Tuesday 11 August 2015

TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI..mwisho

Mwanaume kuwahi kumaliza (Premature Ejaculation - PE) ni jambo muhimu linalomhusu mke na mume, karibu mwanaume mmoja kati ya wanawaume watatu mmoja huwa na tatizo la kuwahi kumaliza mapema.
Nitatumia Neno PE kumaanisha mwanaume kuwahi kumaliza mapema au kwa kingereza (Premature Ejaculation)
Kwa njia zingine kuwahi kumaliza kwa mwanaume ni kitu ambacho kimejificha kwani huwezi kumtambua mwanaume ambbaye ana PE kwa kumwangalia sura, pia ni mara chache sana au ni ngumu sana kwa wanaume kupeana story za mambo kama haya wakiwa wenyewe kwani mwanaume huhofia kuonekana si lolote kwa wenzake (kupoteza ego) sana sana anayejua ni mke wake ambaye anajua inamuathiri kiasi gani na kupata usumbufu kiasi gani kwani wapo wanaume ambao hata huruma hana ile kumaliza tu basi usimguse.

Kwa kuwa hakuna mwanaume anapenda kuwa na PE hii ina maana kwamba kuwa na PE siyo huathiri mwenendo wa sex tu bali hupelekea kuathiri maeneo yote ya maisha kwani mwanaume akiwa na hili tatizo huogopa kushiriki na matokeo yake huwa mtu mwenye masumbufu na mpweke na baadae hukosa ujasiri na huathiri maisha kwa ujumla hadi taaluma yake.

Mambo mengine ya msingi ambayo yanaweza kukusaidia mwanaume ni jinsi ya kutumia akili na mawazo.

Amua kwamba utaweza kuthibiti hiyo hali, jiamini, jitolee, uwe na imani ile ya kuhamisha milima na kwamba wakati umefika unataka kubadilisha uwezo wako katika tendo la ndoa.

MAZOEZI
Pia ni muhimu kuwa mtu wa kufanya mazoezi, kama una misuli ambayo hata kama ulikuwa unakojoa (urinate) ukashindwa kuziba mkojo ghafla basi hii ina maana misuli yako ya PC imelegea na jambo la msingi ni kujifunza kuikaza kwa kufanya mazoezi.
Kuwa na misuli ya PC iliyokaza ni siri kubwa katika kufanikisha furaha ya mapenzi kwa mume na mke.
Nini Imani Potofu kuhusiana na PE?

Eti PE ni kitu ambacho huwezi kuthibiti.?

Ukweli ni kwamba unaweza kuthibiti na mwanaume yeyote anaweza kujifunza kuthibiti PE kama vile ile njia alitumia kubana mkojo wakati mtoto na sasa akilala hakojoi ovyo kitandani.

Eti PE huathiri wanaume wenye umri mkubwa.?

Ukweli ni kwamba PE huathiri wanaume wa umri wowote, ingawa wanaume wenye umri mkubwa huwa na tatizo na kushindwa kusimamisha na hutumia muda mrefu ili uume usimame na kuwa tayari kwa tendo la ndoa.

Eti PE huweza kusababisha kuwa na matatizo ya kuchelewa kusimamisha.?

Ukweli ni kwamba huwezi kukojoa bila uume kusimama hii ina maana kuliacha tatizo kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kuwa na matatizo ya jogoo kushindwa kuwika kabisa.

Eti PE haiwezi kuathiri maisha yako ya kimapenzi na mke wako.?

Ukweli ni kwamba kama una experience PE wakati unafanya mapenzi kawaida unakuwa umejawa na mawazo kwamba unaweza kumaliza mapema na matokeo yake huwezi kufurahia sex na huwezi ku-relax, pia mke wako anaweza kuwa haridhiki na matokeo yake atakuwa anakwambia kichwa kinauma kila siku ukitaka kuwa mwili mmoja hahaha!

Eti PE haiwezi kuathiri kujiamini kwako.?

UKweli ni kwamba kila mwanaume huwa anapenda kuwa mzuri kitandani, PE na kutomfikisha mke pale anahitaji kufika ni sababu tosha ya kupoteza confidence zako.

Eti PE huathiri wanaume wachache sana?

Ukweli ni kwamba wanaume wengi ni wahanga wa hili jambo kuliko watu wanavyodhani.
Hivyo si wewe unayesoma hapa ndo unahusika, huko nje kuna wanaume wengi tu wanakumbana na hii kasheshe, ila wengi wamechukua hatua na kuondokana na hili tatizo.

Eti ukiwa na PE huwezi kubadilika kabisa hivyo ishi nayo ni kilema chako.?

Ukweli ni kwamba kukubali kwamba ni kilema chako ni kosa kubwa sana.
Kufikiria hivyo ni kosa ambalo litakufunga wewe na mpenzi wako kwenye jela ya wale ambao ni wapweke wakati wapo kwenye ndoa.
Siri kubwa ni wewe kuweza kuthibiti PE (piga ua lazima uweze, kama wengine wanaweza kwa nini wewe ushindwe?)
Ukifanikiwa unaweza kuwa ni mwanaume smart sana kitandani ambaye hajawahi kutokea kwani utakuwa ni mwanaume unayejali, uliyejifunza na kugundua feelings zako na hisia zako na jinsi ambayo huwa unasisimka kwa muda wote kitandani na hii itakupa ujasiri wa kuwa mwanaume kiongozi kitandani na kila mwanamke huhitaji mwanaume kiongozi na ambaye ni caring.

No comments:

Post a Comment