Sunday 24 January 2016

PESA NA NDOA.

Hakuna mtu ambaye huwa anaingia kwenye Ndoa huku anajua hiyo ndoa Haitafika mbali.

Jinsi Unavyokuwa na Ufahamu mkubwa wa nini kinaweza kutokea baada ya kuoana hiyo itakuwezesha Kuzuia na Kujiandaa kukabiliana na changamoto zitakazotokea mbele ya safari ya Ndoa.
Matatizo yanayohusiana na pesa yamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ndoa nyingi. Matatizo haya huhusika moja kwa moja na jinsi ya kusimiamia na uaminifu katika pesa.
Kama hujaoa/olewa bado unaweza kukaa partner wako mkaongea masuala ya pesa na pia ukapata ufahamu wake kuhusu suala zima la pesa ili mkiingia kwenye ndoa unajua kabisa mwenzangu ni mtu wa aina gani lipokuja suala la pesa na uchumi kwa ujumla.
Na kama upo kwenye ndoa naamini umemchunguza mwenzako na kujua ana tabia ipi likja suala la pesa.
Hapa chini kuna maswali ambayo kama mwongozo tu hasa pale ynapojibiwa kwa ukweli na uaminifu ambayo inaweza kukusaidia kujua mtazamo wa mwenzako kuhusu pesa.

1. Wakati unafanya shopping huwa unafikiria kitu gani hasa?
(a) Vitu unavyonunua.
(b) Pesa unayotumia kununua hivyo vitu

2. Ikitokea mwisho wa mwezi ukapungukiwa pesa hata kama una mahitaji muhimu?
(a) Nafikiria Kukopa
(b) Sinunue kitu chochote

3. Huna Fedha (cash) na unataka kununua vitu na upo mbali na Bank yako utatoa uamuzi gani?
a) Nitatumia ATM card niliyonayo kwenye ATM machine iliyojirani
b) Sitanunua kitu kwani sipendi kutumia ATM card kwani kuna gharama za kutumia kadi

4. Huwa unajisikia una uwezo kifedha pale ikiwa?
(a) Una nunua kile kitu umekuwa unahitaji.
(b) Unapoiweka fedha kama mali (save).

5. Kwa jinsi unvyowekeza sasa na kuweka akiba.
(a) Hujui kabisa ni kiasi gani utakuwa nacho siku ukistaafu kazi.
(b) Unajua kiwango halisi cha pesa utakuwa nayo utakapostaafu kazi.

6. Unapoweka pesa bank kwa ajili ya akiba.
(a) Unajisikia ni wajibu (inaumiza kidogo)
(b) Unajisikia ni raha sana

7. Ukiwa na rafiki zako, unapoongelea masuala ya pesa huwa hukosi kutaja kipi ?
(a) Punguzo la bei uliyopata
(b) Punguzo la mali uliyonunua

8. Kama umepandishwa cheo utasherehekea vipi?
(a) Kwa kununua kitu maalumu kwa ajili yako mwenyewe
(b) Utaruka hewani na kushangilia “waoooooo”

Kama Amejibu kwa kuchagua (a) nyingi basi ni Mtumiaji mzuri wa pesa na kama amejibu kwa kuchagua (b) nyingi basi ni mweka akiba mzuri

Kama kuna tofauti kubwa yaani mmoja ni mtumiaji na mwingine anapenda kuweka akiba basi uwezekano wa kuwa na migogoro inayotokana na fedha ni kubwa, lakini haina maana kwamba itakuwa migogoro bali changamoto kamili inayokukabili mbele ya safari na unabidi ujiweke sawa jinsi ya kushughulikia Tatizo la pesa ndani ya ndoa.

Na kama partners wote ni Watumiaji; maana yake hakuna atakayekuwa na break ya kuzuia matumizi na matokeo yake mwisho wa njia kunakuwa zogo na matatizo ya fedha kwani mnatumia bila kuwake akiba.
Madeni huumiza ndoa, uwe mwangalifu.
Na kama wote ni watu wa kuweka akiba; hiyo ni nzuri ila mnahitaji wakati mwingine kufurahi kwa kutumia pesa kwa ajili ya just for fun.
Maana mnaweza kujikuta ni mabahiri wa ajabu kiasi kwamba hata raha ya kutumia pesa hakuna.
Kitu cha msingi ni kuhakikisha kila mmoja anamsoma mwenzake kujua mwenzake ana mtazamo gani kuhusu suala la pesa.
na pia kujua ni jinsi gani mnaweza kuhakikisha mnafurahia maisha ya sasa na wakati huo huo mnawekeza fedha na miradi ambayo mbele ya safari mtakuwa na fedha kwa ajili ya kusomesha watoto na hata wakati mkiwa wazee.
Wakati ni sasa usisubiri ukiwa mzee ndo unapanga mipango mikubwa ya kuwekeza anza hata kabla hujaoa au kuolewa.
Kama umeolewa au umeoa; panga malengo, timiza ndoto zako.
Kuwa na ndoa imara yenye afya ni pamoja na kuwa na mafanikio katika Creation of Wealth kwa ajili ya maisha yenu miaka 5, 10, 20, 50 au 100 ijayo.

No comments:

Post a Comment