Sunday 24 January 2016

JE,WEWE UTAKUBALI?

Fikiria wewe ni binti (au mzazi wa binti) ambaye unataka kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma (illiterate) utakubali?

Ni kweli elimu ni kitu kizuri hata hivyo elimu si kigezo cha upendo.
Naamini kitu cha msingi kwa mahusiano yoyote ni upendo wa kweli, kujali, kufanana na kuelewana.
Ukweli binafsi nitakubali kuolewa na mwanaume illiterate kwani inawezekana ana sababu za msingi za yeye kutokwenda shule na baada ya kuoana tunaweza kushauriana ajiendeleakimasomo.
....alisema Judy

Ukweli nitaolewa na yule nimeamua na nimempenda na angalau awe ameelimika.
Sidhani kama nitaweza kukubali ombi la mwanaume yeyote kunioa wakati hana elimu yoyote na hajaelimika, je itakuwaje kwa watoto tutakao wazaa? Je anaweza kupata kazi nzuri kwa ajili ya kuleta kipato cha familia huku hajasoma?
Pia kwa kuwa mimi mwanamke nimesoma na yeye hajasoma maana yake hatufanani na kutokuwa na gap kubwa sana katika uelewa wa mambo kitu ambacho sikipendi.
......Margaret

Nimeona mfano halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaolewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote.
Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika.
Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto.
Sitakubali binti yangu ajiingize kwenye ujinga kama huo hata siku moja na pia nitajitahidi kuelimisha mabinti wasije ingia katika matatizo kama hayo.
.......Mrs Betty


Kama kuna upendo na kuna kufahamiana na kuelewana na kama ni kweli huyu mwanaume ana sifa ninazohitaji Ukweli nitakubali tuoane na nitaomba Mungu aniongoze.
............Julieth

Kwangu kuwa illiterate si kizuizi hasa linapokuja suala la mahusiano pale tu kukiwa na kuelewana kati yangu mimi binti na huyo mwaname na kama ana sifa zile niahitaji. Najua kuna matatizo na watu watasema sana kwa kumkubali huyo kaka ambaye hana shule kabisa hata hivyo kama kuna kujitoa na kumuomba Mungu hakuna lisilowezekana.
...........Esther

Binafsi siwezi kujiingiza kwenye jaribu la kijinga kama hilo na kuona na mwanaume ambaye hajaenda shule.
......Anne

Na Je, wewe msomaji ungekubali? Au unasemaje

No comments:

Post a Comment