Friday 15 January 2016

AJISIKIE VIZURI KWANZA.

Kuna tofauti kubwa sana ya maana na mwitikio wa mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.
Wanaume kawaida wanauwezo wa kutenganisha mwili na moyo.

Kwa upande wa wanawake tunaweza kusema wao wamekomaa kimapenzi kuliko wanaume kwa sababu kwao kutenganisha mwili na moyo inakuwa vigumu na wakati mwingine haiwezekani.
Mwanamke anapompenda mwanaume huanza na hisia za ndani za moyo wake kisha hisia za nje za mwili wake;
wakati mwanaume anapompenda mwanamke huanza kupenda kuanzia hisia za nje za mwilini mwake kisha hisia za ndani za moyo wake.

Ni rahisi mwanaume kukwambia anakupenda kumbe hakupendi bali anakutamani tu na wanawake wamekuwa wanaumizwa sana na wanaume kutokana na hii style yao ya kupenda kwa kumuweka mtu moja kwa moja kwenye moyo wake.

Utafiti mwingi unaonesha kwamba wanawake wengi huwa hawafurahii kufanya mapenzi na mwanaume asiyempenda;
wakati wanaume wanaweza kufurahia na kupata raha ya mapenzi (kufika kileleni) hata kwa mwanamke asiyempenda.
Ndiyo maana mwanaume anaweza kutembea na mwanamke yeyote hata kama ni mbaya kila idara ukilinganisha na mke wake.
Ndiyo maana matukio mengi ya ubakaji hufanywa na wanaume.
Ndiyo maana nyumba ndogo nyingi (wanawake) si wazuri kama nyumba kubwa (wake zao halisi)

Wanaume wanaweza kutenganisha upendo na kufanya mapenzi (love and sex).
Wanawake hutazama kufanya sex ni kitendo cha ziada baada ya upendo wa kweli na wakati mwingine hufanya mapenzi ili kuimarisha mapenzi kwa mwanaume, wakati wanaume sex ni kwa ajili ya kufurahia tu siyo lazima awe anampenda mwanamke anataka kufanya naye sex.

Kwa mwanaume kufanya sex ni kitu kinachofanywa nje ya mwili kwa sababu viungo vyake vya kufanyia vya sex vipo nje na anapofanya mapenzi anakuwa anafanya kitu kwa mtu mwingine (mwanamke) kama vile kupigilia msumari kwenye ukuta;

Kwa upande wa wanawake viungo vya sex vipo ndani ya mwili na kwao kufanya mapenzi ni kama kumkaribisha mtu ndani ya nafasi ya ndani yake, hivyo inakuwa ngumu kutenganisha mwili, moyo na hisia zake.

Kama ilivyo kwa watu wote kwamba mtu mgeni akiingia nyumbani kwako hutajisikia raha kwanza au hutajisikia salama hadi ufahamiane naye, ndivyo wanawake walivyo.Kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu au mgeni au asiyempenda ni sawa na mtu anayeingilia mipaka ya shamba lake,

Kumvamia mwanamke bila kuonesha upendo wa kweli ni sawa na kuvamia mipaka ya mashamba ya watu, au ni sawa na kuingia kwenye nyumba za watu bila kukaribishwa.
Wanawake hupenda kuwa na ukaribu na upendo wa kweli ili kumruhusu mwanaume kuwa naye kitandani na kuingia kwenye nafasi yake ya siri kufanya mapenzi.Ndiyo maana huwa wanajisikia kutumiwa na kuumizwa na mwanaume ambaye haoneshi upendo wa kweli.

Wanahitaji mwanaume anayewasililiza, anayewapenda, anayewajali, anayekuwa tayari wakati wanamuhitaji, mwanaume anayebembeleza, mwanaume ambaye anajua kuwahudumia wao kama viumbe rasmi na maalumu ambao Mungu ametoa zawadi kwa wanaume duniani.
Hii ndiyo sababu mwanamke hupenda kujisikia vizuri kwanza ili afanye mapenzi wakati mwanaume hujisikia vizuri baada ya kufanya mapenzi.

No comments:

Post a Comment