Thursday 10 December 2015

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA MAHUSIANO.3

HATUA YA TATU NI MATESO, MAJONZI NA TABU.

Katika hatua hii Wanandoa hushangaana kwa nini kila mmoja amejiweka gundi kwenye njia zake bila kumjali mwenzake.
Na kila mmoja humwambia mwenzake ungebadilika kila kitu kingekuwa kizuri.
Kama ni mlevi basi hujichimbia mizizi na kuwa mlevi wa kupindukia, kama ni mlevi wa kazi basi ataondoka nyumbani asubuhi na mapema na kurudi midnight eti ana andaa future.
Hata akirudi nyumbani hukuta mke amelala na watoto wamelala na yeye mwenyewe yupo exhausted kiasi kwamba hawezi hata kumuhudumia mkewe.
Hapa ndipo affair nyingi huzaliwa, na ndoa huwa ni vilio, majonzi, Stress, BP, pressure, kukosa usingizi, Wanasheria wa mambo ya ndoa wengi hutajirika kwenye hatua hii ya ndoa hasa nchi zilizoendelea ambako kuachana ni jambo la kawaida tu.

Watoto wengi huachwa njia panda na kutojua nini cha kufanya maana mara kwa mara baba na mama hawaelewani.
Hapa ndipo tunafahamu kwamba kupigiana kelele, kulaumiana, kusuguana, kutishiana hakuwezi kubadilisha wapenzi wetu bali kukubaliana kwamba kuna tofauti na kushirikiana kutatua tatizo kwa hekima na busara hupeleka ndoa kwenda hatua nzuri zaidi.

Hii ni discovery stage ambayo wanandoa hujuana na ni opportunity ya kujifunza na kuzalisha true love.Wale wanaokimbia au kuomba talaka au kutoa talaka huenda kutafuta wapenzi wapya ambao hujikuta wameangukia the same boat na matatizo mapya na makubwa zaidi.

Na ndoa nyingi huvunjika hapa na kukosa kufikia stage inayofuata ambayo ni true love kati ya wanandoa.
Ndiyo maana tafiti nyingi zinaonesha kwamba baadhi ya walioachana kwa talaka kuna wakati hutamani kurudiana na wataliki wao au wangejitahidi kuvumilia na hatimaye kutatua matatizo kuliko njia ya kupeana talaka waliochukua.

Wapo ambao huona haina haja kuendelea na hii cold war na huamua kuchukua uamuzi wa kufanya investigation na kuchukua njia sahihi za kujenga mahusiano imara na yenye afya.
Hata hivyo wanaoamua kuchukua huu uamuzi bora wa imani huwa na milima na mabonde ya kupita kufikia hatua ya mwisho ambayo huwapa raha na experience ya ndoa mpya.

Fuatilia hatua inayofuata ambayo ndio hujenga ndoa zaidi..

No comments:

Post a Comment