Monday 21 December 2015

WIVU ULIOPITILIZA...!!

Wivu mbaya wa kupindukia
Wivu (envy) huu ni wivu ambao mtu anakuwa hana na anakihitaji au anataka mfano pesa, kuwa mshindi, kufanikiwa nk.

Wivu (jealous) huu ni wivu ambao mtu anakuwa na kitu na anaogopa kukipoteza mfano mume, mke, mchumba au mpenzi nk.

Pia kuna wivu mzuri ambao husaidia kuleta maendeleo na mafanikio kwa kila eneo la maisha ya binadamu kama vile kusoma kuhakikisha na wewe una degree, kufanya kazi kwa juhudi ili na wewe uwe na pesa nk

Hapa leo hatuzungumzii ule wivu unaompata mtu baada ya kusikia mume au mke wake au mpenzi wake anafanya mapenzi na mtu mwingine au anauhusiano na mtu mwingine, hapo naamini wivu lazima utakuwepo na kitu cha msingi ni kujihadhari usije ukaua mtu na wewe kufungwa maisha kwani haya tunayasikia kila siku kwenye jamii zetu mara mwanaume kamua mwanamke tena kwenye nyumba ya wageni na wakati mwingine baada ya kufumaniwa.
Masuala ya mahusiano si utani wala masihala, mahusiano hugusa hisia za mtu, huathiri mfumo wa maisha ya mtu hivyo inabidi kuwa makini na mambo unayofanya kwa mume au mke wako.

Hapa tunazungumzia ule wivu wa kupindukia ambao mtu anakuwa na mume au mke au mchumba au mpenzi na kwa kutojiamini kwake anahisi na kuona kwamba huyo mume au mke au mchumba anaweza kuchukuliwa na mtu mwingine au anaweza kumpoteza na wakati huohuo muhusika yupo Innocent.
Kama mtu unayempenda mke, mume au tuseme mpenzi ambaye anaumwa ugonjwa wa wivu, basi inabidi uwe makini kwani wivu katika mahusiano huweza kuharibu kabisa iwe ndoa au uchumba au vyovyote vile, hata kama hayo mahusiano ni mazuri na imara namna gani.
Ndiyo maana wivu ni moja ya dhambi saba zinazoua (deadly sin)


Kumbuka mtu mwenye wivu wa kupindukia kwake kila kitu kinachofanywa na mpenzi wake ni hatari na kitu halisi.
Wivu huweza kuharibu kabisa mahusiano bila kujali partner anafanya juhudi gani kuhakikisha anaweka vizuri mahusiano yenu.
Watu wenye wivu wa kupindukia siku zote wana mihasira isiyo na maana.
Mtu mwenye wivu wa kupindukia anaweza pia kupoteza hata mtu anayejua kupenda au mtu mzuri kwani hakuna mtu duniani anapenda kuishi kwenye kifungo cha mtu mwenye wivu wa kupindukia.

Kumekuwa na kundi kubwa la wanawake au hata wanaume ambao hulalamika kwamba hawapati wapenzi wazuri au kila ninayepata ananikimbia, inawezekana una wivu wa kupindukia hivyo mtu anapima hicho kimo cha maji na anajikuta atazama, hivyo anachoma daraja na kuondoka zake.
Ingawa kila mmoja wetu kwa asili ana wivu Fulani ndani yake, kitendo cha kuwa na wivu wa kupindukia kwa yule unayempenda tena wivu wa kila siku inaweza kuleta matatizo.
Wakati wivu unampata mtu, wapo ambao hujiona tayari mke au mpenzi wake ana taka kumsaliti na hujiona kama vile usalama wao upo mashakani na kwamba mwenzi wake anataka kuchukuliwa na mtu mwingine.
Si kwamba tu wivu ni mbaya bali mtu mwenye wivu hutafsiri vibaya yale mpenzi au mke/mume wake anayafanya au kile kinaendelea katika uhusiano.
Hata kitu ambacho hakipo huwezi kujitokeza na kusababisha kuwa tuhuma kubwa na kuanza kuvurugana ndani ya nyumba hata bila kuchunguza kwanza au kupata ukweli.
Ndiyo maana wapo wanawake na wanaume innocent ambao bado bado hawaaminiwi na waume au wake zao.
Mtu mwenye wivu humfikiria vibaya mwenzake hata bila sababu na kila kitu ambacho wenzake anafanya yeye ni kama anatega tu,
anaangalia utachelewa kazini,
utachelewa sokoni, utaongea na nani nk.
Kwa mfano, mke amepigiwa simu na mume wake mpenzi na simu inaita bila majibu au anaipokea baada ya muda, mwanaume mwenye wivu hapo kapata sababu atasema mengi sana mara hunipendi, au mara ulikuwa na nani au ulikuwa na mwanaume mwingine.
Na hata bila kujua ukweli anaweza kufikia uamuzi kwamba kuna kitu kibaya kinaendelea kumbe hakuna kitu.
Siku nzote ukiwa na mawazo hasi (negative), au mashaka na mtu, au kujisikia hakuna usalama matokeo yake utakuwa unazidi kutengeneza mawazo hasi zaidi, au mashaka zaidi na mwishowe kupoteza usalama kabisa wa ndoa na maisha yako na pia utakuwa mtu asiyeyaamini mahusiano yake.
Kuwa mtu mwenye wivu wa kupindukia katika mahusiano siyo kwamba inakuumiza wewe mwenyewe, bali inaumiza hata yule ambaye unamwonea wivu pia kwani hakuna binadamu anapenda kukaa karibu na mtu ambaye anageuza mazuri kuwa mabaya, anayekupa tuhuma na kutokukuamini wakati huna tatizo.
Ni ngumu sana kuishi na mume au mke mwenye wivu wa kupindukia, kwani hawa watu ni watu wanao penda control mtu kila eneo, ni watu wa kutaka kila kitu kama
anavyotaka yeye, ni watu wa kushambulia na wenye msongo wa mawazo pia, mtu unakuwa mtumwa kwenye ndoa, huna raha na watu wengine, huna raha na maisha nje ya yeye.
Matokeo yake mtu anaona kuolewa au kuoa ni kupoteza uhusu kwa watu zaidi ya yeye na wewe.

Wapo wanamke au wanaume wamepigwa marufuku kupigiwa simu na mtu wa jinsia nyingine au wamepigwa marufuku kuongea na watu wa jinsi tofauti hadi yeye awepo na kwenda mahali hata kama ni dharura bila kumwambia ili na yeye afuatilie.
Wapo wanawake hawaruhusiwi kufanya kazi maofisini kisa wivu eti watachukuliwa na wanaume wengine nani aliyekwambia wanawake ni rahisi kiasi hicho, kila mtu ana tabia yake na malezi yake.
Wapo wanawake hawaruhusiwi kwenda hata dukani au sokoni kisa wivu, hawaruhusiwi kusafiri kisa wivu, sasa maisha ni nini?
Wivu haufuati kabila unaweza kuwa mhehe, mchaga, au hata mkurya, unaweza kuwa mzungu au mwafrika, unaweza kuwa tajiri au maskini.
Kitu cha msingi jiamini kama huyo mume wako au mke wako amekupenda wewe hadi mkapelekana kanisani kufunga ndoa au mbele ya wanaohusika kisheria kwamba mnataka kuishi pamoja sasa una wasiwasi gani? eti atachukuliwa na mwanaume mwingine au mwanamke mwingine, hakuna kitu kama hicho, jiamini na mpe uhuru na mpende zaidi na kumpa kile anataka na kuhitaji, imarisha mapenzi zaidi badala ya kumlinda na kumchunga kama mbuzi.

No comments:

Post a Comment