Tuesday 14 July 2015

Je, ni umri upi unafaa kwa mwanamke na mwanaume kutofautiana wakati wa kuoana?

Ni kawaida kuona akina dada wengi wakiolewa na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao na pia kwa upande mwingine, tumekuwa tukishuhudia vijana wa kiume wakioa wanawake wenye umri mkubwa kuliko wao hadi kuwa gumzo kwa jamii ambazo hazijazoea kuona hayo.
Kwani masuala ya kuoana mara nyingi yamejikita ktk mila na desturi ambazo sasa zinapata challenge kubwa mno.

Katika hali ya ukweli, Umri ni namba tu na hauna nafasi katika kukusaidia kuwa na ndoa imara.
Wapo wanandoa wenye umri sawa na ndoa hadi zimekalia mabechi ya ICU ya ndoa, pia kuna wengine umri upo sawa na wanaaendelea kujienjoy utadhani wapo paradiso.

Ndoa inategemea kukomaa kwa akili kwa wahusika na upendo wa kweli uliopo kati yao, awe amekuzidi au umemzidi au mpo sawa misingi ya ndoa haijajijenga katika tofauti ya umri bali true love and satisfaction emotionally.

Wanasema love is blind ni kweli mapenzi hayaangalii umri bali mioyo miwili iliyopendana na kuwa mmoja.
Hata hivyo wataalamu wanapendekeza kwamba umri mzuri kuoana unapatikana kwa formula ifuatayo:

Umri wa kuoana = ½ ya Umri wako + 7 (Minimum)
Umri wa kuoana = 2 x Umri wako - 7 (Maximum)

Pia jinsi mtu anavyozidi kuongezeka umri zaidi ya miaka 50 kama unaoana naye na wewe upo chini ya miaka 25 fahamu kabisa kwamba suala la sex na kuzaa watoto uwe makini na umejiweka sawa na mmeongea mkamalizana kabla ya kuingia kwenye ndoa na mtu mwenye umri huo.


No comments:

Post a Comment