Thursday 10 March 2016

ANAHITAJI MUDA WA KUPUMZIKA KWANZA.

Wanaume hupenda kuwa wenyewe muda fulani hasa akiwa amerudi nyumbani kutoka kazini au akiwa anatatizika na jambo lolote.
Hivyo basi inawezekana wewe kama mwanamke ndani ya ndoa umezoea mume akirudi kutoka kazini unamkaribisha home kwa kumpiga maswali na kuanza kumueleza kila aina ya matatizo na karaha ambazo zimetokea siku hiyo bila kumpa hata muda wa yeye kupumzika kidogo.

Sina maana kwamba mumeo akirudi nyumbani ule jiwe bila kumpokea au kumuuliza kazi ilikuwaje, nazungumzia suala la kutompa muda angalau dakika 15 kupumzika kabla hujaanza kutoa maswali yako na matatizo yako.

Pia naamini dunia ya sasa wote wanawake na wanaume tunafanya kazi iwe ofisini au shambani hata hivyo tukifika nyumbani kila mmoja hujitahidi kumweleza mwenzake nini kimeendelea au kupeana taarifa mbalimbali za familia ukweli ni kwamba bado mwanaume huhitaji dakika kama 15 kabla ya kujiunga na familia.

Kumbana maswali na kumwambia matatizo na shida tangu anaingia mlangoni si jambo zuri sana kwa mwanaume kwani hujisikia anaishi na mama yake na si mke wake maana mama yake alizoea kumbana maswali tangu anaingia nyumbani kutoka shule.
Kama angekuwa anataka kuishi na mama yake basi asingekuoa wewe bali amekuoa wewe kwa sababu wewe ni tofauti na mama yake.

Baada ya kuchoshwa na kazi, na boss, au wateja au foleni za magari njiani anapowahi nyumbani anachohitaji akifika nyumbani ni busu na hugs kutoka kwa mke wake then aoge na kupumzika kidogo kama dakika 15 hivi ndipo atakuwa tayari kujibu maswali ya mkewe na kuendelea na story zingine pia.

Mpe muda wa kurelax akishafika nyumbani kwani kumbana maswali punde tu anaingia nyumbani kunaweza kusababisha yeye kuchelewa home kwani hujisikia ni usumbufu.
Akishakuwa tayari ameridhikana muda wake kuwa kwenye hilo cave unaweza kuona anaanza kuzungumza mwenyewe then anza kumpa hayo maswali yako.
Pia akigundua wewe ni msumbufu, hata siku ukiwa na point za maana anaweza kupuuzia maana umezoea kuchonga sana akiingia tu mlangoni hata kabla hajafika chumbani.

No comments:

Post a Comment