Monday 29 June 2015

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA.

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA HUUMIZA SANA
Mume wa Jane alipokiri kwamba ni kweli “Nilikuwa na uhusiano na yule mwanamke”.
Jane alipata mshituko ambao hauelezeki ni zaidi ya shock ya umeme.

Kwanza alijiuliza
“Imekuwaje sikuweza kujua dalili kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea na nilikuwa mjinga kiasi gani nisijue;
je, nilikuwa sioni matatizo ya ndoa yangu hadi mume wangu anafikia hatua hiyo, nilikuwa kipofu kiasi gani?
Na huyo mwanamke ametumia mbinu gani hadi kumpata mume wangu nami nisijue?”
Alijiuliza hayo maswali huku machozi yakibubukika kutelemka kwenye mashavu kama mvua za Alnino.

Jane alijikuta yupo katika wimbi kubwa la msongo wa mawazo mazito, hasira na kutojiamini kukaongezeka.
Wakati mwingine alikuwa anafua nguo na ghafla anajikuta anaishiwa pumzi na mapigo ya moyo kubadilika na viganja kuanza kutoa jasho nyembamba kama vile amakutana na simba ghafla.

Wakati mwingine hata kama anatazama TV ili kupoteza mawazo, ikitokea kukawa na program inaonesha affair yoyote ya ndoa basi hujikuta hasira zinampanda na kuzima Tv na kuanza kulia kwa machozi.

Zaidi ya miezi miwili usingizi umeota mabawa na hakuwa na hamu ya chakula na matokeo yake afya yake ikaanza kuzorota na kila mtu akajua Jane anaumwa kwani ule uchangamfu wake na afya yake vinaleta maswali zaidi ya majibu.

Ingawa mume wake alikiri kwamba hawasiliani tena na yule mwanamke, bado Jane alijikuta bado anawaza na kupata picha ya mume wake akiwa anafanya mapenzi ya yule mwanamke na akajikuta anamthibiti mume wake kila movement anayofanya maana haaminiki tena na kitu kidogo tu kilimchukiza mno Jane.
Jane alijitahidi sana asiwaze kuhusu huyo mwanamke hata hivyo alivyokuwa anajitahidi kusahahu ndivyo alivyozidi kukumbuka na kuwaza zaidi na alijikuta mawazo kuhusu huyo mwanamke yanazidi kujirudia na kulata hasira zaidi.

Tukumbuke kwamba ni kweli affair huumiza sana na maumivu yake ni makali kimwili, kiroho na kihisia.
Kukiwa na affair huwezi kukwepa kuwa na msongo mawazo kama ya Jane.
Jambo la msingi ni kwamba Jane si mtu wa hasira za kupigana na kelele kama sisi wengine kwani angekuwa mwingine hapa pasingekalika kabisa.

Msongo wa mawazo huja na mawazo huja kutokana na issue kwamba yule unayemwamini kuliko mtu yeyote duniani anakuwa amekusaliti kirahisi hivyo tena bila wewe kujua.

Wanandoa ambao wanapambana na issue ya affair huwa na kiwango kikubwa cha depression kuliko matatizo mengine ya ndoa.

Ni kweli affair ni dhambi na chukuzo kwa Mungu na ni kitendo kinacholaaniwa kwa nguvu zote hata hivyo hata kama umeumizwa sana jambo la msingi ni kukumbuka kwamba huwezi kujisia hivyo (msongo na mawazo na hasira) milele.
Ukweli ni kwamba kujisikia hivyo upo sahihi na unatakiwa kuweka malengo mapya ya kurudi katika hali yako ya kawaida kitu ambacho naamini ni kigumu sana.
Unatakiwa kuhimili hali uliyonayo ili hayo maumivu na feelings ulizonazo zisikufanye kilema hata ukajiumiza zaidi kama vile kujinyonga au kunywa sumu kwani hapa ndipo utasikia mapenzi yanaua.

Ni muhimu kuchukua hatua Zifuatazo ili kurudi kwenye hali yako ya kawaida;
Jiruhusu mwenyewe kujisikia vile unajisikia, kama ni kulia, lia tena kwa machozi mazito, kama kukasirika basi kasirika na muuliza maswali anayehusika kadri ya unavyotaka ili kujua ukweli. Zaidi jikubali na ukubali kwamba ni kweli yametokea.

Tafuta mtu unayemwamini (mshauri, mchungaji nk) akusaidia kuhimili maumivu na uchungu ulionao kwani kwa kuongea na mtu unayemwamini maumivu huondoka.

Jitoe, jikabidhi (moyo) kwa Mungu.
Yeye peke yake ndiye anajua maumivu.
Mungu ametuahidi kutupa faraja wakati wa dhiki na maumivu hata kama shetani ana mpango wa kuharibu ndoa zetu bado tukiishi katika blueprint ya ndoa kama Mungu anavyotaka tutaishi maisha ya furaha amani na ushindi.

No comments:

Post a Comment