Thursday 10 March 2016

HUWAUMIZA SANA.

Je umemchoma mara ngapi mumeo au mchumba wako?
Ni ukweli usiopingika kwamba hata wanaume huumia sana hisia zao na mtu pekee mwenye uwezo wa kupooza maumivu ni mpenzi wake yaani mke au mchumba yake, Je inakuwaje pale inatokea mke au mchumba ndo anakuwa chanzo cha maumivu ya hisia za mwanaume?
Ni muhimu sana mwanamke (mke au mchumba) kuepuka haya;-

Kumwambia kwamba hana thamani yoyote na kwamba hana lolote na hakusaidii lolote. Hata kama unaongea ukiwa na hasira kumwambia mwanaume yeyote kwenye mahusiano kwamba hana maana unaweza ukajutia. Ni busara kama una hasira na unajiona huwa unakuwa huna break kwa maneno unaongea baki kimya.

Kumfananisha yeye na mwanaume mwingine ambaye amefanikiwa iwe pesa au maisha kwa ujumla. Usimwambie mumeo au mchumba wako kwamba mbona mke wa fulani au mchumba wa fulani amenunuliwa hiki au kile na yeye hawezi, hiyo ni kashfa. Atakwambia uende ukaolewe naye kama wewe ni mchumba na kama ni mke atakwambia nenda kaishi naye au unawasha moto ambao kuuzima unahitahi magari ya fire ambayo tena yanakuja bila maji.

Usimwoneshe kwamba husikilizi pale anaongea hasa anapoongelea jambo lolote analoliona ni la msingi. Hata kama kama anachoongelea unaona kwako ni upuuzi jitahidi kuonesha kama unamsikiliza ikiwezekana hata kuuliza maswali kutokana na anachoongea. Ukimsikiliza atajisikia wa maana na anaweza kuongea na wewe mambo mengi ya msingi.

Usifanye utani (hasa kwa kutumia wanaume wengine hasa utani unaomdhalilisha yeye) hata kama unatumia utani ukiongelea mwanaume ambaye ni rafiki yake. Maana akiumizwa hisia zake kumbuka kutibu ni gharama kubwa sana. Kwani kwa maneno wengine wamevunja ndoa na uchumba.

Kutoa sababu kila mara mumeo anapotaka kufanya mapenzi na wewe, hii ni pamoja na kuwa mwanamke mwenye huzuni mara zote, hakuna furaha wala kutabasamu kila wakati mwanamke ni malalamiko, huzuni na gubu, unafikiri kwa nini aliondoka kwa mama yake na baba yake kama si kukasirikiwa kila mara.
Amekuchagua wewe ili uwe faraja na akiwa na wewe anajisikia raha kama hivyo basi ni afadhari asirudi nyumbani au atumie muda wake na mtu mwingine usidhani eti kwa kukasirika au kuonesha uso wa huruma na huzuni ndipo mwanaume atakuona wa maana au kukuhitaji na kukubembeleza zaidi, ukweli anajiona hawezi kukupa furaha na hivyo afadhari awe na kitu kingine badala yako, who cares hata TV anaweza kuona inamfaa kama si kwenda kuangalia mechi za ligi kuu Uingereza.

No comments:

Post a Comment