Thursday 11 February 2016

MFANYE MWENZIO KUWA NAMBA 1

Kila mmoja anapoacha baba na mama na kuanza maisha mapya na yule amempendaye, basi huwa amefanya uamuzi ambao ni wa maana na busara sana.
Mambo huwa ovyo sana, na huwa inakatisha tamaa sana unapoona mtu ambaye ulichukua uamuzi wa kuishi naye maisha yako yote anabadilika na kuweka vitu vingine kuwa namba moja badala yako.

Mwanaume au mwanamke anapoweka kitu kingine kuwa msingi kwake, kitu cha maana kwake, namba moja kwake na kutumia muda wote na uwezo wake wote kwa ajili ya hicho na mke au mume kuwa kitu cha pili yaani namba mbili.
Bila kumuweka mwenzi wako kuwa namba moja ujue hakuna kitu unaweza kununulia kwa pesa hapa duniani kikamridhisha na kuona unamjali na kumsikiliza.
Kwani hujasikia wanawake wengi ambao waume zao ni watu maarufu na wenye pesa wanalalamika kwamba bado hawahitaji pesa au vitu, wanachohitaji kupata muda na kupewa nafasi ya kwua pamoja, kusikilizwa na kujiona wanaume wanawajali.

Wapo wanaume ambao business ndo kimekuwa kitu cha kwanza kwake na mke anakuwa ziada na hata hudiriki kutoa pesa au vitu ili mke aridhike na kuona anamjali. Hii haina maana usifanye business ila lazima mke apewe muda wa pamoja na wewe na yeye kuwa muhimu.
Wapo ambao utadhani walizaliwa na TV na akiwa na TV mke au mume si lolote, TV anakuwa mke au mume.

Wengine hujikuta wanahangaika na kazi za kanisa (kazi za kanisa zingine si kazi za Mungu) fahamu ukristo wa kweli ni ule kanisa kuanzia nyumbani kwa mke na mume kuwa na amani ya kweli na maisha ya upendo kwa kutanguliza na kumjali mwenzako.
Wengi kazi za ofisini ndo zimekuwa mume au mke, Kumbuka kazi zipo ulizikuta na utaziacha mume au mke ni namba moja.

Wengine watoto ndo wamekuwa wa maana kuliko mume au mke nao pia wamewakuta na watawaacha wenyewe na maisha yenu, watoto wanahitaji upendo lakini isiwe wao wakasababisha mke au mume awe wa mwisho katika kusikilizwa.

Bila mume na mke kila mmoja kumpa nafasi ya kwanza mwenzake basi itakuwa ngumu sana kuwa na ndoa bora kama Mungu alivyopanga.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment