Tuesday 14 July 2015

MAWASILIANO KATIKA NDOA.

Mawasiliano katika Ndoa ni kama barabara ya njia mbili inayoruhusu magari kuingia na kutoka; yaani wanandoa wawili ambao mmoja akiongea mwingine anasikiliza na mwisho wanapata jibu la kudumu la tatizo lililokuwepo.
Mawasiliano mabovu husababisha kutokuelewana ktk ndoa na mahusiano ya aina yoyote.


Ni kitu cha kawaida kwa sasa kuona mabishano ambayo yanaanza asubuhi jua linaochomoza na kuendelea hadi jua linapozama jioni bila ufumbuzi.


Mabishano kama hayo yasiyo na ufumbuzi ni kama Bomu linalosubiri muda ili lilipuke.


Baadhi ya wanandoa hudhani kwamba kuacha tatizo bila kulizungumzia ni kutatua, hiyo si kweli na hali kama hiyo haileti afya ya ndoa bali ugonjwa na matokeo yake ndoto ambazo mtu alikuwa nayo kuhusu ndoa huyeyuka kama barafu lililokutana na jua la mchana.

Kanuni muhimu katika kuhakikisha ndoa inakuwa imara ni pamoja na kila muhusika kujitoa na kuelekeza jitihada za kuhakikisha kila siku anawekeza ili ndoa kustawi.

jambo la msingi ni kuwekeza katika mawasiliano bora

Mawasilinao katika ndoa au mahusiano yoyote ni kama gundi inayounganisha ndoa.


Na ikitokea hiyo gundi ikaacha kufanya kazi basi mahusiano au ndoa huanza kukatika vipande vipande, na ndoa bila kuwasiliano lazima itakufa.

Katika jamii nyingi za kiafrika watu hawapo wazi sana kujieleza kile anahitaji kutoka kwa mwenzake.

Sema kile unataka bila kuzunguka.

Kama hujaridhika na style za sex za mpenzi wako sema ili ajue unataka kitu kipya, kama hujaridhika na chakula anachopika sema ili msaidiane na kuona inakuwaje, watoto, huduma kanisani maana wengine ni kanisani tu na mambo ya nyumba hana mpango, ndugu, kama hujaridhika na jinsi anavyotumia pesa sema ili ajue.

Kubaki kimya na kudhani atajua mwenyewe hata kama utahuzunika hatakuelewa eleza wazi ili kujenga ndoa yako.

hakuna njia nyingine zaidi ya ninyi wawili kuelewana na kukaa pamoja kupata jibu.

Kama unahitaji kitu Fulani kutoka kwa mwenzi wako sema nahitaji kitu Fulani, na kama kuna kitu Fulani anafanya wewe unaona kinakuletea shida mwambie kwa upole na moyo wa upendo na pia mwambie kwa nini unaona kinakuumiza kubaki kimya ni kama bomu ambalo linasubili muda na muda ukifika litalipuka.


Kama unahitaji muda wa kujibakia mwenyewe tu kufikiria mambo fulani fulani sema ili mwenzako ajue ila si kuwa mkali na kufukuza watu bila kusema kulikoni;

kuna wakati binadamu huhitaji awe yeye mwenyewe na Mungu wake, muhimu mawasiliano.


Huishi na malaika kwamba atajua kila kitu ambacho wewe unapenda au hupendi

Ndoa ni kujengana kila iitwapo leo

No comments:

Post a Comment