Thursday 11 February 2016

NDOA NI MFANO WA MBIO NDEFU.

Ndoa inafanana sana na ukimbiaji wa mbio ndefu (marathon) na hutoa matokeo mazuri sana pale wanandoa wanapofahamu kwamba mbio za ndoa yao si mbio fupi.
Sababu kubwa inayofanya wakimbiaji wa mbio fupi kushindwa kukimbia mbio ndefu ni kwa sababu akili zao wameziweka au zimezoeshwa kukimbia mbio fupi tu na si zaidi ya hapo.
Mawazo yao kichwani ni mita 100 tu na kuwaambia wakimbie mita 1000 husababisha kushindwa hata kabla hawajakimbia kwa sababu ya mindset zao na mazoezi na malengo ya taaluma zao.
Hatujawahi kusikia mkimbiaji maarufu wa mbio fupi (ameweza kupata medali ya mbio ndefu, ni vigumu mno.

Kwa nini ndoa nyingi huishia njiani?
Ndoa nyigi (si zote) huishia njiani kwa sababu wanandoa huanza safari ya ndoa kwa kuwa wakimbiaji wa mbio fupi badala ya mbio ndefu yaani marathon.
Hujawa na mawazo ya furaha muda mfupi badala ya kuangalia mbali zaidi miaka 100 ijayo.
Akiumizwa kidogo au kukutana na tatizo kubwa au shida nzito au jaribu kubwa hujiona kama hastahili kuumizwa na pia kama mwenzake anampenda basi amisha ya ndoa ni raha na mstarehe.

Mkimbiaji mzuri wa marathon hawezi kuacha kukimbia akipata maamivu kwenye miguu, au kuchoka au kushikwa na misuli au kukumbana na hali mbaya ya hewa jua kali au baridi kali huwa hakati tamaa huendelea kukimbia huku akivumilia kwani lengo ni kuhakikisha anamaliza hadi mwisho.

Wanandoa wengi huamini kwamba kama umempenda mtu basi ndoa itakuwa rahisi na mteremko kama nyikani kwenye mawindo, waulize wanandoa wote ambao wamekaa kwenye ndoa zaidi ya miaka 10 acha miaka 50, wote watakwambia walipitia hatua zote za kukutana na matuta, siku za giza nene, siku ambazo hujisikia kama mume au mke hafai tena kwa kuwa lengo ni mbio ndefu ndoa zao bado zina Baraka hadi leo.

Usiwe mkimbiaji wa mbio fupi, anza kujizoeza kuwa mkimbiaji wa mbio ndefu za ndoa yako.
Wakati unakimbia marathon kuumia au maumivu ni kitu cha asili hakikwepeki kilichopo ni kupambana tu.
Bila kuwa na maumivu huwezi kumaliza marathon na bila kumaliza marathon huwezi pewa medali.

Kuachana na kumkimbia mwenzako si jibu kwani hata ukae mwenyewe bado utakutana na shida acha zile za upweke na Ukisema utafute mwanaume/mwanamke mwingine huyo ndo atakupa shida mpya kabisa ambazo zitakupeleka ground zero tena.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment