Thursday 3 December 2015

KUBADILI JINA BAADA YA KUOLEWA.

Hivi karibuni kumekuwa na kujiuliza kwingi kwa akina dada ambao wanatarajiwa kuolewa kama anaweza kubadilisha jina la ukoo na kulichukua lile la mume wake.
Wengi wamejikuta wakifanya huku hawajafahamu maana au kwa nini wanachukua hatua kama hiyo hata hivyo ni vizuri kufanya jambo ambalo una uhakika na ufahamu wa kutosha kuliko kufuata tu traditions na taratibu ambazo ni kama kufuata mkumbo.

Pia kuna maswali kwamba je, kubadilisha jina baada ya kuolewa ni suala la kibiblia au ni mapokeo tu na zaidi kwa nini wanaobadili majina ni wanawake na si wanaume.

Je, kubadili jina nyakati za leo kuna manufaa yoyote kimaadili na kiimani?

Wanaharakati wa mambo ya wanawake. wanasema haina haja kubadili jina maana mwanamke anapoteza identity yake na kila kukicha wanawake wanaoolewa kwa hiari yao huamua kubadilisha majina yako na kuendelea kufurahia maisha ya ndoa na waume zao wapya.

Kwa nini anayebadilisha jina ni mwanamke na si mwanaume?

Traditions ambazo ni biblical zinaonesha kwamba kwanza Adamu aliumbwa ndipo Eva (Hawa) na Eva alitoka katika ubavu wa Adamu.
Adamu na Eva baada ya kuunganishwa wamekuwa mume na mke yaani mwili mmoja (one couple).
Mungu amewaunganisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja kufanya kitu kimoja na mke ndiye amemfuata mume (kipande cha ubavu kilichotolewa ili kumuumba Eva) kuwa kitu kimoja kupitia agano la ndoa.
Mbele za Mungu wanandoa wawili mke na mume huwa ni kiumbe kipya kimoja kinachoitwa ndoa moja, hii ina maana kwamba ingawa mwanaume mmoja ambaye hajaoa huonekana ni mtu mzima kiroho bado huwa nusu na huhitaji kuunganishwa na nusu nyingine ya mwanamke kufanya kitu kimoja yaani ndoa.
Mwanaume huwa hajakamilika hadi anapooa na mwanamke huwa hajakamilika hadi aolewe.
Mwanamke kuchukua jina la mume ni kuipa heshima ndoa na kudhihirisha kuwa kitu kimoja kipya kimezaliwa.
Mke anapoolewa hudhihirisha kwa ulimwengu kuwa amepata identity mpya na anatambua uumbaji wa kimungu kupitia ndoa.
Baada ya kuolewa anaingia kwenye agano jipya kati ya mke na mume na Mungu.

No comments:

Post a Comment