Tuesday 14 April 2015

SIFA ZA MWANAUME MUOAJI NA YULE ANAETAKA KUKUCHEZEA..

ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO


1. ANABADILIKA 
Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha 
Kisa Cha Mabadiliko Hayo Kinatajwa Na Wataalamu Wa Masuala Ya Ndoa Kuwa Ni Pamoja Na Kumshawishi Mwanamke Aliyemchagua Aitikie Mwito Wa Kuwa Pamoja Katika Maisha. Lakini Pia Ni Kuwapa Kielelezo Chema Ndungu Au Wazazi Wake Wamuunge Mkono Katika Harakati Zake Za Kuoa. 



2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA 
Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi.



Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi Atapanga Chumba Na Ataanza Kujitemea.



3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA 
Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani, Anawafurahia Watoto Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara Ataonekana Kukueleza Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada Ya Kuwapata Hapo Baadaye.



Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia Maisha Ya Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke Na Mume Wakiwa Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa Nyinyi. Mnapotoka Hukuita Mke Wake!



4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI 
Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki Yako Tu Kwa Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo Anayokufanyia Hayana Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano Kupanga Mipango Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa Ndugu Na Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua Matatizo Yako Na Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha Katika Matatizo Yanayomkabili.



Mara Nyingi Huwa Makini Sana Kutambua Mabadiliko Ya Mapenzi Na Hutoa Uhuru Na Kukumilikisha Vitu Vyake Kwa Mfano Kukupa Funguo Za Chumba Au Nyumba Yake. Hupenda Kutoa Misaada Ya Kumwendeleza Mpenzi Wake Kimaisha, Kama Kumsomesha Au Kumtafutia Kazi.



5. HUFURAHIA UKARIBU 
Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu Na Mpenzi Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake Atayaelekeza Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu Wa Mke Kila Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na Familia Ya Mchumba Wake.



SIFA ZA MWANAUME ANAYEKUCHEZEA 
1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA 
Haonyeshi Kufurahi Unapoanzisha Mazungumzo Kuhusu Suala La Kufunga Ndoa Na Wala Hapendi Kuzungumzia Hilo. Wakati Mwingine Hata Kukutambulisha Kwa Ndugu Zake Au Rafiki Inakuwa Shida.



2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU 
Anakuwa Ni Mtu Wa Kukununulia Mapambo Ya Gharama Na Vitu Vyote Vya Anasa, Lakini Hana Mawazo Ya Kuzungumzia Maisha Yenu Ya Baadaye Wala Kukununulia Vitu Ambavyo Vitakuwa Na Manufaa Katika Maisha Ya Mbeleni. Haangalii Masuala Ya Elimu Wala Kukutafutia Mtaji Au Kazi.



3. HAJALI MACHOZI YAKO 
Unaweza Kugundua Ni Jinsi Gani Hana Mpango Mzuri Na Maisha Yako, Kwani Hata Anapokuudhi Anakuwa Hajali Wala Haumizwi Na Machozi Yako, Ni Busara Kuwa Makini Kwa Sababu Huyo Atakuwa Ni Mtu Wa Kukupa Maumivu Wakati Wote.



4. HAJITOKEZI HADHARANI 
Mwanaume Ambaye Malengo Yake Ni Kukuchezea Huwa Hataki Mapenzi Yenu Yajulikane Hadharani Atakuwa Mtu Wa Kutaka Mambo Yaende Kwa Siri. Hajitambulishi Kwa Rafiki Wala Kwa Ndugu Zako. Hatoi Nafasi Ya Wewe Kumtembelea Nyumbani Kwake Wala Kuwajua Wale Wa Karibu yake na familia yake.

Ukiona hivyo wanasema akili za kuambiwa, changanya na za kwako.

KAULI ZA HATARI KWENYE MIGOGORO YA WAPENZI/WANANDOA.

