Friday 12 February 2016

MWANAMKE MLALAMISHI.

Binadamu ni kuimbe anayependa sana kulalamika iwe ofisini, kanisani, hotelini, kazini, sokoni, darasani, mikutanoni, msibani, harusini nk watu ni kulalamika tu.

Na kwa upande wa wanandoa mwanamke ndiye anajulikana sana kwa kuwa mtu wa kulalamika kiasi kwamba wanaume wengi huwa wanachoka na kuanza kujiuliza hivi mwanamke anahitaji kitu gani maana kila unachompa bado hakiwezi kumfanya asilalamike zaidi.

Je, ni tabia ipi huchukiza wanaume?

Ukiwauliza wanaume wengi kwenye ndoa asilimia kubwa watasema hawapendi kabisa tabia ya mwanamke kulalamika kwa kila kitu na wakati wote.

Kwa nini wanaume hawapendi mwanamke mlalamishi/mnung’unikaji?

Wanaume tangu utoto wao wamefundishwa kuwa tough, kuwa wavumilivu, kuwa unemotional, kuwa wanaume na zaidi kwamba tabia ya kulalamika si ya wanaume.
Matokeo yake wamekuwa watu dhaifu sana linapokuja suala la mtu mlalamikaji na hushindwa kuvumilia kuona mtu analalamika mnuda wote.

Wanaume pia ni watu wa ku-fix matatizo au kutoa solution na si kutafuta solution.
Mwanamke anapolalamika kwa mara ya kwanza humvuta mwanaume kuja kutatua tatizo na akiendelea kulalamika mwanaume hujisikia ameshindwa ku-fix hilo tatizo na hujiona failure mkubwa.
Kulalamika si njia njema ya kuuliza au kupata kitu kwa mwanaume bali ni njia bora ya kumfanya ajisikie vibaya.

Mwanamke mlalamishi ndani ya nyumba kwa mumewe muda wote hufanya mwanaume amuone ni takataka zaidi na kwamba hawezi kukufanya uwe happy na mwanamke usipokuwa happy maana yake mwanaume ameshindwa kazi ya msingi kabisa katika mahusiano.
Anajiona ni sawa na mwindaji anayerudi mikono mitupu nyumbani baada ya siku nzima ya kuwinda.

Wanawake wengi hutegemea sana mwanaume kuwa source ya furaha zao, huo ni mzigo mzito sana ambao mwanaume anaweza kuubeba.
Pia mwanamke unawajibika kabisa kujipa furaha mwenyewe kwanza, unapochukua jukumu la wewe mwenyewe kuwa mwanamke mwenye furaha na mumeo hujiona amefanikiwa sana hata kama hakufanya lolote kwa furaha uliyonayo na zaidi unapokuwa na furaha unaruhusu moyo wa mumeo kufunguka kirahisi kwako kuliko kuwa mwanamke mwenye uso usio na furaha kama vile ulilazimishwa kuolewa naye.

Pia kulalamika kunafanya mwanamke usiwe attractive, mwanamke unapolalamika kwa kila kitu na kila wakati mwanaume hukuona upo ugly na huvutii kabisa ndo maana wanaume wengi wanawatoroka wake zao kisa mwanamke ni mlalamishi na mwanaume anasema nimeshindwa kujua anataka kitu gani na pia nitawezaje kumfurahisha maana ni kulalamika tu kila siku.

Usiwe Chronic complainer maana kuwe na jua unalalamika, kusiwe na jua unalalamika.
kuwe na mvua unalalamika kusiwe na mvua unalalamika.
uwe na kazi unalalamika usiwe na kazi unalalamika.
Ukiwa mnene unalalamika ukiwa mwembamba unalalamika.
Uwe na mtoto unalalamika usipokuwa na mtoto unalalamika
Utaishi na nani?
Nani anataka mtu wa aina hii?
Jirekebishe!

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment