Thursday 10 December 2015

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA NAHUSIANO. (MWISHO)

HATUA YA NNE NI KUUNGANISHWA.

Jambo linalohuzunisha ni kwamba nusu ya mwanaume na mwanamke wanaoamua kuishi pamoja hushindwa kufikia hii hatua ambayo mateso, maumivu, uchungu na kuvumilia kote huanza kulipa.
Asilimia kubwa ya ndoa zinazovunjika sababu kubwa ni kukosa maarifa hasa kabla ya wawili kuamua kuishi pamoja hivyo huingia kwenye ndoa wakitegemea ndoa itakuwa tambarare kama nyikani au watakutana na vichuguu kumbe kuna milima na mashimo.

Hapa mnakuwa mmeshirikiana kutengeneza historia na kwa pamoja mnakubaliana kwamba kweli ndoa haikuwa rahisi hata hivyo mnajisikia proud kwa kuwa mmeshinda hurricanes na storms zote pamoja.

Kila mmoja anamshukuru mwenzake kwa commitment kubwa na dedication aliyoiweka kuhakikisha ndoa inafika mwisho kwa uvumilivu wa hali ya juu, pia mkiangalia mlikotoa mnajisikia ni kweli ninyi ni wanandoa wa tofauti.
Kila mmoja anajiskia yupo karibu na mwenzi wake na more connected kimwili, kihisia na kiroho, pia kila mmoja hujisikia amepata hamu mpya na kubwa kwa mwenzi wake hasa Kutokana na kupoteza muda mwingi wa kuwa intimate kwa kushughulikia migogoro kila mmoja anajiskia yupo nyumbani tena.

Hujikuta zile qualities ambazo uliziona mwanzo kabisa kumbe bado anazo na unaanza kujiunganisha kihisia upya kwa kuwa sasa mnafahamiana vizuri pande zote za maisha yaani strength na weakness.Hii ni hatua ya furaha, hatua ya mapenzi ya kweli, true love, divine love, unconditional love.

Wanandoa wa hatua hii hata watu wengine huwa-admire kutokana na jinsi walivyoshinda aina zote za majaribu.
Wanakuwa role model kwa jamii.

Kama wanandoa wote wangejua kwamba ndoa huwa katika hatua mbali mbali na kwamba mbele ya safari inalipa, basi wangekuwa tough kuhakikisha wanavumilia na kushinda.

Hata hivyo wengi huamini stage (kama kuna matatizo) waliyopo itakuwa ya kudumu na kwamba watakuwa hapo forever, ni kweli ukiwa na wakati mgumu huumiza na hukatisha tama lakini kumbuka “No situation is permanent” hata kama ndoa imefikia hali mbaya kabisa bado huwa na dalili za kuiokoa ni muhimu kuelekeza nguvu hapo.

Ndoa imara si ile isiyokutana na dhoruba bali ni ndoa ambayo inazishinda aina zote za dhoruba nakuendelea mbele kwa kasi ya ajabu.

KUMBUKA;
Si lazima ndoa yako ipitie hatua zote 4 unaweza kuwa kwenye hatua ya kwanza miaka yako yote huku kukiwa na vimsuguano vidogo vidogo kama utaruhusu Kristo kuwa kiongozi wa ndoa yako kwani kama yeye anavyolipenda kanisa basi mume na mke wanahitaji kuishi kwa mfano wa Kristo na kanisa.

Muwe na Ndoa na Mahusiano Mema Wapendwa.

No comments:

Post a Comment