Monday 14 December 2015

UTAZIDI KUUMIA..!

Tafadhari chukua glass ya maji mkononi, usisome tu naomba kama unaweza chukua glass jaza maji na ishike mkononi.

Swali ambalo naweza kukuuliza ukisha ichukua mkononi ni je, glass ya maji ni nzito kiasi gani?
Naamini jibu ni kwamba haina uzito wowote.
Upo sahihi na umebarikiwa kwa jibu zuri.
Hata hivyo ukweli ni kwamba hata kama uzito wa glass yenye maji si lolote, kama ukiishika kwa zaidi ya saa moja utaanza kusikia uzito wake, unavyozidi kuishika kwa muda mrefu ndivyo utajisikia uzito unaongezeka zaidi ingawa uzito wa glass ya maji ni ule ule.
Utajisikia mkono kuanza kuuma na kulemewa na uzito kama vile umeshika bonge zito la tofali la sementi.

Ndivyo mahusiano ya ndoa yanavyofanya kazi wakati mwingine.

Kuishi wawili ni sharing ya mambo mbalimbali na kuna wakati mwenzako anaweza kukwaza, kukuumiza, kukusema vibaya, kufanya vibaya, kukutukana, kukudanganya nk na kila kitu unafanya kwake au wewe unafanyiwa kina uzito mkubwa au mdogo sana moyoni kwa partner wako.
Hata hivyo unavyozidi kutunza vitu vidogovidogo vinavyokuumiza moyo bila kuviweka wazi kwa mwenzako ili muongee na kuyamaliza. Siku zinavyoongezeka na kwenda itafika siku mkusanyiko ya hayo mambo moyoni mwako utaanza kuwa mzito na kujisikia vibaya kwa mwenzako.


Inawezekana chanzo cha hasira zako au uchungu ulionao au maumivu uliyonayo nk ni matokeo ya vitu ambavyo uliweka moyoni mwako miaka 5 au 10 au 25 iliyopita katika ndoa yako.
Kubwa zaidi hukufanya juhudi yoyote kuhakikisha unaongea bayana na wazi kwa mke wako au mume wako na kutokana na hiyo tabia leo umefika hapa baada ya hayo mambo kujijenga kwenye moyo wako kwa miaka zaidi ya 5 nk.

Huku mwenzi wako akiwa amesahau hayo mambo, wewe umeendelea kuyashika ndani ya moyo wako na ni wewe unayeumia kwani mwenzio hajui kama bado yapo moyoni mwako.

Hata ukimwambia leo anaweza kuwa shocked kusikia kwamba bado ulikuwa umeweka jambo au mambo kama hayo moyoni.
Kwa kuwa umeshindwa kuachilia imefika mahali umeona ndoa haina maana kwako, haikupi furaha na unaanza kufikiria mlango wa kutokea
Unajisikia humpendi tena mume wako au mke wako.
Badala ya kidonda kupona sasa inazidi kuwa fresh.
Na kidonda kinazidi kuliwa na wadudu na damu kutoka bila wewe kujua.

Jifunze kuwa wazi na kuongea kwa mpenzi wako kama amekukosea mwambie na msahemeane na kusahau yaliyopita.

No comments:

Post a Comment