Friday 4 December 2015

TUNAJIFUNZAJE KUHUSU NDOA?

Ndoa huweza kuwa ndicho kitu chenye furaha ya ajabu au kuwa kitu kinacholeta huzuni.
Mungu aliweka ndoa ili kumuunganisha mwanaume na mwanamke ili kila mmoja kati yao ampe mwenzake kila hana hata hivyo hizo tofauti zilizopo zinaweza kuwa sababu kubwa ya hawa wawili kuwa vipande badala ya kitu kimoja.
Kumpenda na kuhishi na mwenzi wako ni kazi ya kujitolea kila siku na zaidi kufanya mema kwa ajili ya mwenzi wako.

Matatizo au migogoro au kutofautiana katika ndoa ni kitu cha kawaida na huweza kuleta matokea mazuri kwani wanandoa wanaotatua matatizo vizuri hujikuta wanafahamiana na matokeo hujuana na hujenga ndoa imara.

Ukweli kama kuna ndoa ambayo wanadai hawana hata tofauti au kupishana kwa njia yoyote basi mmoja ya wanandoa amekufa ni mfu au wameamua kula jiwe tofauti zilizopo huku moyoni kila mmoja akiumia kwa jina la amani.

Kwa migogoro katika ndoa wengine ni faida na wengine huwaangamiza

Mmoja anakuwa ametoka katika familia ambayo wakati wa migogoro na zogo wazazi wake walikuwa wanaishughulikia vibaya kama si kuikwepa au kuiacha.
Hivyo hata baada ya kuishi na mke au mume huamini njia waliyotumia wazazi wake ni sahihi. Unapoamua kuoa au kuolewa unatengeneza ndoa mpya duniani ambayo inahitaji njia sahihi ili kutatua matatizo na migogoro.

Inawezakana mmoja au wote wanaamini kukitokea mgogoro wowote wa ndoa ni kitu kibaya, wanaamini wakijaribu kutatua hawataweza.
Migogoro hutokea kwa sababu ya toafuti za kimawazo na kuijaribu kuitatua kwa upendo na hekima kila mmoja akijaribu kuwa sehemu ya suluhisho hujenga ndoa

Wanaamini amani ni pamoja na kutunza matatizo bila kuyaongelea au kutatua. Wanaogopa kuzungumzia matatizo na tofauti zilizopo kwani wanaweza kuwasha moto wasioweza kuuzima.
Hakuna kitu kibaya kama kutunza jambo moyoni ni sawa na magari mawili ambayo yanaelekea kwenye ahead on collision siku ikifika enough is enough hapatatosha.

Wanafahamiana juu juu tu na hivyo kuyajadili matatizo yanayojitokeza ni kuingilia business ambazo ni kuingilia others stuff.
Ukiingia kwenye ndoa kila kitu ni deep hakuna cha others stuff kwani kujuana ni pamoja na udhaifu na uimara na kwa njia hii hujenga intimacy.

Hawajiamini hivyo mgogoro ukijitokeza wanaongea sana ili kujilinda badala ya kusikiliza na kujua watatue vipi.
Tatizo lolote au mgogoro wowote ukijitokeza ni muhimu kila mmoja kutulia na kusikiliza kwa makini kabla ya kuanza kuongea.
Wapo wanaume (si wote) mke hata kama hajamaliza kuongea yeye hudakia na kusema “najua unataka kusema kitu gani” Mke hujiona hajasikilizwa na mgogoro huweza kupanda kutoka kichuguu na kuwa mlima kilimanjaro.

Kila mmoja analenga kushinda au kwamba yeye ni sahihi kuliko mwenzake matokeo yake wanashindwa kutatua na wanaongeza tatizo kuwa kubwa zaidi.
Kumbuka hakuna mtu ambaye yupo sahihi kila siku au siku zote; ni muhimu kutambua kwamba kuna wakati tunakosea na tukubali tumekosa na tuombe msamaha.

No comments:

Post a Comment