Sunday 5 July 2015

MAMBO WANAYOPENDA KUFANYIWA WANAWAKE.

Mapenzi yanataka elimu,lakini si wote wanaojielimisha namna ya kuwafanya wapenzi wao wajione kuwa ni salama na hivyo kuyafanya mapenzi yao kudumu kwa muda mrefu.Wanaume wa siku hizi wamekuwa hawafahamu ni vitu gani ambavyo wanawake wanapenda kuvipata kutoka kwao,,kushindwa kuwa na elimu hii,wanaume wengi wamejikuta wakitumia ukali kuwatawala wake zao,jambo ambalo limekuwa likizidisha migogoro ya kimapenzi.

1: KUTATULIWA MATATIZO.
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo.Mfano ushauri juu ya maisha yao,kulindwa na hatari za kimaisha,kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo.Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili,atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

2: KUBEMBELEZWA.
Wanawake wanapenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni,wengi wao hawapendi kukaripiwa,mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine,Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke ni lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

3: KUWA NAMBA MOJA.
Safari ya penzi la mwanamke haliishii kwenye kumpata na kummiliki,kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba,ni zaidi ya hapo.Jambo lingine ambalo wanawake wengi uhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa.Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukuwa nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla.Wanawake hawapendi kuutwa majina mabaya kwa mfano mjinga,malaya au kuwalinganisha na wanawake wenzao wabaya.

4: KURIDHISHWA KWENYE TENDO.
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani,Ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako.Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.Utndu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.

No comments:

Post a Comment