Saturday 27 June 2015

NAMNA YA KUMSAHAU MPENZI ULIECHANA NAE.

Namna ya kumsahau mpenzi uliyemwacha kwa sababu za kukosa uaminifu na namna ya kuuponya moyo ulioumizwa.
Na pia namna ya kurudi katika hali ya kawaida baada ya kuachana.

Mahusiano ya uchumba yanaweza kuwa complicated kiasi cha kuweza kufikia hatua ya wawili waliopendana kuachana.
Kibaya zaidi ni kwamba wakati wawili waliopendana wakiachana mmoja wao huvunjwa moyo na kupata maumivu yasiyoelezeka kiasi cha kuwa na wakati mgumu kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Huumiza sana kusahau mambo yote (story, memories, ndoto na plan za maisha) ambayo walifanya pamoja.

TUKUMBUKA KWAMBA:
Kuuponya moyo ulioumizwa huchukua muda na uvumilivu.

Tuangalia hatua zifuatazo ambazo zinaweza kuwa mwongozo katika kuponya moyo wako ulioumizwa na kusahau kabisa yale yaliyotokea.


1:-Toa machozi kwa kadri unavyoweza na lia kwa kila sababu unazoamini zimefanya uumie.
Ukiwa umeumizwa ni kawaida au vizuri kulia machozi kwa uwezo wako wote.
Usifikirie kabisa kwamba eti kulia machozi ni kuonesha wewe ni dhaifu, kulia machozi ni kitu cha kawaida na vizuri sana kulia machozi baada ya kuumizwa.
Unapolia machozi unaondoa hasira na kuumia na kujiona umetua mzigo mzito.
Kama unaweza jifungie chumbani, jifungie weka muziki wa sauti ya chini, halafu ruhusu maumivu uyasikie na lia kwa machozi hadi unahisi mzigo kuwa mwepesi.
Jambo la msingi hapa ni kuondoa maumivu na ruhusu maumivu yaondoke.


2:- JISHUGHULISHE. (busy)

Ukitaka kumuondoa mtu kwenye kichwa chako lazima uweke vitu vingine humo kichwani mwako.
Fanya kitu chochote kinachoweza kufanya ubongo wako ujishughulishe ili kuharibu wazo la kuanza kumfikiria yeye.
(fanya kazi yoyote, angalia movie [siziwe movie za mapenzi], safari, shiriki michezo yoyote)
Tafuta kitu ambacho unakipenda kufanya, kitu kinachofanya akili yako kuwa busy ili kuziba nafasi ya kumfikiria mtu ambaye unajitahidi kumsahau katika maisha yako.


3:- TUMIA MUDA WAKO NA RAFIKI ZAKO.

Marafiki ni muhimu sana hasa katika hatua au nyakati kama hizi.
Kwani wanaweza kukufanya ujisikie vizuri na kukufanya wazo la huyo mtu kutokuja kirahisi.
Marafiki huweza kukufanya ucheke na kujiona wewe ni muhimu sana kwao.

ONYO
Waambie mapema rafiki zako wasiongelee kabisa kuhusu huyo mtu ambaye unajitahidi kumsahau.
Wakifanya kosa la kumtaja mara kwa mara unaweza kujikuta badala ya kucheka unaweza anza kutoa machozi.
Hivyo uwe mkweli na waambie wasimtaje kamwe.

Step 4:
4:-MKWEPE, EPUKANA NA HUYO MTU.

Usiende sehemu ambazo unaweza kukutana naye.
Kama unataka kumsahau mtu na unaendelea kukutana naye, huwa ngumu sana kumsahau.
Ukikutana naye Mahali uwe mwema tu, ila haraka iwezekanavyo mpige chenga na kwenda zako kama vile wametangaza kwamba kuna terrorist bomb limefichwa hilo eneo.
Kama unafanya naye kazi ofisi moja au unasoma naye darasa moja (chuo) basi inabidi usiwe unamwangalia sana na kuongea naye, uwe mwema tu na busy na mambo yako.


5:-USIJIFUNGIE NDANI, TOKA NJE KUTANA NA WATU WENGINE WAPYA.

Kujifungia ndani kwa muda mrefu huweza kusababisha process kuwa ngumu zaidi, hata kama unajisikia huna mood unachotakiwa kufanya vaa vizuri (pamba za uhakika, viatu cha uhakika, smile la uhakika) waite rafiki zako na mnaweza kwenda sehemu mkafurahia maisha (siyo kuutwika na uhuni) bali mambo mazuri.
Ukirudi nyumbani baada ya kuwa na rafiki zako na kuonana na watu wengine wapya utagundua kwamba yule uliyeachana naye kumbe si peke yake mwenye smile zuri au sauti, wapo na wengine.
Mungu apewe sifa kwani kuna watu wengine wenye sifa nzuri kuliko huyo unayetaka kumsahau wapo huko nje wanatafuta watu wenye misimamo mizuri kama wewe.


6:-EPUKA VITU VINAVYOHUSU MAPENZI.

Kama unataka kumsahau mtu ni muhimu sana kujiepusha na kusikiliza miziki inayoimba mambo ya mapenzi, movie zinazohusu mambo ya mapenzi kwani huweza kukufanya ujisikie vibaya na kuanza kumkumbuka yule mtu ambaye kwanza ndo unataka kumsahau.
Haijalishi ni Wimbo unaoupenda kiasi gani kama unaimbwa Radioni badilisha channel, na weka nyimbo za furaha (gospel songs ni nzuri sana)
Jambo la msingi unatakiwa kuepuka ni kitu kinaitwa mapenzi kwa wakati huu.


7:- JIFUNZE, JILINDE, JIPE FURAHA.

Wanawake wengi baada ya kuumizwa huanza kujimaliza wenyewe.
Si busara kuacha kujipamba na kuanza kujinenepesha kwa chocolate na sukari eti kwa sababu huna mtu, au kumkomoa uliyeachana naye.
Kinachotokea unakuwa huvutii na unapoteza kujiamini (self confidence).
Usiruhusu maumivu ya kuachwa au kuachana kukumaliza wewe mwenyewe.
Fanya mazoezi, kula chakula bora, fanya kazi, jipambe zaidi ya zamani ili ujisikia mzuri na ujiamini.


8:-KUBALIANA NA HATUA ULIZOCHUKUA.

Unaweza kuwa upo imara sana katika haya maamuzi ya kuamua kuachana na kuponya moyo wako na bado moyo ukaendelea kuumia.
Kumbuka hizi ni hatua na hatua hizi huchukua muda na uvumilivu na lazima ukubaliane.
Huwezi kumsahau mtu kwa siku 5 kama ulipendana naye kwa miaka 3.
Huwezi kujifanya upo imara na huwezi kulia machozi, kubali na kabiliana na hiyo hali hata kama itachukua muda.
Unapokuwa na subira, mambo huwa rahisi sana baadae.

No comments:

Post a Comment