Thursday 28 January 2016

SECOND CHANCE..

Fikiria wewe ni mwanamke ambaye baada ya kuishi na mwanaume kwa muda unaoujua wewe na kwa sababu unazozijua wewe mwanaume hayupo tena na wewe.
Amekuacha na mtoto/watoto na baada ya kuponya majeraha ya kuondokewa au kubaki mwenyewe sasa unajiona upo katika hali ya kutafuta mwanaume anayefaa awe mume wako na ikiwezekana iwe ndoa yenye Baraka na inayokuridhisha.

Inawezakana ulifanya makosa huko nyuma ndo maana sasa upo “single mom” au inawezekana hukufanya makosa bali imetokea tu na umejikuta ni “super single mom” na unataka ujipe second chance na kwamba hupendi ufanye makosa ili kumpata mume anayefaa tena na ikiwezekana awe baba mzuri kwa watoto ambao tayari unao.

TAHADHARI.
Kumbuka hapa kuna mambo mawili wakati unaendelea na taratibu zako za kumsaka mume, kuna suala la kumpenda (fall in love) au kutimiziwa mahitaji uliyonayo (fall into needs)

Hii ina maana gani?
Inawezekana unahitaji baba mpya wa kutimiza mahitaji ya watoto wako au unahitaji mtu wa kukusaidia ili mambo ya fedha yawe sawa au unahitaji mtu wa kukupikia au unahitaji mtu wa kukufulia nguo au unahitaji mtu wa kukusaidia kulipa kodi ya nyumba au unahitaji mtu wa kukutimizia mahitaji yako ya mwili.
Kujiingiza kuolewa ukidhani ni njia bora ya kutatua matatizo uliyonayo ni kujiingiza kwenye crisis ya hali ya juu.

Kuolewa kunatakiwa kuwe na msingi wa upendo wa kweli wa kumpata mtu ambaye atakuwa mwenzi kwa upendo wa kweli ambao unavutia na kumkubali kama alivyo.

Je, ni mambo gani ya msingi kuyafuata ili kumpata mume mwema tena.

1.NENDA POLEPOLE.
Ili kumpata mwanaume anayefaa basi nenda polepole katika process zote mara tano ya ile ulifanya mara ya kwanza kwa mwanaume ulieshi naye.
Usijirushe haraka haraka kwa mwanaume wakati hujui hata jina lake la ukoo.
Pia usijiingize haraka na Kuamini yule aliekuacha atakoma kuringa kwani ndoa ni yako si yake na itachekesha sana siku ukisikia hata huyo mwanaume uliyejiingiza haraka sasa unajuta.
Nenda polepole na penda kidogokidogo, usikubali mapenzi kukufanya kuwa kipofu.

2.FUNGA KUFULI LAKO.
Ulishakuwa sexually active hadi ukawa na mtoto/watoto.
Unaweza kujikuta unaingia kupasha moto mashuka ya kulalia na usijisikie kukosa adabu au kuona ni kitu cha kawaida.
Akishakushika na kukupa kisses kwenye shavu unajiona mwili una “warm up” na unajisikia raha, usilemae utaweka rekodi mpya!
Kama ulishajua utamu wa tunda ni ngumu sana kupiga brake usilivamie tena hata hivyo kuwa na msimamo ndiyo silaha.
Mwambie wazi kabisa mchana kweupe kwamba
“Nakupenda, sitafanya sex hadi niwe nimeolewa na kama inakupa shida naomba uwe wazi maana sitabadilisha msimamo wangu hii ni kwa mwanaume yeyote anayetaka kunioa”

3.IWE SIRI.
Usiwaambie watoto/mtoto wako mapema eti umepata baba mpya au ndugu zako kwamba nimempata handsome wangu wakati hata hujui tabia yake vizuri.
Kama unaweza panga mipango yako nje ya nyumbani na huyo mtarajiwa wako na kama unaweza subiri hadi siku uone kweli una engagement ring kidoleni na matayarisho ya harusi yapo mlangoni.

4.KUBALIANA NAE WAPI MTAISHI:
Je, baada ya kuoana mtaishi kwenye nyumba yake au yako au mpya?
Je, mtakuwa mnalala kitanda kile ulikuwa unalala la jamaa yako wa zamani?
Je, mtakuwa mnalala chumba kilekile ulikuwa unalala na mzee?
Je, kama na yeye ana watoto na wewe unawatoto na watoto wa mmoja wakawa wanawaambia watoto wageni “hii siyo nyumba yenu” utajisikiaje?

5.UWE MVUMILIVU.
Kitu chochote kizuri hutumia muda zaidi na wakati mwingine husuasua hata hivyo uvumilivu hulipa.
Inaweza kuwa ngumu kuliko unavyotegemea kwani kumpata mwanaume atayaekuwa responsible kwa watoto wa mwanaume mwingine si rahisi.
Hivyo jiandae kulipa gharama na usitegemee mambo makubwa sana kwa ndoa yako mpya.

No comments:

Post a Comment