Thursday 24 December 2015

SI HAKI YAKO,NI ZAWADI.

Mungu alitoa sex kama zawadi kwa waliooana.
Ametoa zawadi ya sex ili kutufundisha kuhusu yeye na uhusiano wake na sisi.
Utendaji wa sex ni picha ya muunganiko (sharing) kwa kutoa vyote kwa mwenzako (mke au mume) na pia ni picha ya kumkubali kumpokea mwenzako kama alivyo kwako.

Kuna faida wazi kabisa kwa uhusiano wa tendo la ndoa kwa mke na mume kama vile afya ya mishipa, kupunguza maumivu, kufanya MP kuwa stable, kupunguza depression (unyonge wa kihisia), kupunguza (stress) msongo wa mawazo na kuongeza kuridhika kwa mahusiano ya ndoa.

Mungu anawapa uhuru wanandoa kunywa na kufurahi raha ya mapenzi kila mmoja kwa mwenzake kama wanandoa, hata hivyo sababu za kiroho na kisayansi haziwezi kutumika kama silaha ya mwanandoa mwingine kumthibiti mwenzake.
Uwezo wa kimapenzi kati ya mke na mume bado ni zawadi ambayo tunatakiwa kupeana bure na kwa kupenda na kwa moyo wa furaha (kutoa na kupokea kila mmoja kwa mwenzake katika ndoa).
Pale mwanandoa mmoja anapokuwa na mtazamo kwamba tendo la ndoa ni haki basi kunakusinyaa kwa aina fulani katika mahusiano huanza kujitokeza.
Mke hawezi kuwa na raha ya mapenzi katika ndoa kama mume atakuwa ni mtu wa kulazimisha na kutaka kwa nguvu kama haki yake na pia si raha sana pale mke anapotoa tendo la ndoa kwa sababu anawajibika kutoa hata kama hakuwa tayari.

Tendo la ndoa linaloridhisha ni pale kila mwandoa anakuwa amejiadabisha kutoa kwa uhuru mwili wake kwa mwenzake.
Unapotoa kwa uhuru mwili wako kwa mume au mke wako na kupokea mwili wake kwa uhuru unaipa ndoa kitu sahihi cha asili yake na Mungu hufurahia na kutoa kibali.

1 comment:

  1. Baada ya miaka 5 katika ndoa na mume wangu na watoto 2, mume wangu alianza kufanya tesa na kutoka nje na wanawake wengine na akanionyesha mapenzi baridi, kwa mara kadhaa anatishia kunitukana ikiwa nitathubutu kumuuliza juu ya uhusiano wake na wanawake wengine, mimi iliharibiwa kabisa na kuchanganyikiwa hadi rafiki yangu wa zamani akaniambia juu ya simulizi ya spell kwenye wavuti inayoitwa Dr.Wealthy ambao husaidia watu walio na uhusiano na shida ya ndoa na nguvu za miiko ya upendo, mwanzoni nilitilia shaka ikiwa jambo kama hilo litakuwapo lakini aliamua kujaribu, nilipowasiliana naye, alinisaidia kutoa upendo na ndani ya masaa 48 mume wangu alirudi kwangu na kuanza kuomba msamaha, sasa ameacha kwenda nje na wanawake wengine na wake pamoja nami kwa uzuri na kwa kweli . Wasiliana na cell hii kubwa ya upendo kwa uhusiano wako au shida ya ndoa kutatuliwa leo kupitia: wealthylovespell@gmail.com au moja kwa moja WhatsApp: +2348105150446.

    ReplyDelete