Wednesday 10 February 2016

JE,NDOA INAKUCHANGANYA

Je, unapita katika ndoa ngumu hata unawaza sijui kesho itakuwaje?
Kila siku ikipita unaona afadhari ya jana kwa kwani ndoa ni ngumu, ipo ovyo, kupigana kila wakati, kitu kidogo basi mzozo mkubwa huzaliwa, nyumba ni moto, ni kudharauliana tu na visa kila iitwapo leo?

Kwa tabia mbaya alizonazo partner wako unajilaumu hata kwa nini ulichukua uamuzi wa kuoana naye.
Kila ukimtazama sasa hana mvuto kabisa, amechuja, ni mbaya na havutii, hapendezi tena na anakutia kichefuhcefu unatamani mlale vyumba tofauti au asafiri miaka isiyojulikana.

Unaanza kufikiria kuachana ndiyo njia rahisi na kwamba ni permanent solution.
Wakati huohuo mawazo yako na akili yako na moyo wako na nguvu zako zote umeelekeza nje, kwa partner mwingine ambaye unaamini kwa moyo wako kwamba ni mzuri, mtamu, yupo single, independent, loving, romantic, caring na ukiwa na yeye basi maisha yatakuwa matamu zaidi.

Hata umeamua kubadilisha marafiki ili kukubaliana na nafsi yako kwamba ukiwa na hao marafiki wapya ambao ni single na wenye tabia mpya kama yako basi dunia itakupa kile unahitaji.

Ukweli ni kwamba mambo si rahisi kama unavyofikiria.
Pia ni kweli mawazo kama haya (mawazo ya kujenga nyumba kwa mabua) huwapata wengi sana kwenye ndoa zetu.
Hebu vuta pumzi, pumua upya na jikusanye na kuanza kufikiria upya hata kama ndoa unaona haina ladha, imekuwa upside down, umeshindikana na haina mwelekeo ukweli bado unaweza kuirudisha kwenye siku zake za honeymoon.

Wakati unaendelea kufikiria jinsi utakavyokuwa unajirusha na partner wako mpya katika viwanja mbalimbali, please fikiria kwanza watoto wenu (mtoto), pata picha jinsi utakavyowaambia watoto kwamba wewe na mwenzako mmeachana na wao sasa wanaishi na mzazi mmoja.
Fikiria jinsi ya kugawana picha zilizomo kwenye Album yenu ya harusi, Fikiria mtakavyoanza kugawana mali.
Fikiria utasema nini kwa Mungu maana uliahidi mbele zake na mbele za wandamu kwamba utaishi na hii ndoa hadi kifo kitakapowatenganisha.
Fikiria familia, ndugu, marafiki nk
Na cheti cha ndoa je, rings je?

Je, bado unamawazo ya kuachana naye?
Una uhakika hakuna mambo mazuri kwake kuliko mambo mabaya?
Usije kuwa unataka kubadilisha seat kwenye meli ya MV Bukoba ukaishia kuzama ziwa Victoria.

Naamini unadhani kwa sura aliyonayo huyo partner 2 basi hutapata matatizo au migogoro yoyote.
Ukweli ni kwamba hata ukipata partner mpya kinachobadilika ni sura tu matatizo ni yaleyale kwani wote ni binadamu na ndoa imara si kukimbia matatizo bali kukabiliana nayo na kujifunza na kuendelea mbele.
Je, umeshaomba ushauri kwa kiongozi wako wa dini naye akashindwa? washauri wa mambo ya ndoa nao wakashindwa?

Tafiti zinaonesha wengi walioamua kuachana na kuanza ndoa mpya baada ya muda hukutana na matatizo makubwa zaidi na magumu zaidi kuliko yale ya kwanza na hutamani kama wangerudi kwenye ndoa zao za kwanza.

Kitakachokusaidia ni kubadilisha mtazamo siyo kubadilisha ndoa na ukweli ni kwamba ni rahisi kubaki kwenye ndoa kuliko kuanza ndoa mpya.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment