Thursday 10 March 2016

WENYE TABIA HII..

Kukefyakefyani nini?
Ni kitendo cha kutafuta makosa na kuendelea kulaumu, kulalamika, kusumbua, kutesa, kuchokoza , kuudhi, kushutumu, kuleta mzozo ndani ya wanandoa.
Mara nyingi wanawake ndiyo wenye hii tabia ingawa imegundulika kwamba wapo wanaume wenye tabia hii katika ndoa.

Pia kukefyakefya ni kitendo cha kumsumbua mwanaume kwa maswali, au kumtuma kitu au kumwambia afanye kitu kama vile ni bosi wa kihindi na mfanyakazi wake au mama na watoto wake wakati ni mke na mume ndani ya nyumba.

Inawezekana mume wako anatabia ya kuacha bathroom kuwa chafu baada ya kutumia, akila anaacha meza na vyombo ovyo na vichafu, Inawezekana huwa anatupa nguo ovyo na kusambaa sakafuni utadhani chumba cha watoto wa shule, Inawezekana anakaa tu huku anazidi kunenepeana kama wachezaji wa sumo, au anaangalia TV kama vile ana mkataba na vituo vya TV na umekuwa unamwambia kubadilika lakini habadiliki na umeona dawa nikuendelea kumsema.

Au umekuwa ni mwanamke mwenye maswali hata yasiyo na kichwa na miguu tangu asubuhi wewe ni kuuliza tu nakuendelea kuuliza.
"Unamuuliza, je Ulitoa zile takataka, ulilipa ile bill, umetengeneza lile dirisha, umemwambia fundi kuhusu tatizo la umeme hata hajajibu umeshampachika swali lingine"
Kawaida wanaume huwa hawapendi kuambiwa nini cha kufanya.

Kwa nini kukefyakefya si vizuri?
Kwa sababu husababisha mwanaume kukwazika, kwani hujiona yeye ni mtoto na mke ni mzazi au mama, Hakuna mwanaume anapenda mke wake kuwa kama mama yake mzazi.
Mwanaume hujisikia haheshimiwi na mkewe.

Mwanaume hujisikia kushambuliwa na kudharauliwa nakujiona hafai

Kwa nini wanawawake hupenda tabia ya kukefyakefya?
Wanaume hawafanyi vile wanawake wanawaambia wafanye.
Pia wanawake hudhani kwa kurudia kukumbushia na kusutana basi mwanaume atafanya.
Wapo wanawake wamekulia mazingira ambayo mama zao walikuwa ni watu wa kukefyakefya kwa baba zao hivyo basi nao wanaamini hiyo ndiyo njia pekee ambayo wanaume wanaweza kufanya yale wanasema au wanataka wafanye.
Wengine ni asili yao kufanya hivyo.

Nini matokea ya tabia ya kukefyakefya?

Mwanaume huanza kumkwepa mke wake na kuchelewa kurudi nyumbani au kujibakia ofisini au kazini au kupitia sehemu hadi ahakikishe akirudi nyumbani mke amelala.
Mwanaume anaweza kuanza tabia mbaya za ulevi au kukosa uaminifu katika ndoa
Mwanaume huanza tabia ya kutosikiliza mke wake kwani anamchuja (filter) kwamba huyu ni tabia yake kukefyakefya so msumbufu.
Kuchokana katika ndoa maana hakuna ukaribu (intimacy) pamoja na mawasiliano kuwa ovyo maana mume sasa uwa si msikilizaji mzuri.
Mwanaume hukosa hamu na huyo mwanamke mwenye hii tabia.

Je, mwanamke afanyeje asiwe na tabia ya kukefyakefya?

Kwanza mwanamke lazima akubali kwamba yeye na mume wake wapo tofauti na azikubali tofauti, akubali upungufu uliopo na kuchukua maisha kama yalivyo.
Siku mwanaume akifanya vizuri ampe appreciation.
Lazima mwanamke awe positive kama mwanaume amefanya alichoambiwa afanye kwa maana kwamba usilaumu, shutumu, au kukasirika au kumfanya aonekane stupid.
Kawaida Hakuna kitu kibaya duniani kinachofanya tuone kitu ni kibaya bali ni jinsi tunavyofikiri.
Shirikisha hisia zako kwake kama ungekuwa wewe kila siku unaambiwa kama mtoto mdogo ungejisikiaje.

Inawezekana mumeo huchelewa kurudi nyumbani au kukupa sababu eti anapitia sehemu kumbe anakwepa tabia yako ya kukefyakefya.


Ni afadhari kuishi pembe ya darini kuliko kukaa katika nyumba pana pamoja na mwanamke anayekefyakefya
(Mithali 19:9)

No comments:

Post a Comment