Monday 14 March 2016

SEX WAKATI WA UJAUZITO.

Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili mambo yaende vizuri.

Je, Mwanamke mwenye mimba anaweza kuendelea na tendo la ndoa?

Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni.
Hata kama kunatokea miscarriage bado sayansi inathibitisha kwamba chanzo huwa si sababu ya tendo la ndoa wakati mwanamke ana mimba, bali sababu zingine kabisa.
Tafiti nyingi zimefanywa kwa kufuatilia wanawake ambao waliendelea na tendo la ndoa huku wakifika kileleni (orgasm) na wale ambao hawakuwa wanafika kileleni wakati wa tendo la ndoa, na wale ambao hawakufanya kabisa tendo la ndoa muda wote wa ujauzito.
Matokeo yalionesha kwamba wanawake wote walizaa watoto ambao hawana tofauti yoyote kiafya.
Hivyo tendo la ndoa ni salama kabisa muda wote wa ujauzito.

Je, ni wakati gani huruhusiwi tendo la ndoa wakati wa ujauzito?

Ni pale tu mwanamke anapojisikia kuwa na bleeding au maumivu yoyote au leakage ya majimaji yajulikanayo kitaalamu amniotic fluid.
Mwanamke mwenye mimba haruhusiwi kuingiza upepo (by forcing) kwenye uke wake kwani husababisha kitu kinaitwa Air bubble kitendo ambacho kinaweza kusababisha kifo kwa mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni kwani hu-block mishipa ya damu. Wapo wanaume huwa na mchezo wa kubusu huku wanapuliza huko bondeni kabla ya kuanza kusex.
Pia kama mmoja ya wanandoa ana magonjwa ya zinaa (STD) haruhusiwi tendo la ndoa hadi daktari athibitishe kwamba amepona ama sivyo anaweza kusababisha mtoto tumboni aambukizwe.

Pia ifahamike kwamba si wanawake wote wakiwa na mimba hupenda tendo la ndoa wengine huwa hawapendi kabisa.
Utafiti unaonesha pia kwamba mwanamke mwenye mimba hukosa hamu ya tendo la ndoa miezi mitatu (3) ya kwanza, kisha hupenda sana tendo la ndoa miezi mitatu inayofuata na Pia miezi mitatu ya mwisho hukosa tena hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya saikolojia ya kusubiri mtoto kuzaliwa.
Ingawa uzoefu unaonesha kwamba mwanamke mwenye mimba husisimka haraka na kufika kileleni mapema sana kwa sababu damu huwa nyingi sana kuzunguka uke na hivyo kuwa sensitive zaidi kuliko akiwa hana mimba, pia ni dhahiri kwamba mwanamke anayefurahia tendo la ndoa wakati ana mimba hupata utamu wa uhakika.

Kitu cha msingi pia ni kuzingatia mikao au milalo wakati wa tendo la ndoa kwani mwanamke mwenye mimba anahitaji mikao au milalo ambayo haikandamizi tumbo lake.
Hakikisha mnakuwa na communication nzuri kuhusiana na suala la tendo la ndoa ili kila mmoja aweze kuwa msaada kwa mwenzake.

No comments:

Post a Comment