Friday 4 December 2015

NI WEWE NDO WA KUAMUA KWANZA.

Wakati mwingine hata ndoa ambazo huonekana nzuri huweza kushindwa na zile zinazoonekana mbaya hudumu.

Zipo ndoa ambazo wawili huishi kwa mipaka hadi unashangaa sasa kwa nini inaitwa ndoa, kwa mfano mume au mke anatakiwa kuongea kwa mahesabu kwani akikosea neno anaweza kumkasirisha mwenzake na nyumba ikawa haikaliki na hakuna ladha kabisa kuongea na partner wake matokeo yake hata wakiwa wawili hakuna cha maana cha kuongea na kila mmoja hujibakia bubu kwani hujiona ni bora kuwa bubu kuliko ukaongea na ukawasha moto usioweza kuuzima.

Na mwingine hataniwi hata akifika nyumbani kutoka kazini si mama si mume au watoto wanajua kwamba baba amerudi au mama amerudi kila kitu sasa ni moto.
Swali la kujiuliza je, kwa nini uwe hivyo na unapata faida gani kuwa hivyo?
kwa nini familia iwe na nyoka mtu?

Pia wapo wanandoa ambao huwa hawakubali kushindwa hasa pale kukiwa na tofauti ya mawazo au kutoelewana kati yako.
Kila siku wewe ndiye upo sahihi na kila siku mwenzako ndiye anakosea, haiwezekani binadamu wawili wakaishi pamoja na kila siku au mara zote mmoja ndo anayekosea, huo si ustaarabu na ni ubabe tu.

"Ijulikane kwamba ndoa hurekebishwa kwa kuanza na wanandoa wenyewe, wanaweza kwenda kwa wazazi au marafiki au majirani au mchungaji, au padre au washauri maarufu wa ndoa au mtu yeyote mwenye utaalamu wa kushauri masuala ya ndoa, kama wanandoa wenyewe hawataki kujirekebisha na kuweka mambo sawa tangu chumbani mwao, mawazo au ushauri wa wengine hauwezi kupenya kwenye maisha yao ya ndoa na kuleta mabadiliko".

No comments:

Post a Comment