Wednesday 5 August 2015

HATUA ZA KUCHUKUA BAADA YA AFFAIR.

Ni ukweli ulio wazi na usiopingika suala la mwanandoa kukosa uaminifu ni jambo lenye maumivu makali sana kama vile kukata kisu tumboni, linakasirisha.

Hutoa wazo la kwamba hutamwamini tena na huchukua miezi na miaka mingi sana ili kuanza kurudisha upendo na trust kwake upya hata hivyo siku nyingi hata baada ya miaka 20 ikitokea hujui ameenda wapi unaweza kujikuta unaanza kuwaza labda kaanza tena kwani hiyo hali huendelea kukuwinda maisha mengine yote yaliyobakia katika ndoa yako hapa duniani.

Mwanandoa aliyesalitiwa huanza kuwaza kama kweli hii ndoa itaendelea au ndo imefika mwisho kwani ndoa hujengwa kwa trust na EMS hubomoa trust ya ndoa.

Unapoambiwa kwa mara ya kwanza kwamba mume wako au mke wako ana affair basi unajikuta unasongwa na mawazo negative ambayo hupelekea shock kihisia, uchungu, huzuni ya uhakika, ukali, kutoamini kilichotokea na wakati mwingine unaweza kujikuta upo mad (mwehu); hata hivyo hizo feelings ni kitu cha kawaida na una haki ya kujisikia hivyo.

Hii ina maana kama nikulia lia sana, pia utakosa usingizi na hamu ya chakula pia utasongwa na mawazo kuhusu affair hadi kushindwa kufanya concentration ya kuwaza vitu vingine muhimu kama kazi nk (usipokuwa makini na unavyovuka barabara unaweza kugongwa na magari.

Maisha huanza kuongozwa na emotions badala ya wewe kuongoza maisha na unakuwa na hofu kwamba unaweza usiwe mtu mwenye furaha tena maishani.
Inakuwa ngumu sana kuamini kwamba ipo siku utarudi kwenye hali yako ya kawaida.


Je ni hatua gani zichukuliwe ili kurudi kwenye hali ya kawaida?

Kwanza ni muhimu sana yule ambaye amesalitiwa kuhakikisha anamweleza mhusika vile anajisikia kama ni hasira au maumivu.
Pia anaweza kuuuliza maswali yoyote ili kupata ukweli kuhusu affair ilikuwaje ingawa kuuliza maswali sana huwa na faida na hasara faida ni kwamba utaambiwa ukweli (facts) kuliko kuwa na wasiwasi kutojua affair ilikuwaje.

Hasara ni kwamba unaweza kupewa details ambazo zinaweza kukupa uchungu na hasira zaidi kwani unaweza kuambiwa mambo ambayo yatakufanya utamani kutapika.
Hivyo kabla ya kuuliza jipime kwamba kama una uwezo wa kuvumilia details utakazosikia.

Pili yule ambaye amemsaliti mwenzake anatakiwa kuachana na mwanamke au mwanamke amefanya naye dhambi (affair)

Hakuna mawasiliano kwa kuonana, email, simu, twitter, face book, barua au njia yoyote ya mawasiliano duniani.
Kama anayehusika amegoma hii kanuni basi ni dhahiri hajaacha na ataendelea kumuumiza mwanandoa mwenzake.

Kama mtu wa tatu au yule mwanamke au mwanaume ametembea na mwanandoa ataendelea kusumbua kuwasiliana na mwanandoa aliyemsaliti mwenzake inabidi msaliti awasiliane na mwanandoa mwenzake kwamba
“Yule mwanaume au yule mwanamke bado ananisumbua kutaka tuwasiliane”
ili kila mmoja ajue namna ya kusaidiana kukata mawasiliano kwani kuendelea kuwasiliana hudhoofisha process za healing.

Tatu, kwa aliyesalitiwa kubali kwamba feelings ulizonazo katika janga hili ni kitu halisi na zinaumiza na ni kitu kigumu.
Huna haja ya Kujikataa na kuamua kupunguza. mawazo, maombolezo, kushuka chini ni vitu vya kawaida.

Nne, uliesalitiwa unaweza kumtafuta mtu unayemwamini ambaye unaamini anaweza kukusaidia ushauri na kukuombea na unatakiwa kuelezea the whole story hata kama inauma.
Lazima uwe makini na mtu unayemuomba ushauri kwani kuna mwingine badala ya kujenga; atakubomoa vipande vipande na kuharibu maisha yako miaka 50 ijayo.

Tano wote wawili (mkosaji na aliyekosewa) kukaa pamoja na kujadili ili kujua sababu ya affair ilikuwa nini, affair ilikuwa na maana gani

No comments:

Post a Comment