Saturday 11 June 2016

TABIA HIZI WAKATI MWINGINE ZINAKERA KTK NDOA.


Kuna wakati mwanandoa mmoja anajikuta yupo ndani ya ganda la yai kwa maana kwamba anajikuta anakabiliana na mke au mume ambaye anadhibiti, anayeamulisha, anapenda ufyate ulimi, anakukalia kooni, huna hiari yako na anakusimamia kila kitu.


Judy ni mmoja ya wanawake ambao wanatabia ya kufanya auditing hadi chumbani.

Kwanza mumewe huambiwa asahau tendo la ndoa siku za wiki (weekdays), labda Ijumaa usiku au Jumamosi usiku, pia watoto lazima wawe wamelala dakika 90 zilizopita na wawe kweli wamelala fofofo kwa kukaguliwa zaidi ya mara tatu na kuthibitisha kwamba kweli wamelala folilo kabla ya wao kuingia kwenye sita kwa sita.


Mume wake lazima ahakikishe ameoga kwa dakika 30, ahakikishe ametumia sabuni, kitamba (washcloth) na kupiga mswaki, akitumia dakika pungufu ya hizo lazima ataambiwa hajaoga akawa safi (amelipua) hivyo hawezi kupata unyumba (kama una hasira hapa nyumba haitoshi).

Pia mume anatakiwa ahakikishe anatandika taulo sehemu ambayo yeye Judy atalala wakati wa tendo la ndoa kitu kinachofanya eneo la kufanyia mapenzi kuwa dogo.


Anatakiwa kuhakikisha taa zimezimwa wakati wa tendo la ndoa na wanaenda kulala kabla ya saa nne usiku siku ya kupeana unyumba.

Pia kunatakiwa kusiwe na sauti ya binadamu au kitu chochote ndani ya mita 500 vinginevyo hakuna unyumba.

Ni kweli ni muhimu sana binadamu kuwa na taratibu lakini taratibu zingine badala ya kuwajenga wanandoa huwabomoa na kuwa vipande vipanda ambavyo kuvirudisha inakuwa ngumu maradufu.


Mume wa Judy itafika siku atasema “enough is enough”


Jeffy ni mwanaume ambaye kwake kila kitu ni utaratibu, akikwambia anapiga simu saa mbili kamili ni kweli atakupigia saa mbili kamili. Akikwambia atakuwa mahali fulani saa fulani, count him there. Jumamosi anakata majani kuzunguka nyumba yake na Jumapili jioni anaosha gari lake, kwa ufupi shughuli zake zinafanywa kwa mtindo wa saa.


Likija suala la tendo la ndoa na mke wake basi utaratibu wake ni kila baada ya siku tano, penda usipende mwanamke awe anataka au hataki period.

Kutokana na tabia za controlling wapo wanaume wamefanya wanawake kujisikia baridi kali mwilini kila mlango ukigongwa mume anapofika nyumbani kutoka kazini na kumfanya mwanamke kuwa turned off ile jioni na usiku mzima.


Hapa haijalishi umesoma au hujasoma, upo smart au ovyo, tajiri au maskini, kumbuka skills zinazokufanya ufanikiwe kazini kwako wakati mwingine ndo skills zinazofanya ushindwe masuala la chumbani kwako na mke wako au mume wako.

Tabia za kudhibiti na kutaka kila kitu kufanyika kwa umakini wa kupindukia (Control & Perfection) wakati mwingine huharibu mapenzi na ndoa badala ya kujenga.

No comments:

Post a Comment