Monday 14 December 2015

KWANINI HUGOMBANA BAADA YA NDOA?

Mahusiano ni kitu special na maalumu na wakati mwingine hushangaza sana.
Hivi inakuwakeje wapenzi wengi hugombana baada ya kuoana tu?
Ni mara chache sana kuwaona wachumba wakigombana.

Issue hapa ni kwa nini watu hugombana baada ya kuoana na wakati kabla ya kuoana kila mtu alikuwa anamuelewa mwenzake hadi wakafikia hatua kukubaliana kuoana na wakioana tu mambo huanza, yaliyojificha huanza kuwekwa juu ya meza?

Ukiangalia kwa undani sana utakuta kwamba kabla ya kuoana mambo mengi unafanya ni hiari na baada ya kuoana ni wajibu.

Kabla ya kuoana una options kwa maana kwamba unaweza kujitoa au kuendelea naye na baada ya kuoana hakuna options, mwisho wa reli,hakuna njia, unafungwa kwenye box hakuna kutoka.

Pia kabla ya kuoa wengi huwa hawawi 100% honest, kila anachofanya kwa mchumba ni kizuri kwani uchumba huhusicha social activities na romantic interest, so wengi hufungana kamba kwamba everything is ok, hata kama hapendi au anaona kina bore bado atajifanya anakipenda na hakuna shida. Mkioana hakuna kufungana kamba wala kufurahishana ni task oriented institution na deep sharing ya kila kitu na ni real life na kazi.

Mfano:
Jeffy amependana na Anitha (siyo majina halisi) na ni wachumba ambao si muda mrefu watafunga ndoa kuwa mke na mume.
Jeffy anapenda sana kwenda kutazama Soka, imefika siku Yanga na Simba wana mechi na Jeffy hawezi kukosa anamwambia mchumba wake leo naenda kutazama mechi Yanga na Simba wanacheza je tunaweza kwenda?
Anitha hapendi ila kumfurahisha mchumba wake anakuali waende na tiketi zinakatwa wanaenda, wanafurahi na Anitha anashangilia mchezo bega kwa bega na mpenzi wake Jeffy.

Wiki inayofuata Anitha anajiunga na kwaya kanisani na anamuomba awe anamsindikiza kwaya na ikiwezekana wakimaliza anamrudisha nyumbani kwa wazazi wake, kwa kuwa Jeffy anataka kuonesha anajali hana shida yupo tayari kukodi hata Tax mpenzi awahi kwaya church au akimaliza kwaya aende nyumbani salama (moyoni Jeffy hapendi kwaya anampenda Anitha tu na anafanya ili Anitha afurahi).

Baada ya kuoana, kuna mechi ya Yanga na Simba na Heffy anamuomba Anitha waende kutazama mechi,Anitha anakataa kata na kutoa sababu kwamba hapendi kwenda kupoteza muda kwa kuangalia Yanga na Simba wakati ana mambo ya msingi ya kufanya.
Jeffy anashangaa kwani kabla ya kuoana alisema anapenda. Anaoana amedanganywa.

Wiki inayofuata Jeffy anaombwa na mke wake Anitha amsindikize kanisani kuimba kwaya, Jeffy anakataa kwa madai kwamba ana kazi za msingi sana kuliko kwenda kumsindikiza mkewe kwaya na hata hivyo si anaweza kwenda mwenyewe na kurudi kwani kwaya si huduma yake (Jeffy anajitetea). Mke wake naye anashangaa inakuwaje kabla ya kuoana alikuwa ananisindikiza hata kunitafutia tax ili niende na kurudi salama leo inakuwaje?

Je, wewe hujawahi kuwa Jeffy au Anitha katika mahusiano yako?

Orodha ya mambo huendelea na inafika mahali kila mmoja anajiona kama amedanganywa kwani Yule alitegemea amebadilika hapo frustration na disappointments huanza na migogoro huanza na kama wajinga wote kunaanza disconnection ya emotions kimwili na kiroho.
Hapa mmoja anajisikia hasikilizwi not understood, valued, loved au appreciated, kila mmoja anapenda mwenzi wake amsikilize, amwelewe na ampe thamani ya kila anafanya.
Kila mmoja anajiona mwenzake haweki msukumo wa kutosha kuhusu Mahusiano yao na kwamba yeye si kipaumbele tena ndipo closeness huanza kupotea.

Ukweli ni kwamba disagreement ni part of marriage, huwezi kukwepa muhimu ni kuzingatia kwamba unahitaji kuwa
Positive,
Fanya kila kitu katika wakati wake,
Uwe unachunga mdomo wako,
Usibishane au kugombana na spouse wako mbele ya public,
Ukikosa kubali na omba msamaha na wote kusameheana na kusahau
Zaidi mawasiliano ni muhimu sana.
Usimlaumu mwenzako badala yake fahamu kwamba sasa unaishi kwenye realm life hivyo changamka na mpende Zaidi ikiwezekana Fanya yale ulikuwa unafanya hata kabla hamjaoana.

No comments:

Post a Comment