Saturday 2 April 2016

KUPATA MCHUMBA SAHIHI...2

Haijalishi mtu unayetaka kuoana mmekutana wapi;
hata kama ni kanisani, shuleni, kwenye mkesha wa maombi, kijijini, mjini, hotelini, sokoni, kwenye daladala, barabarani, ofisini, kazini, safarini, kwenye semina au hata kama ni kwenye internet au njia yoyote ile ambayo Mungu anaweza kuitumia maana Mungu hafungwi na njia za kukutanisha watu.
Au Haijalishi ni mzungu, mwarabu, mchina, mwafrika, au awe mnene, mwembamba, mrefu kama Ngongoti, mfupi kama Zakayo,
Awe amesoma au hajasoma, awe mbena au mchaga au mhaya au mgogo au mzigua, au awe anatoka Canada, Kenya, Uganda, Nigeria au Tanzania. Pia haijalisha ktk kukutana naye umeunganishiwa na rafiki yako, au mchungaji wako, au wazazi wako au mtu wako wa karibu.
Kitu cha msingi ni wewe kuwa makini kujiuliza haya maswali matano muhimu.


1. JE, TUNAFANANA?

Ndoa ni kama jengo la nyumba na nyumba ni sharti iwe na msingi. Msingi imara huwezesha nyumba kuhimili kila aina ya janga linalotokea kama vile mvua, upepo, mafuriko, dhoruba, tetemeko la ardhi nk. Na kuna aina ya material zinazotumika kujengea msingi na hizi aina za material ndizo huelezea aina ya msingi na uimara wake.

Unaweza kujenga ndoa kwa kuvutiwa na umbo la mtu (mvuto wa nje) au urembo tu. Pia sasa hivi kuna uzuri mwingi tu na unauzwa dukani (body shops)
Unavutiwa na kipande kimoja tu cha mwili wake kama vile shingo, matiti, matako, unene, au wembamba, nywele, smile, anavyotembea, miguu, au kifua nk.
this is just physical attraction kuna siku anaweza kubadilika kuna kuugua, kuna ajali, kuna kubadilika mwili nk kwa hiyo ku-base kwenye mwonekano wa nje peke yake lisiwe jibu kwako kuona huyu mtu ananifaa.
Hapo utakuwa umejenga msingi wa nyumba kwa kutumia mabua au miti hakika nyumba ikishika moto hata majivu tunaweza tusipate.

Ndoa hujengwa ktk misingi 3 muhimu ambayo lazima mfanane au kuwa kitu kimoja. Ni muhimu kusiwe na gap kubwa sana katika mambo haya matatu,
Nayo ni Kimwili,
Kiakili na
Kiroho
(Mind, Body and Soul).
Mara ya kwanza mnapokutana wote mmoja anapata kuvutwa na mwingine kwa njia ya tofauti na huko kuvutwa kuna base kwenye mwonekano wa tabia kama vile anavyoongea, anavyotabasamu, anavyopenda na kwa hayo tu huwezi kusema biashara imeisha ananipenda au nimempenda na kukubaliana kuoana.

Unapotumia muda zaidi kuwa naye na kumjua zaidi, uhusiano unakua na unamfahamu zaidi ya ile physical attraction ambayo uliipata kwa mara ya kwanza sasa unaweza kutambua mambo anayopenda,
mawazo yake katika mambo mbalimbali ya kiroho,
kimwili na kiakili,
unaweza kujua talents zake na hobbies zake
hapa ndo inabidi uwe makini kufanya assessment kwani hapo ndo biashara yenyewe kwani ukimpenda na ku fall in love unakuwa blind halafu utaona kila kitu shwari hata watu wakikwambia kuna tatizo utakataa na kuwambia yupo sawa kabisa na bila yeye wewe maisha hayana maana, kumbuka huyo ni mchumba si mke/mume.
Unahitaji kuwa mchunguzi zaidi kuliko kupendwa. Kumbuka hapa unatafuta mchumba hajawa mke so ukiona kuna dalili au tabia ambayo ni hatari inabidi uwe makini.

Upendo wa kweli hauwezi kuwepo bila bonding ya kiroho.
Kutofautiana kiroho na kiimani ni moja ya sababu ya ndoa kuvurugika na hatimaye kuvunjika. Hivyo ni vizuri kupata data kamili kwa kuthibitisha imani yako na yake.

2. JE, UNAKUBALIANA NAYE KTK MAMBO YAKE?
Mtu ambaye kwake pesa na kazi ni namba moja yaani ni kitu cha kwanza, kwake bila hivyo hakuna maisha, yaani muda wake na akili yake ni pesa na kazi kwanza,
Then mambo ya michezo kama soka, au kushabikia tu michezo ni kitu cha pili, familia (mke au mume na watoto) ni kitu cha tatu kwake,
Na mwisho Mungu, yaani Mungu ni kitu cha ziada kwake, akiwa hana cha kufanya ndo anakumbuka mambo ya Mungu, Kama wewe ni dada ukapata kijana wa kiume wa aina hii kuendelea naye fikiria mara mbili.

Au mwanamke ambaye kwake kujiremba, kujisifia au kusifiwa na kuhudhuria sherehe (mama wa shughuli) kwake namba moja, then familia na Mungu baadae.
Kama ni kijana wa kiume binti wa aina hii fikiria mara mbili kabla hujaamua.

Kama ninyi ni Christians kitu cha kwanza ni kila mmoja kuwa na uhusiano na Mungu wake kwanza then familia yaani mke/mume na mtoto then kazi hii ni pamoja na kazi ya Mungu.
Hivi unaweza kwenda kuimba kwaya wakati mke au mume yupo kitandani anaumwa na hakuna mtu mwingine? Mlio kwenye ndoa tusaidie hapo!.....

ITAENDELEA....

No comments:

Post a Comment