Saturday 16 April 2016

KUHUSU NDOA..

Tafiti nyingi zinafanana na zinakubali kwamba ndoa nyingi imara ni zile ambazo mke na mume huwa na sifa nyingi zinazofanana.
Kundi la watafiti lilikusanya ndoa 35 ambazo ziliwekwa katika makundi matatu kundi la kwanza lilikuwa la wale ambao ndoa zako zilikuwa za furaha, kundi la pili zile zilikuwa ni zile wanandoa walikuwa na wakati mgumu kuishi pamoja na kundi la tatu la wale walikuwa njiani kuachana.

Majibu yalikuwa ni kwamba wale walioishi kwa furaha walifanana sana katika mambo mengi (general activities), walikuwa marafiki na walifanana katika kujihusisha binafsi na mwenzake.
Wale ambao hawakuwa na furaha kuishi pamoja hawakufanana katika utendaji wa mambo yao kila siku, pia hawakufanana linapokuja suala la mwitikio wa hisia zao.
Wale waliokuwa wanataka kuachana kila mmoja alikuwa na sifa nyingi zisizofanana kabisa.

Kiwango cha furaha katika ndoa huweza kujieleza kutokana na kufanana kwa wanandoa katika sifa binafsi walizonazo.
Hii ina maana wanandoa wakifanana kiuchumi, tabia, mazingira, tamaduni, matumizi ya pesa, kiwango cha energy, uwezo wa kuongea na kusikiliza, kiimani, kihisia nk inakuwa rahisi kila mmoja kutegemea nini kutoka kwa mwenzake.

Hivyo ukitaka kuwa na ndoa imara ni muhimu kuwa na balance account ambayo kufanana ni zaidi ya tofauti kwa sababu kila tofauti iliyopo inahitaji kupatanisha na kuweka kuikubali hata kwa maumivu.

No comments:

Post a Comment