Tuesday 14 July 2015

MAPENZI NI MATAMU LAKINI PIA NI MACHUNGU.

Ukweli Mapenzi ni Matamu na ni Machungu!

Je, umewahi kumpenda mtu kuliko maisha yako mwenyewe na ukampa kila anachohitaji lakini ukaishia kujuta kwa sababu amekusaliti na kukuumiza?
Sisi sote kwa kuwa tuna hisia tumeshapitia (au tunapitia) katika kuguswa na machungu ya aina hii.
Maisha ni kama fumbo huwezi kujua nani utakutana naye na itakuwaje, kuna watu tunakutana nao na kuachana nao baada ya siku moja, au wiki moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au miaka kadhaa, lakini wapo ambao tukikutana nao hugusa mioyo yetu na kujiona maisha bila wao hayana maana ndipo tunapotoa mioyo yetu na roho zetu kwao hata hivyo huishia majanga makubwa na ukichaa wa ajabu na kuumizwa kusikotamkika.
Kuna swali kubwa ambalo huulizwa na watu wengi kwamba inakuwaje watu wawili mwanaume na mwanamke ambao walikuwa wanapendana pia wakapata watoto, wakajenga maisha pamoja na kuishi pamoja lakini wakaishia katika zogo kubwa la aibu na kutukanana, kuumizana na kuaibishana hadi mahakamani kwa uadui mkubwa?
Hakuna mtu anayeingia kwenye Ndoa akitegemea ndoa kuishia njiani.
Pia hakuna mtu anayeweza kuutoa moyo wake na roho yake ili aishie mikononi mwa mtu atakayemuuumiza na kumtesa kihisia, kiakili au kimwili.
Hata hivyo hasira tunaziona, machungu tunayaona, kudanganyana tunakokuona na wakati mwingine kuuana tunakuona hutokea kwa sababu ya upendo.

Upendo ni kitu kinachofanya maisha kuwa na maana duniani.
Mapenzi ni kiini cha maana ya maisha ya dunia, upendo huweza kuhamisha milima, upendo huweza kudondosha kuta nene na ndefu kwa kuziyeyusha kama barafu.

Hata hivyo ukweli ni kwamba Love is never painless.
Hili halipingiki kwani kila unavyopenda zaidi yule mtu akikuacha basi kuumia kupo.
Wapo watu wamepitia katika kuumizwa na wapenzi wao wa mwanzo na wakipata mpenzi mpya hutoa masharti kwamba tupendane ila usije kuumiza moyo wangu.

Hicho ni kitu kisichowezekana kwani huwezi kupata upendo mkubwa ambao siku ukiachwa huwezi kuumia.
Unavyozidi kupendwa na kupenda mambo yakigeuka kuumia kupo hakukwepeki.

No comments:

Post a Comment