Saturday 27 June 2015

MKE MMOJA,MUME MMOJA.

Kuna neno moja ambalo ni neno la msingi na muhimu sana linapokuja suala la ndoa hasa katika lugha ya kingereza nalo ni loyalty.
Maana ya hili neno ni kuwa mtiifu, au mwaminifu kwa hali ya juu iwe katika biashara au mahusiano nk.
Ni neno linalofanana na neno allegiance, truth, faithfulness.
Mke wako anafahamu kwamba yeye ni mke wa mume mmoja, anajijua kwamba yupo committed kwako 100%
Lakini kuna wakati mke wako Hujiuliza maswali kama ni kweli wewe ni mume wa mke mmoja, hasa pale anapokuona unavutiwa na mrembo/warembo unaokutana nao mtaani au hata kwenye TV.
Ni kweli ulikubali kwenda mbele ya kanisa ili kukubali kwamba unataka kuwa na ndoa ya mke mmoja hata hivyo namna unaishi na yeye inampa wasiwasi kwamba wewe ni mume wa mke mmoja.
Mke wako amekuwa insecure kwenye eneo hili na anahitaji reassurance na si wewe kumtania au kuleta dhaka au kuleta mahoka au kufanya masihara au kuleta mizaha au jokes au kuleta matani au kutumbuiza au kufanya Vichekesho au michezo.
Yupo serious anahitaji umuhakikishie kwamba wewe ni mume wa mke mmoja kama ulivyomuahidi hata ukaamua kufunga naye ndoa takatifu ya mke mmoja na mume mmoja.

Je, umewahi kufikiria namna ilivyo ngumu kwa mke wako kukuamini kwamba wewe ni mume wa mke mmoja hasa kutokana na wanaume wengi wanavyo- cheat, dunia inavyopambwa na kila aina ya warembo, dunia ilivyojaa wanawake wanaoshawishi wanaume kwa kuvaa wanavyotaka wao, namna Tv, Radio na internet zinavyopotosha watu kuishi kwa uadilifu katika ndoa?
Unahitaji kumhakikishia kwamba wewe ni mume wa mke mmoja!


Wanaume wote tunahitaji kujifunza kuwa

Mke anapokuwa na uhakika kwamba mume wake amefanya agano (covenant) na Mungu kwamba atajitahidi kumfanya Mwokozi wa maeneo yote ya maisha yake pamoja na ndoa yake mke hujisikia salama.

Mke anapokuwa na uhakika wa upendo na uaminifu wa mume wake kwake anajisikia kuwa na nguvu na kuhamasika kuhakikisha ndoa inakuwa bora zaidi.

Hii ni kutokana na namna Mungu amemuumba mwanamke na ndiyo maana agano la ndoa lina msingi wa kuaminiana (loyalty) hadi kifo kwa wawili (mke na mume) wanapooana.


Mke hujisikia mume anaonesha loyalty pale;

Anapomuongelea vizuri mbele za watu,

Anapojihusisha na mambo mazuri kuhusu mke wake,

Anapomsaidia kutoa maamuzi yanayohusiana na watoto wake,

Anapokuwa hamsahihishi mbele za watu.


Pale anapokuwa hawatamani wanawake wengine,

Pale anapofanya ndoa kuwa kitu cha kwanza,

Anapokuwa hamlalamikii (critical) mke mbele za watoto na watu wengine,

Pale anapohusishwa katika mambo ya jamii hata kama wengine wanaona aibu kwenda na wake zao,

Pale anapowaambia watoto wanatakiwa kumheshimu mama yao,

Pale anapoongea positively na si negatively.

NB:
Mke uliyenaye anakutosha

No comments:

Post a Comment