Kugombana hakuna maana ya kumalizika kwa uhusiano hasa kwa wale walio kwenye ndoa. Mambo yanatokea, yanatatuliwa na mwisho wake maisha yanaendelea kama kawaida.

Kwa bahati mbaya sana ni kwamba, wengine wanapokuwa kwenye migogoro na wenzi wao, badala ya kutafuta njia za utatuzi, wanazalisha tatizo lingine!
Jambo la kusikitisha ni kuwa, tatizo jipya linalozaliwa linaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi katika uhusiano huo na mwisho wake kusababisha kuachana kabisa.
Zipo kauli ambazo ukizitoa kwa mpenzi/mke/mume wako wakati mkiwa kwenye ugomvi, zinaweza kuzalisha tatizo kubwa zaidi mbeleni.


KWA NINI KAULI?
Inawezekana ukajiuliza; ni kwa nini nimesema kauli? kwa kawaida, watu wakiwa kwenye ugomvi, jambo kubwa linalotokea ni kutupiana maneno.
Katika hali hiyo basi, kwa wenzi au wanandoa ni vyema kuchunga ndimi zao maana zinaweza kusababisha matatizo makubwa siku zijazo.

1.‘HUNA AKILI’
Wako baadhi ya watu wakigombana (hasa wanaume) wamekuwa na tabia ya kuwaambia wanawake wao: “Wewe huna akili kabisa...yaani hutumii akili kabisa katika kufanya mambo yako.
“Unakurupuka tu. Sasa ishu kama hii, hata mtoto mdogo anajua ni makosa, inakuwaje wewe unakosea?”
 
Hili ni jeraha la moyo. Mwanamke ukimwambia hana akili anajisikia vibaya, unampa kovu kubwa moyoni mwake. Anajiona wa hali ya chini na anahisi ameshuka thamani yake.
Kwake, kumwambia hana akili, ataanza kuwaza kuwa yupo mwanamke mwingine ambaye kwako ana akili kuliko yeye. Ni maumivu makali sana kwake.

2.‘NITAKUACHA’
Baadhi ya wanaume wana ulemavu huu. Ugomvi kidogo tu, atamwambia mwenzake: “Endelea na tabia zako za hovyo, ipo siku utajuta. Nimevumilia mengi sana lakini kuna siku nitachoka.
“Hutaamini macho yako. Siyo lazima niishi na wewe. Siwezi kuendelea kuteseka nikiwa na wewe. Nitakuacha nakuambia ukweli.”
Hii ni kauli mbaya ambayo inapandikiza chuki ndani ya moyo wa mwanamke. Kwanza kwa kumwambia hivi, hata kama alikuwa hakusaliti, unamfanya aanze kufikiria kutafuta mtu mwingine wa kumliwaza.
 
Kauli hii hasa kama ukiirudia zaidi ya mara mbili, humkaa akilini mwake na huanza kuwaza kuhusu kuwa na mwanaume mwingine nje ili apate mahali ambapo hata kama ukimuacha, atapata pumziko la uhakika.

3.‘NAKUVUMILIA TU’
Ni kweli mapenzi ni uvumilivu. Kuvumiliana ni siri ya uhai wa ndoa nyingi lakini hilo linapaswa kubaki moyoni.
Kugombana na mwenzako halafu umwambie kuwa unamvumilia tu, inamaana kwamba kuna siku uvumilivu wako utaondoka na utafanya maamuzi magumu – kuachana!
Si kauli njema kwa mwenzi wako. Mbaya zaidi humfanya aanze kufanya maandalizi ya mtu wa kuziba nafasi yako hata kama ni kwa usaliti. 

4.‘KUNA SIKU UTAJUTA’
Kauli hii haina tofauti kubwa sana na iliyotangulia maana kinachofanyika hapa ni kumuandaa mwenzi wako kwa ajili ya matatizo siku zijazo.
Kumwambia: “Kuna siku utajuta, endelea na mambo yako tu, utaona.” Hii inamaanisha kwamba, uamuzi ulio ndani yako si mzuri kwake lakini ni suala la muda tu.
Ataamini (na ndivyo ilivyo mara nyingi) kuna muda ambao atajuta sana kwa sababu yako. 
Hiyo ni sawa na kutengeneza bomu unaloliandaa kulilipua muda ujao.
Bado zipo kauli zaidi ambazo zina maudhi lakini pia zinaweza kusababisha matatizo zaidi kwa mwenzi wako


Wednesday 8 April 2015

MPE NAFASI MPENZI WAKO KWA WANAUME WANAOKUSUMBUA KINGONO..

Kuna malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wasomaji wakielezea jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, wengine wakidai wanataka kuwaoa, wengine wakieleza wazi kuwa wanataka kufanya nao mapenzi tu tena kwa ahadi ya malipo manono.
Kimsingi hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunakoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwashika sehemu zao nyeti bila ridhaa yao.
 
Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao. Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao.
 
Hata hivyo, kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata baadaye. 
Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana!
 
Niseme tu kwamba, wanaume siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.
 
Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala kwamba kila mtu anaweza kumchezea.
Lakini mbali na hilo, unajiwekea mazingira ya kuwafanya wanaume wakuheshimu na kugwaya hata kukutamkia maneno ya kijinga.
 
Vaa kiheshima, acha utani wa kijingajinga na wanaume na hakikisha unakuwa na tabia ambazo zitawafanya wanaume wakware wajue kwamba wewe ni mtu mwenye ndoa yako usiyetaka kuutia doa uhusiano wako.
Hata hivyo, huko mtaani unakopita unaweza kukutana na mwanaume anayejua fika wewe ni mtu ulie kwenye uhusiano wako lakini anakusumbua kila siku huku akikushawishi kwa njia mbalimbali.
 
 Huyu hutakiwi kumchekea na kumpuuzia, una kitu cha ziada unachotakiwa kukifanya. Nasema hivyo kwa kuwa kuna wanaume vinga’nganizi. Unampa maneno makali ili akukome lakini bado anaendelea kukusumbua.
 
 Inapofikia hatua hiyo jaribu kumshirikisha mpenzi wako au mumeo.
Hiyo itasaidia sana kwani mumeo anaweza kuchukua hatua zinazostahili dhidi yake na hatimaye kuweza kupunguza kasi ya usumbufu huo. Kamwe usithubutu kukaa kimya.
Mbaya zaidi ni kwamba unaweza kukuta shemeji yako ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wako ama mwanaume anayemfahamu vilivyo mumeo akakutongoza. Huyu ni hatari sana na wala usisubiri akutongoze mara mbili. Siku ya kwanza tu atakayokutamkia maneno yake ya kipuuzi, kwanza geuka mbogo, mkaripie kwa ukali kisha mpe taarifa mpenzi wako.
 
Baada ya hapo, mwanaume huyo hutakiwi kumheshimu, mchukukulie kama mjinga mjinga fulani. Nasema hivyo kwa kuwa mwanaume wa dizaini hiyo akikutokea kisha ukawa unamchekea ipo siku anaweza kukulazimisha kufanya naye mapenzi.

JE,UNAMPENDA AU UNAJILAZIMISHA?...Jipime kwa maswali haya

Watu wengi wako kwenye uhusiano wa kimapenzi bila kujua kama kweli wanapenda kwa dhati au wanajilazisha? Ili kutambua upendo wako jipime kwa maswali yafuatayo:

1 - Unapoamka asubuhi wazo la kwanza kukujia linamhusu mpenzi wako au unafikiria zaidi kazi na mambo mengine? Una msukumo wa kutaka kumsalimia na pengine kumuuliza anapenda afungue kinywa kwa chakula gani?

2 - Je umekuwa mwepesi na mwenye furaha kubwa kuwaambia rafiki zako wa karibu juu ya hisia zako kwa mpenzi wako? Unajisikiaje wanapokushawishi vibaya kuhusu yeye?

3 - Je, anapokwambia anakuja kukutembelea huwa unajisikia hamasa moyoni kiasi cha mwili kusisimka?

4 - Unapokuwa peke yako mawazo yako yanatawaliwa na yeye au unafikiria kucheza gemu kwenye simu yako na kujifariji kwa vitu vingine?

5 - Unapompima kwa kumlinganisha na wengine anachukua nafasi ya kwanza au anazidiwa?

6 - Je, unapomfikiria na kupata kivutio fulani ndani ya moyo wako kuhusu ucheshi na utani wake huwa unatabasamu hata ukiwa peke yako?

7- Unajisikiaje wazo la kusalitiwa linapokujia, unaona ni sawa au unahuzunika kiasi cha kupoteza furaha na kutamani uambatane naye kila aendako ili usiibiwe?

8 - Hebu jiulize ni mara ngapi umekuwa ukishawishika kumnunulia mpenzi wako nguo, mapambo au vitu kwa lengo la kumfanya avutie au ndiyo umemtelekeza na kumwacha aonekane mchafu na asiyevutia mbele za watu?

9 - Je, umekuwa mtu wa kujijali mwenyewe kwa mavazi na mwonekano wako kwa lengo la kumfanya mwenza wako afurahie kuwa na wewe au ndiyo unajiweka katika mazingira ya ovyo yanayomtia aibu kwenye jamii?

10 - Unapoota ndoto za kimapenzi usiku, amekuwa akikutokea yeye au kuna wanaume/wanawake wa pembeni ndiyo wanajitokeza katika kuota kwako?

11- Unaposikiliza nyimbo za kimapenzi huwa unahisi ujumbe huo ni kwa huyo umpendaye au unauelekeza kwa mtu mwingine?

12 - Je, marafiki wa karibu wa mpenzi wako wamekuwa wakikupa kipaumbele au wanakudharau na kutopenda kukutana na wewe?

13 - Unajisikia furaha kuwa naye au huwa unapenda ubaki mwenyewe nyumbani ili ufanye mambo yako unayodhani uwepo wa mpenzi wako ni kikwazo?
14 - Je, umekuwa ukitafuta kwa nguvu nafasi za kukutana na mwezako au ndiyo kila siku uko bize na kazi?’

15 - Unapomtathmini mpenzi wako unajiona umepata au umejishikiza wakati ukitafuta mwingine?

16 - Umekuwa mwepesi kiasi gani kukumbuka ahadi zako kwake au kila unachopanga kumfanyia unasahau? Kumbuka kuhusu kumpigia simu, umekuwa ukijikuta ukisahau mara kwa mara?

17 - Vipi mpenzi wako anapopata nafasi ya kukushika sehemu yoyote mwilini wako, huwa unahisi msisimko mkali au mpaka ulazimishe hisia?

18 - Je, uko tayari kumwamini kiasi cha kumwekea dhamana?

19 - Kama utasikia mpenzi wako anakusifia kwa wenzake au kukuthamini kwa lolote utajiona mwenye bahati duniani?

20 - Unapofikiri hadhi yako unaona inalingana na mwenzako au unahisi umemzidi na kwamba mapenzi yako ni kama umemsaidia kumweka juu?

21 - Unapopata siku ya kupumzika, mtu wa kwanza kumpa kipaumbele cha kujumuika naye ni huyo mpenzi wako au unapenda kufanya mambo mengine?

22 - Je, umekuwa ukitamani kumpigia simu kwa lengo la kusikia tu hata sauti yake na ukahisi furaha?
Mpenzi msomaji wangu, haya ni baadhi ya maswali ya msingi ambayo majibu yake yanaweza kukusaidia kujua kama unampenda au unaulazimisha moyo wako. Naomba ukae peke yako na ujibu maswali haya ambayo mengi yako kwenye msingi wa jibu la ndiyo au hapana.