Friday 22 January 2016

MAPENZI BAADA YA KUOANA?

"Nilidhani tunapendana sana lakini baada ya honeymoon ndoa imekuwa maafa"


Tume Date kwa miezi sita na tulijiona duniani ni sisi tu kwa moto wa mapenzi/mahaba, lakini baada ya kuoana nyumba yetu imekuwa uwanja wa vita kwa kutokuelewana, Why?


Hili swali na mengine mengi yanayofanana na hilo huulizwa na maelfu ya watu ambao wameoa haijalishi mmeishi miaka mingapi, na wengine wamepeana talaka na kuoa na kuolewa mara nyingi zaidi na bado maswali kama hayo yapo.

Wengine wamewauliza wazazi wao, viongozi wao wa dini na pia washauri wao, lakini wakirudi nyumbani baada ya kupewa ushauri na majibu bado hali ni ile ile ni kama vile kutibu cancer kwa kutumia Asprini.

Inakuwa raha sana kabla ya kuoana/uchumba na baada ya kuoana hali inakuwa tofauti kabisa na wengine wanajuta kwa nini waliolewa na kuoa.

Pamoja na kuwa na TV, radio, magazeti, vitabu vyenye topic nzuri za kuimarisha ndoa zetu na semina mbali mbali, lakini bado mapenzi baada ya ndoa yanazidi kuwa kitendawili.

Ni ndoa chache kwa sasa ambazo zimebarikiwa kufahamu siri hii kubwa ya mapenzi baada ya kuoana na kutokana na kufahamu siri hiyo hao wanandoa wanaweza kukuthibitishia kwamba hakuna kitu kizuri duniani kama kuwa na mke au mume. Ndoa ni tamu, ndoa ni mpango wa Mungu kumkamilisha binadamu, ndoa ni msingi wa familia na taifa.

JE,SIRI NI NINI?

Tuanze kwa kuangalia msingi kabisa wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi hatua kwa hatua na leo napenda kukuletea utangulizi wakati tunaelekea kuchambua hili suala.


Mapenzi yana lugha kama zilivyo lugha za kawaida yaani Kiswahili, Kingereza au Kichina. Wengi tumezaliwa tunaongea lugha tulizafundishwa na wazazi wetu au ndugu zetu na kutokana na kuzifahamu vizuri zimekuwa lugha mama yaani Primary. Tunajisikia raha kutumia hizo lugha na pia tunajisikia raha kusikia kwani tunaelewa kuliko lugha zingine.


Katika mapenzi kuna lugha pia (emotional love languages) kwa hiyo mwanaume anaweza kuwa ana lugha yake na mwanamke ana lugha yake katika kuitikia mapenzi au kujisikia kwamba anapendwa. Kutokujua lugha ya mwenzake ni sawa na watu wawili (wanandoa) kuishi pamoja na kuwasiliana kwa kutumia kichina na kiswahili na kudhani wataelewana. Haitawezekana kamwe!

Hujasikia mwanaume analalamika kwamba "Mke wangu nimepa kila kitu, nimemjengea nyumba nzuri, nimemnunulia gari zuri, fedha za matumizi nampa nk, lakini analalamika kwamba simpendi, hiyo ni kudhihirisha kwamba huyo mwanaume kwa kumpa nyumba nzuri na gari zuri mke wake kwake ni lugha ya kuonesha anampenda mwanamke, wakati mwanamke kupewa gari na nyumba kwake bado si kupendwa yawezekana kusikilizwa na kuwa na muda pamoja (quality time) kwani ni lugha inayoeleweka kuonesha anapendwa.

...Je,lugha hizo ni zipi na zinafanyika vipi??


ITAENDELEA.....

No comments:

Post a Comment