Tuesday 18 August 2015

KUNA TOFAUTI...!!

Wanandoa imara au waliofanikiwa katika ndoa yao ni wale ambao wanaweza kukaa pamoja na kujadili tofauti zao katika namna ambayo huwezesha kujenga ukaribu kimapenzi (intimacy) zaidi.

Wanafahamu jinsi ya kukubaliana na kutokukubaliana (disagreements), wanafahamu namna ya kuhakikisha kutokukubaliana hakusababishi maafa kwenye maeneo mengine ya mahusiano yao.
Si kweli kwamba tunaolewa au kuona ili kuchukuliana katika migogoro hata hivyo kutofahamu namna ya kupambana na migogoro huweza kusababisha kutofanya vizuri katika mambo mengine ambayo ndo sababu za kuoana.

Kukwepa migogoro au kukwepa kuongea pamoja eti kunaweza sababisha mgogoro mzito si hekima wala busara kwani njia bora ni kuwa wazi kuongea pamoja ili kujadili tofauti au kutokuelewana kunakojitokeza ili wanandoa waweze kufahamiana zaidi.

Kwa lugha nyingine si rahisi mke kufahamu mume anapenda chakula gani bila kuongea kwanza, pia haina maana kukaa kimya kwa kuwa mke anapika chakula usichopenda basi atabadilisha na kukupikia chakula unapenda. Si rahisi mume kukupeleka outing kama hamuongei.

Wapo wanandoa ili kuepuka migogoro huacha kuongea na kuwa kimya, ni muhimu sana wanandoa kufahamu utafiti wa ndoa imara unasemaje.
Kila ndoa imara kwa wastani ina maeneo 10 ambayo wanandoa hawafanani au hawawezi kukubaliana au kwa lugha nyingine hawataweza kufikia muafaka maishani mwao.

Kwa nini hizi ndoa imara pamoja na tofauti 10 na bado zinaitwa ndoa imara?
Jambo la msingi au siri kubwa ni kwamba wanandoa wanafahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti na kuishi nazo, kupendana pamoja na kutofautiana na zaidi kila mmoja anamuelewa mwenzake na kukubaliana kihisia na kuchukua nafasi yake kama ni yeye.

Wanandoa imara hufurahia na kusherehekea tofauti zao na hufarijika kwa kuwa sasa anamfahamu mwenzake, anajua eneo ambalo wapo tofauti then wanaaendelea kupendana huku kila mmoja akifahamu namna ya kukabiliana na hizo tofauti.

Hawa wanandoa imara wanafahamu wazi kabisa kwamba hata kama watabadilisha partners bado watapata matatizo mapya katika maeneo ya kutokukubaliana, kuwa tofauti na kwa huzuni kubwa kazi kubwa itakuwa ni mizigo waliyotoka nayo kwenye ndoa zao za kwanza kama vile watoto nk ndiyo maana kwao talaka haina sauti wala nguvu na huwa haizungumzwi, ni neno lililofutwa katika maongezi.
Zaidi ya kukabiliana na tofauti na kutokukubaliana pia ni muhimu sana kusherehekea/kumbatia mabadiliko.
Wakati tunaoana huwa tunaahidi kukaa pamoja hadi kifo kitakapo tutenganisha hata hivyo huwa hatuahidi kubaki vilevile bila mabadiliko yoyote, tunahitaji kukua, kuongezeka skills, kwa wabunifu na wazuri zaidi kila siku zinavyozidi kwenda.
Kuna mambo mengi tunaweza kujifunza kadri ziku zinavyozidi kwenda kama vile kusema asante, kuomba msamaha.
Hivyo inawezekana kujifunza tabia njema ambazo zinaweza kujenga ndoa na kuziacha tabia mbaya ambazo zinaweza kuharibu ndoa.

No comments:

Post a Comment