Tuesday 1 March 2016

UPENDO HUWA HIVI..

Mara ya kwanza ulipopendana na mume wako au mke wako au mchumba wako, kuwaza kuhusu yeye kulikuja kwenyewe automatically.
Ulitumia masaa mengi sana kumuwaza namna anavyoonekana, ukijiuliza atakuwa anafanya nini katika muda fulani, ulikuwa unarudirudia kuwaza na kujiuliza vitu vizuri ambavyo ungemwambia au kuongea naye wakati mkiwa wote, ulimtumia emails nzuri zenye maneno matamu, ulimtumia sms mara kwa mara kuonesha ulikuwa unamuwaza, uliandika hata barua nzuri kuonesha hisia zako na kwamba ulikuwa unamuwaza, ulihangaika kutafuta maneno matamu ambayo akiyasikia anafahamu kwamba zaidi ya kumpenda ulikuwa unamuwaza.
Na hata usiku ulimuota (ndiyo maana ulikuwa unamwambia usiku hukulala) yeye kwa sababu ulikuwa unamuwaza kuliko kitu chochote.
Ikafika Mahali ukakiri kwamba;
“Siwezi kuacha kukuwaza wewe!”
Hata hivyo kwa baadhi ya wapendanao (inawezekana hata wewe unayesoma hapa ndicho kinachoendelea katika ndoa yako) baada ya kuoana mambo huanza kubadilika kwani mwanamke sasa amempata mwanaume aliyekuwa anamuhitaji; na mume ameshapata trophy ambayo alikuwa anaiwinda miaka yote, sasa kazi ya kuwinda amemaliza, mission accomplished, job done, malengo yametimia.
Miali ya ukaribu wa kimapenzi inaanza kuwaka kwa udhaifu mkubwa na kilichokuwa kinasukuma kumuwaza sasa kinapoa, sasa unaweka malengo katika kazi na taaluma yako au marafiki, au mambo unayoyapenda wewe binafsi na baada ya muda unaanza kuacha kutimiza mahitaji ya mke wako au mume wako.
Hata hivyo bado ukweli unabaki palepale kwamba ndoa imemuongeza mtu maalumu katika maisha yako na hii haitabadilika na kama uwezo wako wa kufikiri unashindwa kumweka mtu aliyeongezeka katika mawazo yako ili kumpa nafasi basi unakoelekea ni hatari.
Kama hujifunzi kumfikiria/kumuwaza mke wako au mume wako basi unaweza kuishia pabaya, inaweza kufika birthday yake usijue, inaweza kufika anniversary ya ndoa yenu na usikumbuke na ukalaumiwa kwamba humfikirii yeye bali wewe mwenyewe.
Utakosa opportunities nzuri za kuweza kuonesha upendo wako kwake.
Kuonekana huna wazo lolote kuhusu mke wako au mume wako ni adui mkubwa wa kudumisha moto wa ukaribu wa kimapenzi katika ndoa.
Mwanamke siku zote ana hamu ya kufahamu namna mume wako anavyomuwaza na hii humfanya kujisikia anapendwa.
Je, ni mara ngapi au ni muda kiasi gani umekuwa kuitumia kuwaza namna unaelewa na zaidi unavyoweza kuonesha upendo kwa mume wako au mke wako?
Je, ni tukio gani (birthday, anniversary, holiday) ambalo sasa unaandaa ili kuonesha unamuwaza na unamkumbuka?
“Great marriages come from great thinking”

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment