Friday 4 December 2015

NI UFUNDI WA KUTATUA MIGOGORO KTK NDOA.

Wapo wanandoa ambao ni kama ua, hata audhiwe vipi anabaki kimya anaogopa asije akasababisha mwenzake kukasirika au kuzozana.
Wengine ni mwewe kitu kidogo tu ni kuzozana hadi yaishe.
Wewe je ni mwewe au ua?

1.MAWASILIANO YALIYO WEZA.
Wanandoa lazima waongee kwa uhakika wao wenyewe kila mmoja kwa mwenzake kuelezea hisia za ndani kabisa na kila mwanandoa lazima amtie moyo mwenzake.

2.KUONESHA UPENDO WA KWELI NA KUJALI
Wanandoa lazima wawe na uwezo wa kuonesha upendo na kujali mwenzake hasa ili kuzuia hali ya kuzolota tabia ya kupenda mwenzake kila wanapoendelea na maisha na kuishi.

3.MAPENZI NA FARAGHA
Wanandoa ni muhimu kila wakati kuchochea mahusiano ya tendo la ndoa linaloridhisha ili kuwa na mahusiano imara na wawili kuwa na faragha pamoja.

4.KUTATUA MATATIZO NA MIGOGORO.
Wanandoa ni muhimu kuwa na ustadi, au busara au hekima na uwezo wa juu sana kumaliza migogoro au tatizo au tofauti yoyote inapojitokeza haraka iwezekanavyo.

5.KUYAMALIZA
Pia ni muhimu sana kwa wanandoa kuwa na hekima ya kujua jinsi ya kumaliza mgogoro kuliko kwenda sambamba kila mmoja bila kuridhika na uamuzi wa mwenzake, kama mmoja amekosa basi akubali amekosa hata kama wewe ni mwanaume na jamii inakuona kama waziri au mbunge au kiongozi mkubwa kwani ndani ya nyumba wote ni kitu kimoja.

6.MGAWANYO WA KAZI
Katika ulimwengu wa sasa ambao wanawake na wanaume wote huondoka asubuhi au muda wowote kwenda kuwinda kwa ajili ya mkate wa familia bila kuwa na mgawanyo mzuri wa kazi nyumbani mmoja huweza kulemewa na zaidi kuzusha migogoro mingine.
Hivyo basi wanandoa lazima wawe wanagawana kazi na kusaidiana vizuri na kila mmoja kumtanguliza mwenzake.

7.JINSI YA KUZOZANA
Ni vizuri kila mmoja kutoa dukuduku alilonalo au kama kuna kitu kinamuudhi au kinamsumbua au haridhiki nacho kwa mwenzake ni vizuri kukiweka mezani na kikamalizwa kwa kujadiliana kuliko kukaa na donge moyoni huku unaangamiza na afaya yako.
Wapo wanandoa ambao hata kama kuna jambo gumu limamuumiza hayupo tayari kumuuliza mwenzake kwa kuogopa wasije wakaanza kuzozana au kuogopa mwenzake asije akakasirika. Ukweli ni kwamba afadhari umwambie akasirike na muyamalize kuliko kukaa nalo moyoni.

No comments:

Post a Comment