako hii ni pamoja na wanawake kujua wanaume wapoje.
Masuala ya mahusiano kwa sasa yanaandikwa na kuzungumzwa kila mahali na bado yanazidi kuvunjika haraka kama yanavyojengwa haraka.
Wanaume kama wanyama wengine (Species) wa kiume (siyo wote) hawako interested sana na romance bali wanataka sex moja kwa moja bila kupoteza muda, na hata kabla hajaoa anaweza kuwa alifundishwa na kufundishika, lakini siku zinavyozidi kwenda wengine hujisahau na kurudi kulekule kwenye utaratibu wao.
Wanaume ni kama vile hawana muda for sweet nothings (kwa mtazamo wao) acha kwamba wao akiona titi tu ameshasisimka na kuwa tayari.
Hivyo ukiona hufanyi vile anatakiwa ni vizuri kuongea naye ili mrudi kwenye mstari kuliko kulalamika au kubaki kimya na kudhani anajua kile anafanya.


Hata kama tangu akwambie "nakupenda" ni wiki mbili zilizopita au mwezi uliopita; kwa mwanaume hana maana kwamba hakupend, anakupenda sana.
Hata kama mwanaume anajua kabisa kwamba mwanamke anapenda kusikia neno “Nakupenda” mara kwa mara kama mwanamke mwenyewe anavyopenda kujiangalia kwenye kioo, wanaume wengi bado anaweza asiwe tayari kusema.
Hiivyo usiwe mwanamke wa hofu na mashaka unachotakiwa kujua ni kwamba wapo wanaume wapo hivyo so mnaweza kukaa pamoja na kukumbushana kwamba sasa unahitaji akwambie nakupenda.

Kawaid wanaume wenyewe kwa wenyewe hupenda sana kusifiana kuhusu mambo ya mahusiano ya kimapenzi ya nyuma na hujisikia vizuri, wakati huohuo hawapendi kabisa kusikia wake zao au wapenzi wako wa kike wakizungumzia mambo ya mahusiano yao ya nyuma.
Hivyo ni busara kuwa makini kuongea mambo yako (details) na mwanaume, ama sivyo mnaweza kukwazana.

Wanaume wengi hawapendi sana mwanamke anayetoa maelekezo, ushauri, mapendekezo au maswali kwa kurudiarudia mara nyingi.
Wanaume wanatumia sana akili wakati wanawake wanatumia sana moyo.
Hata kama hajafanya inawezekana bado anapiga hesabu zake kichwani jinsi ya kutekeleza, hana maana kwamba hakuelewa.

Usifikiri mwanaume atakasirika sana akisikia wanaume wengine wamekusifia mke wake au mpenzi wake.
Wanaume wengi hujiona fahari kusikia wanaume wengine wanamsifia mke wake au mpenzi wake.
Pia hata kama mwanaume utamuona anamwangalia mwanamke kwa jicho au kumsifia, haina maana kwamba si mwaminifu au ana uhusiano naye, wanaume ndivyo walivyo.

Wanaume wengi siyo waongeaji na huwa wanashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya wanawake wanaongea sana.
Kwa hiyo kama wewe mwanamke ukiona mume wako au mpenzi wako unapoongea naye ana hali ya kutokukusikiliza inawezekana kichwani mwake yupo busy, siyo kwamba hapendi unachoongea ila wewe ndo hujamwelewa.

Wanaume huumia moyo kama wanawake, hata kama amevaa mwili wa chuma na kichwani chake ni cha shaba bado ndani amebeba moyo laini wa nyama, na bado anahitaji kujisikia anapendwa na anahitajika na mwanamke.
Mwanaume si jiwe kwamba hana feelings, hata wanaume imara, wababe na jasiri huwa wanalia na kuvunjika moyo.
Hivyo mwanamke Unahitaji kumpa kile anastahili.

Wanaume ni watu wa sport na wanawake ni watu wa romance.
Mwanaume yupo tayari alale anaangalia kombe la dunia (soccer) kwenye TV lakini si michezo ya kuigiza au tamthilia hata kama ni saa moja. Pia anaweza kuwa yupo tayari kwenda Dar kutoka Morogoro kwenda kuangalia mechi ya Simba na Yanga lakini akawa hayupo tayari kwenda Dar kufanya shopping na wewe sana sana atakupa pesa ukanunue mwenyewe.
Ukitaka kumpatia mwambie mechi ya Yanga na Simba tutaenda wote na kabla ya mechi tutapitia Shopping kwanza , anaweza kukubali kuliko ukikataa na kumwabia hakujali kwa kuwa anapenda.

Hakuna kitu kinawauma wanaume (siyo wote) kitendo cha mwanamke kudai kitu chake au ahadi yake au zawadi yake au kuanza kubishana kwa kutofanya kile aliahidi kabla ya sex.
Utaharibu mambo!
Afadhari participate kwanza na mkimaliza ndo anza kasheshe zako maana atakuwa amepunguza pressure yake hapo atakusikiliza na kukuona wa maana, lakini si kabla

Haya ni maoni tu, usichukulie ndiyo msingi wa mahusiano yako na mumeo kwani kila ndoa ina mwanaume wa aina tofauti. ila kama unaona yanaelekeana basi ni muhimu kufahamu haya kabla hujaanza kumbadilisha mumeo au kumlalamikia.

No comments:

Post a Comment