Wednesday 18 November 2015

NITAJUAJE NI YEYE?

Uchumba ni mtamu acha kabisa, ila kumbuka ndoa ni kitu halisi!

Yupi anaweza kuwa mchumba halisi ambaye atakuwa mke au mume wako?

Ukizingatia kwamba kuoa au kuolewa ni uamuzi ambao unaweza kupelekea kuwa mtu wa furaha katika maisha yako au mtu wa huzuni na kujuta siku zote katika maisha yako.
Mambo ya msingi kuangalia ni haya:

MAHUSIANO HUWA RAHISI TANGU SIKU YA KWANZA:

Tangu siku ya kwanza nilipojikuta naonana uso kwa uso upendo uliokuwa kati yangu na yeye ulikuwa natural, nilijihisi nimemuona mwanamke ambaye namfurahia kila kitu, namkubali kama alivyo, nilihisi kama tulizaliwa tuishi pamoja na sasa nimempata mtu ambaye nimekuwa namtafuta, nilijiona atanitosheleza kimwili na kiroho, ninapoongea naye naridhika kwa mvuto alionao.
Kila kitu katika mahusiano na urafiki wetu kilikuwa natural na kutupa hisia mpya kabisa hapa duniani.

Wapo ambao katika safari ya uchumba hadi ndoa hufikia kuzipiga na kugombana mara nyingi sana, leo wanazipiga au kununiana au hugombana na kesho wanapatana tena na kurudiana.
Wanaendelea na kasheshe hizo hizo mara kwa mara hadi wanaoana.

Inawezekana unarudiana naye labda kwa kuogopa ukiachana naye hutapata mtu mwingine wa kuoana naye, au umri unaona umeenda sana, au unataka kuondoa nuksi ili na wewe ujulikane uliolewa, au rafiki zako watakucheka au una hamu sana na sex, Kumbuka ni busara kuachana wakati wa uchumba kuliko kuachana ikiwa ndoa.
Ukiingia kwenye ndoa utakumbana na storm ambayo itakuja kupima kama sababu zako za kuoana zilikuwa strong kuliko storm yenyewe na kama zilikuwa weak storm itakuchukua bila huruma.

UHUSIANO MZURI NA FAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI:

Inaweza kuwa tofauti kidogo hasa linapokuja suala la dini, kabila, nk kwani mara nyingi wazazi na familia nyingi huwa na lao kuhusu kabila au dini.
Ikitokea kwamba mchumba wako ni kabila moja, dini moja na bado ndugu zako, familia yako au marafiki zako hawaelewani naye ni vizuri kufikiria upya.
Wewe umelelewa na familia na kutokana na hayo malezi ndivyo ulivyo na umempata huyo mchumba kutokana na tabia yake aliyokulia au kulelewa na hiyo familia na kama bado hakubadilika maana yake hapo kuna bendera nyekundu inawaka na inaashiria kuna kitu hakipo sawasawa.

Kawaida ukishaingia kwenye mapenzi (fall in love) huweza kupunguza uwezo wako wa kuamua na kuona kasoro ndiyo maana wanasema love is blind.
Hii haina maana kwamba unatakiwa kuvunja mahusiano eti kwa sababu ya ndugu, familia au marafiki hawakubaliani na huyo mchumba wako ila ni kawaida kwamba inawezekana kuna kitu ndugu zako na familia yako wanakiona na wewe hukioni ambacho mbele ya safari mkiwa kwenye ndoa unaweza kukumbana nacho na bahati mbaya umewakana wazazi ndugu na marafiki.
Utaenda kwa nani kuomba ushauri maana umekuwa kichwa ngumu.

Jaribu kuchunguza kile ambacho ndugu zako au familia au marafiki wanasema vibaya kuhusu huyo mtu wako inawezekana ni kweli.
Ni kawaida kama umepata mtu wa kufanana na wewe basi huweza kujichanganya kirahisi sana na ndugu zako, familia yako na marafiki zako.

HUTAONA KITU KIKUBWA CHA KUMBADILISHA:

Kawaida, hata kama mnapendana kuliko binadamu yeyote chini ya jua, bado tofauti ndogondogo zitakuwepo; hata migogoro itajitokeza pia.
Ila kama kuna jambo kubwa sana unaona ni muhimu sana yeye abadilike basi hiyo ni ishara kwamba fikiria kwa makini.

Tatizo ukishashambuliwa na chemicals za love unaweza kujikuta unadhania kwamba haina shida kwa tatizo au kasoro alizonazo na utavumilia.
Ukiingia kwenye ndoa chemistry ya mapenzi hushuka na kupanda kutokana na jinsi mnavyojitahidi kuimarisha ndoa yenu; hapo ndipo sasa utagundua kwamba ulichemka and too late.
Usiingie kwenye ndoa ukidhania utambadilisha mtu sana sana wewe ndo utabadilishwa.
Kama umegundua kuna kitu ambacho ni tatizo kubwa sana mbele ya safari na hutaweza kuishi nacho ni vizuri ku move out kuliko kupoteza muda wako na kujifariji na baada ya miaka 3 ya ndoa ujikute upo kwenye jehanamu yako mwenyewe na upweke uliokithiri.
Watu hupata upweke lakini upweke wa kwenye ndoa ni mbaya kuliko upweke mwinghine wowote duniani.

NI RAFIKI
Mvuto wake ni kitu muhimu sana katika mahusiano.
Ndani ya mahusiano lazima kuwa na mzizi mkuu wa urafiki ambao hata mkiwa wawili sehemu yoyote duniani bado mnajiona hamjapungukiwa na pia bado mnajiona ndiyo marafiki bora duaniani.
Je, unajiona unahitaji kutumia muda na yeye tu?
Je, unajisikia raha kuwa na yeye wawili tu?
Je, unahisi yeye ndiye anastahili wewe kumwambia siri zako na kwamba ni yeye tu anakufahamu kuliko mtu yeyote duniani, kama ni NDIYO, basi mshike vizuri.
Kuwa best friends hata baada ya kuoana ni raha sana, na ndoa hudumu, maana hakuna anaye bore mwenzako.

UNAPOFIKIRIA KUOANA NAYE HAIKUPI SHIDA:

Kama unajikuta unapofikira kuoana naye huna wazo lingine la kuhisi ndoa inaweza kuwa na matatizo na unajisikia amani ya kweli moyoni na kwamba future yako na yeye itakuwa sawa basi umepatia.

Mwisho Kumbuka Kumuomba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mtu wako maana yeye ndiye anajua liubavu lako lipo wapi.

“Marriage is not about finding a person you can live with, it’s about finding the person you can’t live without.”

No comments:

Post a Comment