Wednesday 5 August 2015

USIACHE HASIRA ZIKAJAA..

Kutoweza thibiti hasira husababisha kutokuelewana katika ndoa.
Kila mwanandoa anahitaji kuwa makini na hasira zake ambazo wakati mwingine hupelekea kuwa mtu wa kukefyakefya, mtu wa vijembe na kejeli, pia mtu wa kulaumu kila wakati na vitu kama hivi ni moja ya alama kuonesha kwamba ndoa imeanza kuchimbika.

Tunahitaji constructive ways za ku handle hasira katika ndoa.

Siku zote binadamu hupenda ku-fight back, kitu kidogo huwa issue kubwa kabisa hata hivyo mtu mwenye busara anafahamu fika kwamba kusamehe na kusahau nia kuishi katika mapatano ni sehemu ya gharama ya amani na upendo katika ndoa imara.

Mwanamke mwenye busara husema:-
"Ingawa mume wangu hutupa nguo na soksi huko na huko anapobadilisha namuona ni mume mzuri kwani ananijali, who care! Kama ananitimizia mengine mengi tu hili ni kitu gani linisumbue!"

Mwanaume mwenye busara husema:-
"Hata kama mke wangu hapendi kusafisha nyumba mara kwa mara hivyo jinsi anavyopika chakula kitamu na alivyo mwema kwangu ninampenda na ninaridhika na ndoa yangu".

Ingekuwa wengine kwa matatizo yaliyoelezwa hapo juu basi ingekuwa shughuli nzito kwani wanandoa wengi huangalia negatives badala ya positives na ukweli ni kwamba ukiwa unaangalia negatives maana yake unaweka sumu katika mahusiano yako.

Kumbuka mke na mume wanapoanza kuzozana ni kama kutoboa matundu kwenye bwawa na baada ya muda bwawa zima hupasuka na kutoa maji ya fujo hivyo kuhimilia hasira ni jambo la msingi.

Pia si busara sana kusubiri hasira zijazane kwani itafika mahali intensity itakuwa kubwa sana na mkaanza kulipuana kama mabomu.


Kama ikitokea mnabishana kwa ajili ya kitu chochote si vema kumwambia mke wako au mume wako “hoja yako ni rubbish”
Uwe makini na kile unaongea ukiwa na hasira

Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.
Mithali 15:1-2

No comments:

Post a Comment