Wednesday 5 August 2015

MWANAMKE..JIAMINI JINSI ULIVYO..

Anayekupenda anakupenda kwa sababu ya jinsi ulivyo Na jiamini kwa jinsi nilivyo.


Wanawake wengi hasa katika jamii za leo wengi wanaukataa mwonekano wao na kuhisi size au shape walizonazo bado hazijafikia kiwango kinachotakiwa na wapenzi wao.

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba asilimia 80 ya wanawake wenye umri miaka 18 hadi 35 hawaridhiki na size na shape za miili yao.
Wengine wanajiona ni wembamba sana na wengine wanajiona ni wanene sana, wengine wanajiona matiti ni madogo mno, wengine wanajiona matiti ni makubwa mno, wengine wanaona ngozi zao si laini kwa kiwango kinachotakiwa na wengine wanajiona ni wazee mno kuliko umri wao.
wengine wanajiona ngozi zao ni nyeusi mno hivyo wanahitaji kubadilisha kuwa nyeupe zaidi.
Wakati mwingine unashangaa kumuona mwanamke au binti aliyekuwa na size na shape nzuri amejibadilisha na kuwa na shape nyingine kabisa, hata unaweza kumsahau na kudhani ni mtu mwingine kabisa.
Anajiona amejitahidi kufikia viwango anavyodhani ndo anapependeza.
Wanawake wengi sasa wanapigana kufa na kupona linapokuja suala la mapaja, vifua, tumbo, unene na wembamba hata rangi.
Wengine wamejiingiza kwenye dieting ambazo matokeo yake wamekuwa wanaishi katika njaa na hatimaye kupoteza kinga ya mwili na kushambuliwa na magonjwa ovyo.
Sikatai upunguze uzito au kuwa mrembo!

Kuwa na negative image ya mwili wako husababisha kutojiamini na kutojiamini husababisha kuuchukia mwili wako na matokeo yake unaweza kuathiri maisha na uhusiano wa mapenzi ya yule umpendaye.
Kwa kuwa huupendi mwili wako, umeuchukia, hujiamini imekuwa vigumu hata kuwa uchi mbele za mume wako kwani unaogopa eti mwili hauvutii
"The body is not looking good"
Nikuulize swali!
Je, ni mumeo aliyekwambia mwili wako hauvutii au ni mawazo yako na mtazamo wako?

Kitu cha msingi ni kufahamu kwamba mume wako anakupenda kwa sababu ya jinsi ulivyo na anakupenda zaidi ya hilo umbo ulilonalo.
Jiamini na kujipa raha na mume wako kwa amekupenda wewe kwa sababu duniani upo wewe tu hata kama mpo mapacha bado yeye amekupenda wewe.
Ni kweli kuna wanawake kwenye TV na kwenye magazeti ambao kwa jinsi walivyo unaweza kuvutiwa uwe kama wao hata hivyo kila mtu duniani aliumbwa tofauti na hiyo tofauti ndiyo imefanya tuwe na mtu ambaye ni wewe.

Ukiona mume anakulaumu sana kwa sababu ya umbo lako, lazima kuna sababu nyingine nyuma yake ipo, otherwise atasaidiana na wewe kuhakikisha unakuwa anavyotaka yeye na si kukulaumu sana.
Ukiona kelele ni nyingi sana kwamba siku hizi huvutii inaweza kuwa ni kweli umejiachia na kutojipenda na kuwa mrembo na sexy ingawa pia uwe makini inawezekana hiyo ni sababu tu nyuma yake ana lake jambo.

Mume wako anakupenda si kwa sababu ya umbo lako tu kuna vitu vingi vinavyomvutia inawezekana ni:-
Unavyotabasumu
Unavyomkubali yeye kama alivyo
Unavyotembea
Matiti yako
Matako yako
Shingo yako
Macho yako
Nywele zako au
Jinsi unavyoongea nk
Ni vizuri pia ukaongea na mpenzi wako kwamba unataka kufanya kitu fulani kabla ya kubadilika na kuwa mtu mwingine na baadae ikawa masheshe, inawezekana akawa anavutiwa sana na weusi wako na wewe ukaamua kujipiga mkorogo na kuwa tofauti ikawa balaa.

Elekeza mawazo yako katika maeneo ya mwili ambao unaona kwako ni mazuri zaidi kuliko kuelekeza kwenye maeneo ambayo unadhani hayapendezi.
Kutumia uzuri wa mtu mwingine kuwa kipimo chako husababisha kujiona inferior zaidi kuhusiana na mwonekano wa mwili wako kuliko ungeamua kujiamini na kuukubali mwili wako kama ulivyo.
Usitamani kuwa na matiti makubwa kama fulani, au kuwa na nywele ndefu kama fulani matokeo yake kwa kuwa haiwezekani utajikuta huufurahii mwili wako.
Mungu hahitaji kuwa na watu ambao wote wananafanana ndiyo maana kila mtu alimuumba kuwa tofauti na hii tofauti ni pamoja na muonekano wa mwili wako na ndiyo inayofanya mtu upendwe na ufurahie mahusiano.

wewe ni mwanamke wa tofauti, upende mwili wako na jiamini kwani jinsi ulivyo ndivyo ulivyo hakuna mtu aliyekama wewe duniani ni wewe tu.

No comments:

Post a Comment